Warioba: Kura ya maoni Aprili ndoto

Warioba: Kura ya maoni Aprili ndoto

Mfikirishi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
8,939
Reaction score
10,403
Nimesoma kwa undani mahojiano ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na gazeti la Nipashe na kubaini kuwa kwa ustawi mzuri na amani ndani ya nchi yetu ni busara tusahau kwa muda masuala yote ya Kura ya Maoni na Katiba Mpya...

Kama kweli nchi yetu ni maskini kama inavyotamkwa na wengi ni bora tukafanya uchaguzi alafu baadaye ufuate mchakato wa Katiba tena kwa kufuata vigezo na masharti si kukurupuka!!

Mimi naomba niongezee "Katiba Mpya Kabla ya 2015 ni Upotoshaji"
Ni aibu kuona kuwa suala la Katiba ya Nchi watu wanalichukulia kirahisi rahisi kama Katiba za NGOs zao tu kule mtaani!!
Tukiendelea kudanganywa na wapiga porojo na wenye mamlaka hii nchi itaishia pabaya!!
TUSIDANGANYIKE!!
=========================

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, ametabiri kukwama kwa kura ya maoni kuhusu Katiba pendekezwa, akieleza kuwa maandalizi hafifu ambayo yamefanyika hadi sasa hayaruhusu zoezi hilo kufanyika.

Aidha, amesema iwapo kutatokea ujanja ujanja wowote wa kutaka kukiuka sheria ya kura ya maoni, nchi itaingia kwenye matatizo.

Akizungumza katika mahojiano na NIPASHE jana, Jaji Warioba alisema wiki iliyopita, wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, walikutana na majadiliano yao yalijikita kwenye maandalizi ya kura ya maoni kuhusu Katiba pendekezwa.

Alisema sheria namba tatu ya mwaka 2014, ambayo inahusu kura ya maoni inaeleza kuwa jambo la kwanza kufanyika ni uboreshaji wa daftari la wapigakura, ambalo utafuatiwa na elimu kwa umma kwa miezi miwili kisha kampeni kwa mwezi mmoja.

"Tukaona kuna umuhimu wa kufanya maandalizi kwa umakini mkubwa kabisa, tumeichambua sheria hii ya kura ya maoni, tumeona mahitaji ya sheria hii lakini utaratibu wa sheria hauanzi mpaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeanza aundikishaji wa wapigakura," alisema.

ELIMU KWA UMMA
Akizungumzia msingi wa elimu kwa umma, Jaji Warioba alisema NEC inapaswa kufanyakazi hiyo kwa kushirikiana na asasi za kiraia kwa kipindi kisichopungua miezi miwili ili kuwaelimisha wananchi nini kilichopo ndani ya Katiba na utaratibu wa kura ya maoni.

"Kwa hiyo tuna miezi mitatu, ratiba iliyowekwa na serikali inasema wanakamilisha kuandikisha Machi kisha kampeni inaanza mara moja. Kipindi cha elimu hakikuwekwa kwenye ratiba. Mimi nafikiri ni vizuri kufuata sheria kwa sababu tukiendesha hii kinyume cha sheria inaweza kuleta matatizo," alisema.

Jaji Warioba aliongeza kuwa: "Na kama tukifuata sheria inavyosema, ni kwamba NEC ikimaliza kazi Machi; Aprili na Mei itakuwa ni elimu, Juni ni kampeni kwa hiyo kura ya maoni itakuwa ni Julai."

Hata hivyo, alisema kura hiyo kufanyika Julai ni matatizo kwa sababu ni wakati ambao maandalizi ya uchaguzi mkuu yatakuwa yameanza na itakuwa kipindi vyama vya siasa vinakuwa vinateua wagombea wake.

"Ukafanye yote kwa pamoja inaweza kuleta matatizo lakini muhimu tunalosema tuifuate sheria kuwepo na kipindi cha elimu kwa umma."

KAMPENI
Alisema sheria hiyo inataka baada ya elimu kwa umma, ziundwe Kamati mbili katika ngazi ya Taifa na ngazi ya jimbo, zitakazoendesha kampeni kwa mwezi mmoja, huku moja ikiunga mkono Katiba pendekezwa na nyingine ikiipinga.

"Kamati ya moja itakuwa inawaambia wananachi wapige kura ya ndiyo na kamati ya pili itakuwa inawaambia waikatae wapige kura ya hapana," alisema.

Alisema kamati zote hizo zitatakiwa kuwa na viongozi wanajulikana na ijulikane mapato ya kampeni yatatoka wapi na wananchi wajue kampeni zitakavyoendeshwa.

