Warioba na muundo wako wa muungano.

Infopaedia

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
1,231
Reaction score
1,491


Mimi bado najiuliza, mathalani kipindi kile huyu mzee mwenye kifimbo bado yupo. Halafu huyu jamaa aliyejishika kiuno kushoto angepewa kazi kama aliyopewa karibuni ya kukusanya maoni ya rasimu ya katiba mpya. Hivi kweli kwa pose hili, hata kama asilimia mia ya watoa maoni wangetaka muungano wa serekali tatu, kweli huyu jamaa angempelekea mwalimu rasimu ya serekali tatu!!!!? Najaribu kupata picha ingekuwaje lakini sipati kabisaaaa. Labda munisaidie, kwa kuzingatia hii photo ingekuwaje wakuu?
Kilichoniumiza mimi ni allowance walizokuwa wakilipwa. Juzi nimemsikia mwenyekiti wa jukwaa la katiba akisema kuwa, jamaa walikuwa wakilipwa mpaka ''risk allowance''. Jamani jamani, yaani nyie kuja huku 'sitimbi maji kumkamuwa chura' ni risk kwenu. Sasa sisi tunaoishi huku ndiyo mnataka kutuambiaje! Au sijaelewa dhana nzima ya hiyo ''risk allowance''!!! Kibaya zaidi wanaharakati wana wa-prove wrong kwa kutumia takwimu zenu hizohizo ambazo mmetumia kuhalalisha serekali tatu. Nashindwa kuelewa hizi Tanzania shilingi 35,000,000,000 ndiyo zimefanya kazi hii au zilienda kwenye kazi nyingine!!!!?
 

Sasa umeandika kitu gani? Soma kwanza rasimu ya pili alafu ndio uje na hoja zako. Mwl. Nyerere mnamsingizia bure, hakuwa na mawazo mgando kama nyinyi. Kama angekuwepo hadi leo angekuwa wa kwanza kukubali muungano wa muundo wa shirikisho wenye serikali tatu. Tatizo mnakiririshwa hoja msizozijua.
 
Kwa lugha yako nimeandika kwamba, Warioba kawawekea watanzania maneno midomoni. Hapo je? Na kwa taarifa yako. Katika hii mifumo tunaanza na 3, 2, halafu 1. Usiniambie Nyerere angerudi nyuma kwenda 3. Ningemchana kama ninavyochana.
 
Hivi wewe wajua maana ya research? Wawezaje kwenda site kutafiti ukimwona chura unamwita samaki? Warioba kaandika wanachokitaka wananchi na kusema kawawekea maneno mdomoni wewe ndo ulowekewa na hao ccm wasiosoma katikati ya mistari ya kilichoandikwa kwenye rasimu ya pili. Jipe muda uisome neno kwa neno kisha urudi hapa kutengua shutuma zako kwa jaji warioba.
Tume imefanya vema sana kwa kutuonyesha usanii wa kinachoitwa muungano wa nchi zisizokuwepo kama Tanzania bara ambayo sijui ipo wapi. Tuache kupotoshana kwani Tanganyika ilikwenda wapi?
Kuhusu posho tume haikujipangia bali walipewa kwa kazi hiyo. Ulitaka waitumieje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…