na wewe umetuchosha kama mtoa mada, mnatumiwa na Wazinzibar kuwasaliti Watanganyika kama ilivyo Olesendeka aidha kwa makusudi au kwa kutojitambua wakati wao wanaofaidika kwa serikali mbili wakiwa kimya. Inauma sanaKwa nini warioba anataka kulazimisha matakwa yake aache wajumbe wapime na kuamua kipi chema au kipimhakifai kwenye rasimu yake.
Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.
Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sana. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.
Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo
- Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?
- Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?
Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.
Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.
jee kwa nini Kinana na Nape Nnauye wanawalazimisha wabunge na kuwatisha wakubaliane na mawazo ya kimaiti ya ccm hawawachi wakatumia akili na maarifa yao kupima yaliokuwa mema na muhimu katika rasimu?Kwa nini warioba anataka kulazimisha matakwa yake aache wajumbe wapime na kuamua kipi chema au kipimhakifai kwenye rasimu yake.
Ivi mtu mzima unaposema uongo unapata faida gani?Mimi nimesikia kuwa hotuba yake itakuwa na page zaidi ya 80 ambayo amepanga kuisoma kwa mda wa masaa 8.
Jamaa anajua Ya Moyoni duKujiunga juzi hiyo sio issue kwani watu hapa wana ID tano tano hata wewe ukitaka kujiunga tena kwa jina linguine poa. Ila nimemsifu kitu kimoja anajua hadi yale maneno ya rohoni hatakayoyasema Warioba na akazidi kutabiri bunge litakuwa vp nimempa Big up sana mtoa mada.