"Hizi kamati hazijaundwa na ni lazima ziundwe na ziandikishwe kwenye tume ya uchaguzi," alisema.
Jaji Warioba alisema maandalizi hayo hayajafanyika na haijulikani itafanyika lini na kwa namna gani.

UBORESHAJI WA DAFTARI
Alisema NEC inatumia utaratibu wa kuandikisha wapigakura kwa njia ya kielektroniki (BVR), ambao alisema ni mzuri na unaoweza kuzuia udanganyifu.
Alisema utaratibu wa BVR unafuta wapigakura wadanganyifu ambao wamekuwa wakijiandikisha zaidi ya mara moja, lakini NEC italazimika kufanya uhakiki baada ya kumaliza kuandikisha wapigakura.

Alisema uandikishaji huo ulitumika Malawi mwaka 2004, lakini uliibua malalamiko kwa kuwa wakati wa uandikishaji serikali ya nchi hiyo haikupata muda wa kuhakiki taarifa za wapigakura.

Alisema mfumo wa BVR unafuta majina ya wapigakura watakaojiandikisha zaidi ya mara moja na kubakisha jina kwenye kituo atakachokuwa amejiandikisha mara ya kwanza, hivyo ili kuepuka malalamiko hayo hata hapa nchini ni vyema uhakiki ukafanyika.

"Ukitumia utaratibu huu, ukimaliza unatakiwa uhakiki, bandika vituoni kila mtu aone. Ambaye hataona jina lake mfumo huo utamwonyesha jina lake lilipo," alisema.

Alisema zoezi la uandikishaji unaofanywa sasa na NEC linawahusisha pia vijana watakaoshiriki uchaguzi mkuu ambao ifikapo Oktoba watakuwa wametimiza miaka 18.

"Ukiwaandikisha sasa hivi, wakijakupiga kura ya maoni watakuwa hawajafikisha miaka 18, usipowaandikisha sasa hivi, ikifika Oktoba hawatakuwa na haki ya kupigakura, tukaona hilo tatizo kwa hiyo tunaona maandalizi yafanywe," alisema.

Alisema bila kufanya maandalizi, kunaweza kuwa na wapigakura wasio na sifa au wanaweza wakakwama kushiriki uchaguzi mkuu.

Serikali imepanga kura ya maoni kufanyika Aprili mwaka huu, ingawa makundi mbalimbali ya jamii yanaeleza wasiwasi kwamba kutokana na maandalizi hafifu, uwezekano wa kufanyika kwa kura hiyo ni mdogo.

Baadhi ya mambo yanayohojiwa ni kutosambazwa kwa nakala za Katiba inayopendekezwa kwenda kwa wananchi ili waisome na kuielewa Katiba inayopendekezwa kabla ya kuipigia kura kuikubali au kuikataa.

WANANCHI VUNJO
Alisema kuhusu wananchi wa Vunjo, mkoani Kilimanjaro ambao wamemchangia ili akawape elimu ya Katiba, alisema wajumbe wa iliyokuwa tume yake wataendelea kutoa elimu kwa kutumia rasilimali na uwezo usio na mashaka na usioegemea upande wowote.

"Sisi tunafanya, lakini moja ambalo tuko makini kabisa hatutaki kuonekana tunaungana na kundi lolote. Tunasema tukiwa na uwezo tutaendelea kutoa elimu lakini uwezo ule ni uwezo ambao hauna mashaka, hatutaki kuonekana tunajiunga na kundi lolote," alisema.

Chanzo: Nipashe
 
Duuh, CCM walizarau ushauri wa huyu mzee, lakini kwa kadri siku zinavyozidi kwenda, kile alichokisema naona kama kitaenda kutimia,,!! Na ikiwa hivyo, sijui itakuwaje?

Aibuu
 
Duuh, CCM walizarau ushauri wa huyu mzee, lakini kwa kadri siku zinavyozidi kwenda, kile alichokisema naona kama kitaenda kutimia,,!! Na ikiwa hivyo, sijui itakuwaje?

Aibuu

Huyu mzee ndio chanzo cha matatizo mengi yanayoikumba ccm kwa sasa. Alitaka kutimiza azma ya chuki yake kwa Mwalimu.
 
Huyu mzee ndio chanzo cha matatizo mengi yanayoikumba ccm kwa sasa. Alitaka kutimiza azma ya chuki yake kwa Mwalimu.

Hivi mtu kama mimi nikitoka nikakwambia wewe ni mlopokqji usiyejua unacholopoka utasema nimekutukana? Hivi chama cha mapinduzi na hili taifa ni kipi bora kwako? Hivi mzee WARYOBA na NYERERE walitofautiana lini?

eti anakiharibu chama? chama ni nini? hivi hujui taifa lako ndio unaweza kujivunia? huu uzubaifu wa akili yako unauleta mbele za watu bila kufikiri kama haukuwa na maana kutuonyesha ulivyo mjinGA...

