security guard
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 799
- 603
Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba Jaji (Mstaafu) Joseph Warioba amekemea vyama vya siasa vinavyoelekea kutafuta Katiba mpya kwa njia ya maandamano na kuwagawa watanzania.
Ametahadharisha kuwa dhana hiyo inaweza kusababisha kupatikana kwa katiba ya kikundi cha kisiasa kinachotafuta maslahi binafsi kinyume cha matakwa ya wengi.
Jaji Warioba ametoa tahadhari hiyo katika mkutano na waandishi wa habari Dar es salaaam wiki iliyopita, huku akivitaka vyama vya siasa kuacha kasumba ya kujitazama vyenyewe badala yake visaidie kujenga umoja wa kitaifa.
"hatutapata katiba kwa maneno ya majukwaani na maandamano, hatutaki katiba ya kikundi cha watu, tunataka katiba ya nchi," amesisitiza Jaji Warioba na kuongeza:
"huu utaratibu wa kuzungumza kwenye majukwaa, vyama vya siasa vnazungumza kwa kujitazama vyenyewe, kinachofanyika sasa kinaweza kuwagawa wananchi badala ya kuwaleta wananchi pamoja"
Habari hii ipo kwenye GAZETI la JAMHURI la leo Jamanne Oktoba 1-7, 2013.