warioba kuchafua hali ya hewa bungeni

warioba kuchafua hali ya hewa bungeni

wananchi wa nchi gani hiyo?? labda kuzimu manake katika pita zangu zote kote watu wanashangaa na kumshangaa warioba kuwa ameyatoa wapi hayo maoni?? mbona wao wanataka serikali mbili?? au moja?? tatu kazitoa kuzimu??

KUZIMU NAYO NI NCHI? Bahati mbaya hao ccm waliokutuma hawajakupa mbinu wanazotumia kulaghai watu! Nenda ukirudi bila shaka ngalau utajaribu kiasi chake kuwadanganya viziwi na vipofu. Lakini kwa wanaona umechelewe!! Pole sana!!
 
Warioba ni mtoa hoja ambayo ndio rasimu ya pili ya katiba ambayo ndio maoni ya wananchi.....Hicho ndio atakachopresent na ofcourse ni lazima akifafanue kwa kadri ya uwezo wake ili wajumbea waelewe, kabla ya kuijadili hiyo rasimu. Hawezi kukabidhi tu halafu akaondoka ! Lazima afanye presentation pia ! Hilo liko kisheria ndugu yangu na vile vile kwenye kanuni imeshapitishwa kwamba atapresent na hakuna mtu atakayeruhusiwa kumkatiza wakati anafanya presentation !
Eh, kumbe hawaelewi......!
Bora umetufumbua macho katika hili.

Warioba wa ajabu sana pale wilayani kwetu bariad wamehoji kata si zaidi ya tano halafu anasema watanzania wengi wametoa maoni yao sijui kayatoa wapi.

Kwanza hakuna Wilaya inayoitwa Bariadi, tunatambua nyie akina "Simuyu Kwetu" na wengine mpo kwenye Lumbumba Project, ikiwa ni mbinu butu ya kujibu mapigo ya wana CDM, tunamshauri Ndugu Mnawie ambaye ndiyo masimamizi wa Project hiyo aajiri watu wenye uelewa mpana wa kuweza kujenga hoja au kujibu kwa hoja iliyojengeka kujibu mapigo ya wana CDM sio kuajiri mbulula kama huyo inayijiita "Simuyu Kwetu" wakati wala haijui Bariadi ikoje. wameona wasukuma ni wajinga wajinga wa kuwahadaa, Waaambie hutudanganyiki tena.
 
hugochavez naona ulichoandika zaidi ni hisia na utashi wako na wa huyo 'mtonyaji' habari wako! Mzee Warioba anawajibu wa kufafanua kwa vizuri na undani zaidi kile kilichokusanywa na tume yake na wewe huna nafasi ya kumshauri vinginevyo...eti asiongelee kura ya siri au wazi, mara nani atawasemea wanaotaka serikali moja, nne, tano au...
Mzee Warioba hamung'unyi maneno and please let him call a spade a spade and not a hoe! .....No wonder hugochavez died !!! ...and today it is exactly one year and six days since he died March 5, 2013!!!!
 
Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni

Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.

Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sasa. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.

Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo
Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?

Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?

Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.

Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.

Warioba ni mtizamo wake kama yeye, mwache ajisemee mwenyewe ikiwa +ve or -ve, yeye atakuwa katimiza wajibu wake! acahan na mambo ya kuvuruga mchakatao!
 
Umetumwa na baadhi ya watawala ndani ya CCM wamezowea kutoa ahadi kwa wananchi kuwapa 'keki' wakati wao wanataka 'mkate' halafu mwishowe keki yenyewe haipatikani badala yake vinatolewa visingizio kibao.
 
Warioba si mmoja washiriki wa hilo Bunge.....Yeye analeta rasimu kama wananchi walivyoonyesha msimamo....

Baada ya hapo, hao waliopo hapo Bungeni, ndio watakaomua, kukubali maoni ya wananchi au kuridhiana na kuyaacha na kuweka ya kwao !

Warioba anafanya presentation ya mawazo ya wananchi na kuondoka. Kuridhiana au kutokuridhiana kwa wabunge wa bunge maalumu, hakumhusu !

Hayo maridhiano yana nguvu kushinda nguvu ya wananchi na rasimu yao siyo! Kama ni ndiyo basi mchakato ungeanzia bungeni kwanza kabla ya kwenda kwa wananchi.chama kinachochezea hii nchi kilaaniwe
 
Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni

Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.

Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sasa. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.

Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo
Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?

Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?

Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.

Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.

Watu wengine bwana, kama wa..nge vile. Kwa hiyo ukitonywa na huyo basha wako kuwa Warioba anatembea na mama yako utakuja kuweka humu jamvini? CCM hupofusha ufahamu, ni kirusi cha ukimwi ktk mwili wa siasa na demokrasia ya Tanzania. Walioathirika na kirusi hiki huzungumza km mandondocha yasiyoyojua usiku wala mchana. Poleni waathirika wote.
 
Binafsi sioni ulichotonywa maana hayo yote yako mtaani mda mrefu. Hayo atakayoyasema ndo aliyotumwa na aliyeunda tume, Rais wa nchi. Serikali tatu hazikwepeki hata Sitta anajua hilo
 
Warioba wa ajabu sana pale wilayani kwetu bariad wamehoji kata si zaidi ya tano halafu anasema watanzania wengi wametoa maoni yao sijui kayatoa wapi.

Wilaya moja kata sita!Hiyo sampling mbona inatosha kabisa,ina maana kwa wilaya zaidi ya 180 za Tanzania ukizidisha mara tano = kata 900,basi kunauwezekano wa kuwepo coverage kubwa sana,maana wengine walitumia mtandao kuwasiliana na tume na walikutatana na makundi mbalimbali kama taasisi za vyuo vikuu nk.Ngoja wataalam wa research waje kutusaidia
 
Back
Top Bottom