Jana wakati unasema haya maneno najua ulikuwa na usingizi ebu ukiamka asubui hii utafakari upya.
 
Hivi mtu kama mimi nikitoka nikakwambia wewe ni mlopokqji usiyejua unacholopoka utasema nimekutukana? Hivi chama cha mapinduzi na hili taifa ni kipi bora kwako?

Hivi mzee WARYOBA na NYERERE walitofautiana lini? eti anakiharibu chama? chama ni nini? hivi hujui taifa lako ndio unaweza kujivunia? huu uzubaifu wa akili yako unauleta mbele za watu bila kufikiri kama haukuwa na maana kutuonyesha ulivyo mjinGA...

jana wakati unasema haya maneno najua ulikuwa na usingizi ebu ukiamka asubui hii utafakari upya.

Huna maono, achana na mimi.
 
Sidhani kama Warioba ana lolote la maana. Keshamaliza majukumu yake kuhusu Katiba NA Tume kuvunjwa akae pembeni. Anataka nini huyu mtu ambaye aliwahi kuwa Waziri mkuu. Tumkumbuke kwa lipi alipokuwa Waziri mkuu alilowatendea Watanzania.

Kila kitu na wakati wake na mahali pake. Ukienda Msikitini au kanisani lazima uendane na mahali hapo. Ukikutwa unakula Chakula chooni una walakini hapo si mahala pake.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba amesema, kura ya maoni ya katiba pendekezwa iliyopangwa kufanyika April 30 itakuwa ngumu kufanyika kwa vile muda wa elimu kwa wapiga kura hautoshi.

Amedai kisheria zinatakiwa siku 60 za elimu na siku 30 za kampeni.

Kutoka magazetini.
 
Hakuna kushiriki kwny upuuzi wao huo.Kwanza kwani katiba pendekezwa ipo? si yapo mautumbo ya 6 na chenge na vilaza wote waliobaki kwaajili ya posho pale Dodoma.SHAME
 
Kufanya mambo hovyo hovyo ndo imeshakuwa jadi ya Serikali yetu. Mungu atatunusuru tu.

Nawahurumia sana Watz wenye uelewa wa mambo jinsi wanyoumia ndani ya mioyo yao wanapoona mambo yanavyopelekwa pelekwa. Ni huzuni na stress kubwa.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba amesema, kura ya maoni ya katiba pendekezwa iliyopangwa kufanyika April 30 itakuwa ngumu kufanyika kwa vile muda wa elimu kwa wapiga kura hautoshi.

Amedai kisheria zinatakiwa siku 60 za elimu na siku 30 za kampeni.

Kutoka magazetini.
Kwani elimu kwa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu inatolewa kwa utaratibu gani?
 
Hakuna kushiriki kwny upuuzi wao huo.Kwanza kwani katiba pendekezwa ipo? si yapo mautumbo ya 6 na chenge na vilaza wote waliobaki kwaajili ya posho pale Dodoma.SHAME
Nyie mkisusa, sisi twala
 
Kwani elimu kwa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu inatolewa kwa utaratibu gani?

Mbona unajitoa ufahamu kwenye mambo ya msingi. Hapa linazungumziwa suala la kura ya katiba mpya kwa kuzingatia sheria iliyowekwa na bunge ya mabadiliko ya katiba, wewe unaongelea uchaguzi mkuu.

Hata hivyo uchaguzi mkuu una elimu kwa wapiga kura? Nyie ndio mnaofanywa watanzania kila siku kuwa na mawazo mgando. Think out of the BOX mkuu, don't be narrow minded
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba amesema, kura ya maoni ya katiba pendekezwa iliyopangwa kufanyika April 30 itakuwa ngumu kufanyika kwa vile muda wa elimu kwa wapiga kura hautoshi.

Amedai kisheria zinatakiwa siku 60 za elimu na siku 30 za kampeni.

Kutoka magazetini.

Watabadili tu tarehe ili kukidhi hayo matakwa ya siku...inaweza kufanyika may 2015
 
Hakuna kushiriki kwny upuuzi wao huo.Kwanza kwani katiba pendekezwa ipo? si yapo mautumbo ya 6 na chenge na vilaza wote waliobaki kwaajili ya posho pale Dodoma.SHAME

kata yetu imepokea nakala 900 zinazogawiwa kwa makundi mbalimbali
 
Back
Top Bottom