WARIOBA asema kweli - Hakuna atakayeweza kumfunga Paka kengele

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Kwa aliemsikiliza Jaji warioba atakuwa ameupata ukweli wa hatari inayoikabili Tanzania huko tuelekeako.

Chains au minyororo au tuseme links zile zilizomfanya na kuwafanya CCM waibuke na ushindi kuanzia diwani mpaka Raisi ni mchezo hatari unaoweza kuipeleka nchi katika shida.

Kwa mara ya kwanza kutakuwa hakuna kukosoana wala kukamatana kila mmoja anamwogopa mwenzake maana wizi wa kuiba kura na matangazo yamefanywa shirika.

Wabunge wa CCM hawana faida hata chembe hawawezi kuijenga wala kuibana au kuikosoa serikali na hata kuielekeza pia watakuwa hawathubutu ,ndio tukaona kwa vile hilo haliwezekani ni lazima wawemo wabunge wa upinzani japo mmoja ili aweze kuwa au kutumika kuikosoa na kuipinga serikali kwa nguvu zake zote.

CCM wanaiharibu nchi.
 
Swali kwa mleta habari, nini kifanyike kwa mtazamo na maoni yako?

Sio kutupigia kelele hapa zisizo na tija.
 
Warioba haaminiki tena. Tangu mwanaye Kippi alipopewa uDC akawa mbwa asiye na meno.

PM mstaafu unalalamikia kwenye makongamano? Kwann hataki kum-face Magufuli?

Uchaguzi Serikali za Mitaa 2019 umenajisiwa akakaa kimya. Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020 umelawitiwa kiasi cha kuogofya na matokeo bandia yakatangazwa hakukemea.

Sasa hivi hizi ni lugha za danganya toto tu. Na pengine amepangwa na Magufuli mwenyewe ili ionekane kuna ukosoaji nchini.
 
Chains au minyororo au tuseme links zile zilizomfanya na kuwafanya CCM waibuke na ushindi kuanzia diwani mpaka Raisi ni mchezo hatari unaoweza kuipeleka nchi katika shida.
Hili liko wazi na limesemwa sana na wachambuzi wengi hadi wa nje ya Nchi. Ni ushirika mbaya kabisa kwani yote yaliyofanywa na 'taasisi hizo' sasa yapo hadharani mitaani.
 
Warioba haaminiki tena. Tangu mwanaye Kippi alipopewa uDC akawa mbwa asiye na meno.

PM mstaafu unalalamikia kwenye makongamano? Kwann hataki kum-face Magufuli?
Hapo umeandika nini sasa? Hivi ulimsikia vizuri yule mzee au unaleta ushabiki wa kitoto?
 
Swali kwa mleta habari, nini kifanyike kwa mtazamo na maoni yako?

Dio kutupigia kelele hapa zisizo na tija.

Ww fanya ushabiki, lakini vitendo vilivyovyafanywa kwenye uchaguzi wa juzi ni mambo ya hatari sana. Unapoona mtu mmoja anaagiza taasisi zote za umma kutekeleza jinai sio jambo dogo. Akina Iddi Amin walianza kuchinja watu baada ya kuanza kuchezea mifumo ya nchi na wakafanikiwa, baada ya hapo walienda hatua zaidi, kilichotokea Uganda kilitugharimu hata sisi.
 
Warioba haaminiki tena. Tangu mwanaye Kippi alipopewa uDC akawa mbwa asiye na meno.

PM mstaafu unalalamikia kwenye makongamano? Kwann hataki kum-face jiwe?
PM mstaafu katoa anayoyaona na Magufuli yameshamfikia loud and clear, bila hata ya kuhitaji kudukua simu za waTz.

Yule sio wa kukaa nae pekee yako kisha umwambie asiyoyapenda.
 
Ww fanya ushabiki, lakini vitendo vilivyovyafanywa kwenye uchaguzi wa juzi ni mambo ya hatari sana. Unapoona mtu mmoja anaagiza taasisi zote za umma kutekeleza jinai sio jambo dogo. Akina Iddi Amin walianza kuchinja watu baada ya kuanza kuchezea mifumo ya nchi na wakafanikiwa, baada ya hapo walienda hatua zaidi, kilichotokea Uganda kilitugharimu hata sisi.
Ushabiki uko mahala gani hapo katika mchango wangu tafadhali??
Kwahiyo nimekosea kumtaka maoni juu nini kifanyike huyo mleta mada??
Au nikweli habri hii inamleongo mwingine tofauti na nijuavyo mimi,kwamba tunajenga taifa kupitia hoja zetu??
Unakwama wapi mkuu??

#Nini kifanyike
 
Warioba haaminiki tena. Tangu mwanaye Kippi alipopewa uDC akawa mbwa asiye na meno.

PM mstaafu unalalamikia kwenye makongamano? Kwann hataki kum-face jiwe?
Tutamkumbuka sana Che Nkapa
 
Wapinzani hawakua na msaada wowote zaidi ya kupinga kila kitu. Wapinga maendeleo hawastahili kuwepo bungeni. Wapeleke kelele zao kwenye magazeti mitandao na media zingine. Kama kuna cha maana wananchi na serikali wataona.
 
Ww fanya ushabiki, lakini vitendo vilivyovyafanywa kwenye uchaguzi wa juzi ni mambo ya hatari sana. Unapoona mtu mmoja anaagiza taasisi zote za umma kutekeleza jinai sio jambo dogo. Akina Iddi Amin walianza kuchinja watu baada ya kuanza kuchezea mifumo ya nchi na wakafanikiwa, baada ya hapo walienda hatua zaidi, kilichotokea Uganda kilitugharimu hata sisi.
Huyo alikuwa bado kuzaliwa, sijui kama ataelewa
 
Wazee wetu wametulia tu wakitazama viongozi wetu wakifanya madudu....mfano ndugai anavunja katiba waziwazi viongozi wetu wastaafu wako kimya tu...
 
PM mstaafu katoa anayoyaona na Jiwe yameshamfikia loud and clear, bila hata ya kuhitaji kudukua simu za waTz.
Yule sio wa kukaa nae pekee yako kisha umwambie asiyoyapenda.
Unapoomba apointimenti ili umkalishe umueleze hayo mkiwa wawili uso kwa uso, hakikisha umewaaga familia yako umeandika urithi kabisa.
 
Swali kwa mleta habari, nini kifanyike kwa mtazamo na maoni yako?

Sio kutupigia kelele hapa zisizo na tija.
Japo swali lako umelielekeza kwa mleta mada..si vibaya nikikushirikisha maoni yangu niliyotoa kwenye uzi mwingine:

Back
Top Bottom