Warioba,maneno haya ya Nyerere hata ungekesha serikali tatu ni ndoto za ali-nacha

Warioba,maneno haya ya Nyerere hata ungekesha serikali tatu ni ndoto za ali-nacha

Taswira

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2012
Posts
1,198
Reaction score
447
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania" - Ukurasa wa 61.
1010332_678415008867133_1699515160_n.jpg

 
Jalibu kufatilia maandiko mengine sio umeliona ilo tu ndio unakurupuka kuliweka humu tena nahisi umeliona kule twitter kwa mjumbe mmoja wa katiba kuna mtu amemtweet!!!!!!
 
Serikali tatu ni laana kwa watakaoibariki, dhambi hiyo itawapukutisha kama ambavyo mti hupukutisha majani wakati wa kiangazi.
 
Mimi hawa jamaa wananichekesha sana, Linapofika suala la Muungano Nyerere anakuwa mungu, Ila kwenye Rushwa, Ufisadi na umasikini Nyerere ni Shetani.

Rushwa ni janga la kitaifa na wala siyo CCM, angalia ndani ya CDM kinachoendelea mpaka uchaguzi usifanyike na kuanza kufukuzana hovyo, ni rushwa tu.
 
Na pia ukumbuke CCM aliyokuwa akiiongoza kupindi chake sio hiii inayojiongoza yenyewe leo, Nyerere angekuwapo leo angejionea hali halisi nina hakika angetumia busara kujibu hili pia angesoma alama za nyakati kama alivyosoma miaka ile na kuachia madaraka "Kun'gatuka"..........huko Zanzibar wameshabadili katiba mara kadhaa, tena bila mashauriano wenzao wabara, unadhani kuna nini tena hapo........Zanzibar inajiona ni Nchi kamili ndani ya Nchi nyingine ya Tanzania, waacheni wakajiamulie mambo yao wameshajifunza mengi nina hakika wamekomaa.
Muungano kwao umeshakuwa koti, umewabana now wanataka kuuvua.........Kumbuka maneno ya Karume.
 
Hivi nyie watu mna nn na huyo Nyerere? Yeye alikuwa Mungu?
Sasa Nape tangu lini akawa na akili? wanamkumbuka Nyerere maji yanapowafika shingoni, kwahiyo huu ufisadi uliojaa serikalini na udini nchini Nyerere Alivibariki hivi? haya Nape tupe aya ya Nabii Nyerere aliporuhusu ufisadi
 
hatutungi katiba ya CCM wala katiba ya Nyerere.

tunatunga katiba ya watanzania wote.

hivi ni lazima kujivua ufahamu ili kuwa mwanaccm??
 
"CCM si baba wala mama yangu..." - Julius Kambarage Nyerere

Kwa maana nyingine sio kwamba kila mara mawazo ya CCM yatakuwa sahihi ikiwemo hili la mgawanyiko wa serikali.

Maneno ya Nyerere sio sheria na lazima watu watambue kuwa huo ulikuwa ni muono au mtazamo wake tu.

Kama ni kuiua Tanzania basi CCM chini ya uongozi wa Nyerere ndio walikuwa wa kwanza kufanya hivyo siku walipoiunganisha Tanganyika na Zanzibar...

Yaani kwa maana nyingine siku ambayo Tanzania inazaliwa ndiyo siku Tanzania ilipouawa..
 
Hili ndilo tatizo kubwa tulilonalo - sio CCM, si CDM wala si CUF.

Katika mfumo wa vyama vingi, suala la muungano na hata idadi ya serikali, lisingepaswa kuwa ni suala la sera ya chama cha siasa. Hayo ni mambo ya msingi ambayo yanahitaji mustakabli na maridhiano ya kitaifa bila kujali wenye vyama na wasio na vyama wala ni chama gani cha siasa kipo madarakani. Tukiendelea kuacha jambo hili likawa ni sera ya vyama nchi yetu itayumba sana.

Leo CCM ipo madarakani inataka nchi iwe na serikali mbili na hawaamini katika muungano wa hiari, kesho CDM ikiwa madarakani itataka tuwe na serikali tatu, wanaamini katika muungano wa hiari, keshokutwa wakiingia CUF watataka muungano wa mkataba, wanaamini katika muungano/mkataba wa hiari.

