Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wananchi wa nchi gani hiyo?? labda kuzimu manake katika pita zangu zote kote watu wanashangaa na kumshangaa warioba kuwa ameyatoa wapi hayo maoni?? mbona wao wanataka serikali mbili?? au moja?? tatu kazitoa kuzimu??Tatizo lake babu liko wapi? Yeye atawakilisha mawazo ya wananchi ambayo ccm wanataka kuyapotosha hata kumuona mzee WARIOBA hafai. Tatizo la serikari ya ccm haiutaki ukweli na kamwe hawataweza kusema ukweli mpaka walazimishwe.
Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni
Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.
Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sasa. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.
Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo
Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?
Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?
Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.
Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.
wananchi gani? mbona mnalazimisha? na kwann mna hofu?CCM hawawezi kuiruka hii issue ya serikali 3, wananchi ndio wanataka jamani !!
Kabisa kabisa mkuu mimi namshangaa sana mambo mengine anayosema ni uongo kabisa tena wa mchana kweupe.warioba anazeeka vibaya kama slaa
mkuu hivi mkoroshokigoli maana yake ni nini??unaposema wabunge wana akili timamu,wabunge hawa wanaotukanana Kubwa jinga???
Mkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babu
huyu dawa yake ndogo tu, subiri ayaseme hayo kwanza. tumechoka kuyumbishwa na mtu mmoja, sijui kwann anajipendekeza hivi huyu mzee.Kabisa kabisa mkuu mimi namshangaa sana mambo mengine anayosema ni uongo kabisa tena wa mchana kweupe.
wananchi wa nchi gani hiyo?? labda kuzimu manake katika pita zangu zote kote watu wanashangaa na kumshangaa warioba kuwa ameyatoa wapi hayo maoni?? mbona wao wanataka serikali mbili?? au moja?? tatu kazitoa kuzimu??
huyu dawa yake ndogo tu, subiri ayaseme hayo kwanza. tumechoka kuyumbishwa na mtu mmoja, sijui kwann anajipendekeza hivi huyu mzee.
Kwani serikali tatu ni kitabu cha mungu kwamba hakiwezi kubadilishwa?CCM hawawezi kuiruka hii issue ya serikali 3, wananchi ndio wanataka jamani !!
Unajidanganya kujiaminisha hivyo lakini kwa kuwa ndiyo mawazo yako baki nayo yatakusaidia kwenye mishe zako ila kwenye ujenzi wa jamii mpya hayana nafasi kabisa.si busara kumdhihaki wala kumbeza Warioba kwa namna yoyote ile, anajua nini kinaendelea kuliko hata JK mwenyewe acheni busara yake itende kazi maana anafanya kwa ajili ya waTZ na si kwa ajili ya CCM.
Huyu analake jambo unavyohaha kana kwamba kunamtu kamtuma alete anayotaka kuyaleta ni vema akawa mkweli kuliko kutunga uongo anaotunga.huyu dawa yake ndogo tu, subiri ayaseme hayo kwanza. tumechoka kuyumbishwa na mtu mmoja, sijui kwann anajipendekeza hivi huyu mzee.
Kwahiyo ile akili ya vijana wa bavicha iliyojaa gongo wewe ndiyo unaiona ya maana?Hiv vijana wa ccm kama hugochavez mnakuwaga darasa la ngapi, maana upeo wenu wa kufikiri huwa mdogo sana
warioba anazeeka vibaya kama slaa
Acha zako wewe maridhiano gani ilhali wabunge wa CCM wanafanya yao si tuliyowatuma wananchi??. Tumeshatoa maoni yetu kupitia Warioba leo CCM wanapinga na kulazimisha wabunge wasimamie matakwa yao si ya sisi tuliowatuma kisha unasema maridhiano??? Mtu akimtaka mkeo kwa nguvu akatishia kukufukuza katika nyumba yake uliyopanga, utatafuta maridhiano kwa kumpa mkeo ili maridhiano yawepo??? Kwa taarifa tu wananchi tunamuunga mkono Warioba na tunalaani CCM wanayoyafanya bungeni huku wakila kodi zetuMkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babu
Acha zako wewe maridhiano gani ilhali wabunge wa CCM wanafanya yao si tuliyowatuma wananchi??. Tumeshatoa maoni yetu kupitia Warioba leo CCM wanapinga na kulazimisha wabunge wasimamie matakwa yao si ya sisi tuliowatuma kisha unasema maridhiano??? Mtu akimtaka mkeo kwa nguvu akatishia kukufukuza katika nyumba yake uliyopanga, utatafuta maridhiano kwa kumpa mkeo ili maridhiano yawepo??? Kwa taarifa tu wananchi tunamuunga mkono Warioba na tunalaani CCM wanayoyafanya bungeni huku wakila kodi zetuMkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babu