Infopaedia
JF-Expert Member
- Oct 28, 2011
- 1,231
- 1,491

Mimi bado najiuliza, mathalani kipindi kile huyu mzee mwenye kifimbo bado yupo. Halafu huyu jamaa aliyejishika kiuno kushoto angepewa kazi kama aliyopewa karibuni ya kukusanya maoni ya rasimu ya katiba mpya. Hivi kweli kwa pose hili, hata kama asilimia mia ya watoa maoni wangetaka muungano wa serekali tatu, kweli huyu jamaa angempelekea mwalimu rasimu ya serekali tatu!!!!? Najaribu kupata picha ingekuwaje lakini sipati kabisaaaa. Labda munisaidie, kwa kuzingatia hii photo ingekuwaje wakuu?
Kilichoniumiza mimi ni allowance walizokuwa wakilipwa. Juzi nimemsikia mwenyekiti wa jukwaa la katiba akisema kuwa, jamaa walikuwa wakilipwa mpaka ''risk allowance''. Jamani jamani, yaani nyie kuja huku 'sitimbi maji kumkamuwa chura' ni risk kwenu. Sasa sisi tunaoishi huku ndiyo mnataka kutuambiaje! Au sijaelewa dhana nzima ya hiyo ''risk allowance''!!! Kibaya zaidi wanaharakati wana wa-prove wrong kwa kutumia takwimu zenu hizohizo ambazo mmetumia kuhalalisha serekali tatu. Nashindwa kuelewa hizi Tanzania shilingi 35,000,000,000 ndiyo zimefanya kazi hii au zilienda kwenye kazi nyingine!!!!?