Kama wazalendo, tunapswa kuweka sera na maslahi ya vyama ama makundi yetu kando linapokuja suala la msingi la kitaifa, hasa KATIBA. Warioba mwishoni mwa hotuba yake alisema maneno mazuri sana namna tume yake ilivyofikia maamuzi wakati wa kutengeneza rasimu ya katiba. Alisema wajumbe wa tume walikuwa na misimamo yao ambayo mingine ilikuwa inakinzana. Lakini waliweza kuweka misimamo hiyo kando na kutanguliza maslahi ya taifa. Alisema, wajumbe wote walikubaliana na kila kifungu katika rasimu ya katiba. Na la muhimu sana ni kuwa, katika kufikia maamuzi yao, hakuna hata mara moja ambapo walifanya maamuzi kwa kupiga kura. Hili ni la muhimu sana kuzingatiwa katika bunge hili la katiba. Kulikuwa na mjadala wa kura ya siri au ya dhahiri - haukuisha! Wabunge/wajumbe wajaribu kutafuta muafaka wa kitaifa badala ya kufikiria sera za vyama vyao.

Tume ya Warioba imefanya kazi nzuri sana. Bunge la katiba lisiharibu kazi hiyo nzuri. Hata kama rasimu itafanyiwa marekebisho makubwa, lakini cha muhimu iwe ni kwa maslahi ya taifa/watanzania na si vyama vya siasa. Kwa sehemu kubwa, wajumbe wa Zanzibar ndio wenye nafasi kubwa ya kuamua muelekeo.
 
^^
Taifa gani linaloishi katika nyakati zisizo badilika?
^^
 
Tatizo la CCM bado wanadhani wanayo hakimiliki ya kufikiri kwa niaba ya Watanzania. Bado wanadhani ni mawazo yao tu ndio yanapaswa kuwa. Nyakati zimebadilika, na hamuwezi kushindana na nyakati....
 
Mimi hawa jamaa wananichekesha sana, Linapofika suala la Muungano Nyerere anakuwa mungu, Ila kwenye Rushwa, Ufisadi na umasikini Nyerere ni Shetani.

Well said mkuu.
Aina muungani siyo biblia au msahafu kwamba hatuwezi kuwa dynamic kuendana na matakwa ya watu, nyakati na mazingira.
 
Serikali tatu ni laana kwa watakaoibariki, dhambi hiyo itawapukutisha kama ambavyo mti hupukutisha majani wakati wa kiangazi.
Toeni solution ya kero za muungano chini ya serikali 2 sii kuung'ang'ania tuu halafu kila mwana ccm anasema kero zitafutiwe ufumbuzi.Imekuaje zanzibar ikawa nchi?ikawa na katiba yake?bendera yake?ikawa na amiri jeshi wake?
 
Ukiona mwanadamu anakuja humu ndani kwa kinga ya Nyerere utajua kaishiwa hoja.
Nikwambieni kwa dhati kabisa, Kama mwalimu angekuwa hai asingekubali huu muundo wa serikali mbili.
Mwalimu alituachia nchi moja yenye serikali mbili lakini leo tunanchi mbili zenye serikali mbili.

Jamani acheni kumtumia Nyerere vibaya! Mbona azimio la arusha mlivunja,rushwa,ufisadi! Vyeo vya kifalme acheni kabisa hatutakubali
 
Rushwa ni janga la kitaifa na wala siyo CCM, angalia ndani ya CDM kinachoendelea mpaka uchaguzi usifanyike na kuanza kufukuzana hovyo, ni rushwa tu.

Hivi we ndugu unatumia upande gani wa akili kuilinganisha cdm na uongozi wa nchi hii ya tanzania? Hivi unajua kuwa cdm ni kipande kidogo sana cha nchi kilicho amua kujitambua kutoka ktk bahari kubwa ya wenye madaraka ya nchi hii? Eti rushwa ya cdm!!, unaweza kulinganisha cdm na serikali ya nchi hii kwa rushwa? RUDI SHULENI.
 
CCM mlikuwa wa kwanza kupuuza na kubomoa misingi ya taifa,,, Nyerere aliacha serikali mbili katika nchi moja nyie mmechakachua sasa ni serikali mbili nchi mbili!!! Msitafute mchawi, wachawi ni nyie wenyewe, alichofanya warioba ni kuweka mambo wazi,,,,
 
Back
Top Bottom