warioba kuchafua hali ya hewa bungeni

CCM hawawezi kuiruka hii issue ya serikali 3, wananchi ndio wanataka jamani !!
 
Tatizo lake babu liko wapi? Yeye atawakilisha mawazo ya wananchi ambayo ccm wanataka kuyapotosha hata kumuona mzee WARIOBA hafai. Tatizo la serikari ya ccm haiutaki ukweli na kamwe hawataweza kusema ukweli mpaka walazimishwe.
wananchi wa nchi gani hiyo?? labda kuzimu manake katika pita zangu zote kote watu wanashangaa na kumshangaa warioba kuwa ameyatoa wapi hayo maoni?? mbona wao wanataka serikali mbili?? au moja?? tatu kazitoa kuzimu??
 
unaposema wabunge wana akili timamu,wabunge hawa wanaotukanana Kubwa jinga???
 
Mkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babu

Warioba hajaharibu popote ila ccm ndo mnamhofu kwa kuwa mna nia ovu ya kuteka mchakato kinyume na taratibu, go Warioba go.!!
 
Kabisa kabisa mkuu mimi namshangaa sana mambo mengine anayosema ni uongo kabisa tena wa mchana kweupe.
huyu dawa yake ndogo tu, subiri ayaseme hayo kwanza. tumechoka kuyumbishwa na mtu mmoja, sijui kwann anajipendekeza hivi huyu mzee.
 
Huyu kakurupuku na hisia za woga wa kuogopa atakachokisema Warioba,anajifanya ku-pre empty kwa kuelezea vitu anayoviogopa mleta uzi na asivyopenda Warioba aongelee,Warioba ni mtu huru sana ,mkweli na sio mnafiki,ata ulileta uzi 100 humu jf sidhani kama utaweza kumzuia mzeee Warioba kuongea what he thinks is right.
 
wananchi wa nchi gani hiyo?? labda kuzimu manake katika pita zangu zote kote watu wanashangaa na kumshangaa warioba kuwa ameyatoa wapi hayo maoni?? mbona wao wanataka serikali mbili?? au moja?? tatu kazitoa kuzimu??

Yaani pita zako zote LUMUMBA wewe gamba mmoja huko kijiweni kwako ndo i disqualify maoni ya wananchi wa nchi nzima ambao tume imezunguka kwao kuyakusanya!?you can't be serious.
 
huyu dawa yake ndogo tu, subiri ayaseme hayo kwanza. tumechoka kuyumbishwa na mtu mmoja, sijui kwann anajipendekeza hivi huyu mzee.

Tatizo unayesema hivyo huna jeuri yoyote kwa Warioba, ccm mna jeuri kwa wana siasa njaa lakini sio kwa watu wa type ya akina Warioba, Butiku na sasa kiboko yenu Mamnvi, mtamfanya nini Warioba!? mtamnyang'anya kadi..!?
 
Altiyetoa mada hii ni sisiemu kwa asilimia mia moja.Jaji warioba yuko huru kutoa maoni yake kwa njia yoyote ile.Serikali ya Tanganyika ndiyo itakayofanya muungano huu uwe wa ukweli na imara.Kura ya siri ndiyo itakayowafanya wajumbe wengi(hasa wa chama tawala)kutoa maoni yao kwa uhuru zaidi wakikwepa panga kali la chama.
 
si busara kumdhihaki wala kumbeza Warioba kwa namna yoyote ile, anajua nini kinaendelea kuliko hata JK mwenyewe acheni busara yake itende kazi maana anafanya kwa ajili ya waTZ na si kwa ajili ya CCM.
 
si busara kumdhihaki wala kumbeza Warioba kwa namna yoyote ile, anajua nini kinaendelea kuliko hata JK mwenyewe acheni busara yake itende kazi maana anafanya kwa ajili ya waTZ na si kwa ajili ya CCM.
Unajidanganya kujiaminisha hivyo lakini kwa kuwa ndiyo mawazo yako baki nayo yatakusaidia kwenye mishe zako ila kwenye ujenzi wa jamii mpya hayana nafasi kabisa.
 
huyu dawa yake ndogo tu, subiri ayaseme hayo kwanza. tumechoka kuyumbishwa na mtu mmoja, sijui kwann anajipendekeza hivi huyu mzee.
Huyu analake jambo unavyohaha kana kwamba kunamtu kamtuma alete anayotaka kuyaleta ni vema akawa mkweli kuliko kutunga uongo anaotunga.
 
Mkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babu
Acha zako wewe maridhiano gani ilhali wabunge wa CCM wanafanya yao si tuliyowatuma wananchi??. Tumeshatoa maoni yetu kupitia Warioba leo CCM wanapinga na kulazimisha wabunge wasimamie matakwa yao si ya sisi tuliowatuma kisha unasema maridhiano??? Mtu akimtaka mkeo kwa nguvu akatishia kukufukuza katika nyumba yake uliyopanga, utatafuta maridhiano kwa kumpa mkeo ili maridhiano yawepo??? Kwa taarifa tu wananchi tunamuunga mkono Warioba na tunalaani CCM wanayoyafanya bungeni huku wakila kodi zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…