WARIOBA,niambukize BUSARA na UJASIRI

kensh

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2012
Posts
527
Reaction score
113
Nilimsikiliza,alitulia,akasema bila kumung'unya maneno wala kupepesa macho.Alinikonga moyo hakika.ALIFUNIKA!

Hawakutegemea kama angewachinjia baharini kiasi kile,walidhani angejitia ktk siasa za kitoto zile za kusujudu maoni ya mwenyekiti.Alionesha maana ya kuwa mzee,aliukubali uzee,hakutaka kuitwa bebi kama lile lililomuopoaga Lulu.

Aliyasema yaleyale tuliyoyataka sisi tuliomtuma,tulimwambia akaseme tunataka serikali 3,hakutuangusha hata kidogo.

Mzee alionyesha ujasiri,alinifanya niutamani uzee,hasa ule kama wake,yaani ule uzee unaomfanya mzee awe na hamu ya kuwa rejea bora ya jamii yake.Hakujari wana ccm wangemuonaje.HAKUJARI WALA KUOGOPA!

Hakuzingatia yaliyompata Mansoor yule wa Zenji,aliyetimuliwa uanachama wa ccm kwa kuiota Tanganyika huru na Zanzibar huru.

Mzee Warioba,niambukize UJASIRI
 
Kweli mzee Warioba amejaa busara sana,tofauti na wenzake wa CCM waliojaa fitna na uzandiki
 
^^
Busara hujengwa na wewe mwenyewe haitumwi kama bluetooth, ujasiri huwa na sababu nyuma yake
^^
 
Ya ni vizuri kuwa na role models km warioba wakutosha ktk kamili. Viongozi km hao ni nadra sana kuwapata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…