Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni

Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni

hata mimi nakushangaa wewe kabla ya Walioba............unaonekana unapima upepo na hiyo kura ya siri inakuumiza sana ila ujue mwisho utafika tu na utabaki kushangaa wewe na si huyo Walioba
 
Kwa nini warioba anataka kulazimisha matakwa yake aache wajumbe wapime na kuamua kipi chema au kipimhakifai kwenye rasimu yake.
na wewe umetuchosha kama mtoa mada, mnatumiwa na Wazinzibar kuwasaliti Watanganyika kama ilivyo Olesendeka aidha kwa makusudi au kwa kutojitambua wakati wao wanaofaidika kwa serikali mbili wakiwa kimya. Inauma sana
 
Kujiunga juzi hiyo sio issue kwani watu hapa wana ID tano tano hata wewe ukitaka kujiunga tena kwa jina linguine poa. Ila nimemsifu kitu kimoja anajua hadi yale maneno ya rohoni hatakayoyasema Warioba na akazidi kutabiri bunge litakuwa vp nimempa Big up sana mtoa mada.
 
Walioba ana haki ya kuzunguza yale anayoona yanafaa kwake kama mtu yeyote alivyo na haki.
 
Kwa akili yako mtu anaetetea kura ya wazi ndie anatetea maslahi ya nchi?mtu anaetetea serikali mbili ndie anatetea maslahi ya nchi?

Kumbe maslahi ya taifa yamebadilika na kua ni kura ya wazi na serikali mbili?uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana,sijui niufananishe na uwezo wa nini,hata fisi anakuzidi kuwaza.
 
Mbona yuko sahihi?!!? Mwenyezi Mungu amsaidie asifanye-editing alichopanga kuzungumza.
 
Kama ni kusikia tu hata mimi nimesikia Warioba atagawa Tablets kwa wajumbe wote!Nawatonya tu kama mleta uzi

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.

Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sana. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.

Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo

  • Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?

  • Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?

Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.

Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.

Watu wanaojua umuhimu wa utaifa na wanaishi kwa matashi waliopewa na Mwenyenzi Mungu hawaishi kwa kuangalia upepo unakwendaje. Watu wanaongalia upepo ni watu waogo na ambao ni vigeugeu hawafai hata kuwa wajumbe wa nyumba kumi. Binadamu halisi husimamia kitu kile anachokiamini kuwa ni sawa hata kama ulimwengu wote utakuwa kinyume na hicho anachoamini. Ilimradi huo ndio ukweli nadhani mwanadamu halisi anapaswa kusimamia hicho. Nitampongeza binadamu yeyote anayeweza kusimamia ukweli hata mbele ya mashetani wasiotaka ukweli. Mtu wa namna hiyo nitamfananisha na Dr. Martin Luther wa Ujerumani.
 
Kwa nini warioba anataka kulazimisha matakwa yake aache wajumbe wapime na kuamua kipi chema au kipimhakifai kwenye rasimu yake.
jee kwa nini Kinana na Nape Nnauye wanawalazimisha wabunge na kuwatisha wakubaliane na mawazo ya kimaiti ya ccm hawawachi wakatumia akili na maarifa yao kupima yaliokuwa mema na muhimu katika rasimu?
Mda mwingi nimekuwa nikieleza kuwa Simiyu Yetu hutumii akili anaposema, badala yake anakariri tu maneno kama kasuku vile. Leo amethibitisha hili.
 
Kujiunga juzi hiyo sio issue kwani watu hapa wana ID tano tano hata wewe ukitaka kujiunga tena kwa jina linguine poa. Ila nimemsifu kitu kimoja anajua hadi yale maneno ya rohoni hatakayoyasema Warioba na akazidi kutabiri bunge litakuwa vp nimempa Big up sana mtoa mada.
Jamaa anajua Ya Moyoni du
 
Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.

Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sana. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.

Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo

  • Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?

  • Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?

Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.

Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.

Ubaya uko wapi ktk hayo mambo mawili uliyodokeza hapo?
MICCM utaijua tu!
 
Mkuu kuna watu ndani ya jamvi hawana jbusara. Hupenda kusikia iwanayopenda kusukia .hao ndio mbumbumbu wa siasa ukweli warioba ni mmoja wa viongozi waliochanganyikiwa.hata alipokuwa pm hakuna alichokifanya kiasi cha mwalimiu nyerere kushutumu kukiThiri kwa rushwa na hatimaye akajiuzuru.ni mmoja ambition ambaye hajui athari za kuvunjika kwa muungano.kwamba hajui licha ya kuwa nchi nyingi zilizovunja muungano zilipata athari gani.hajui madhadhara au athari ya serikali tatu ni nini.anafikiria gharama.lakini hafikiri athari zake.
 
Wewe umesema yako acha naye aseme ya Tume yake; UBAYA HAPA NINI. Wakipiga kura ya wazi nami nitapiga KURA
 
Nikiikumbuka hotuba ya warioba hakika nimeshindwa kumbaliza huyu mzee
 
Back
Top Bottom