Warioba: Tulipoingia madarakani na Rais Mwinyi mwaka 1985 tuliikuta nchi haina fedha za kigeni!

Warioba: Tulipoingia madarakani na Rais Mwinyi mwaka 1985 tuliikuta nchi haina fedha za kigeni!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Makamu wa Rais na Waziri mkuu mstaafu mzee Sinde Warioba amesema mzee Mwinyi alipoingia madarakani kama Rais mwaka 1985 na yeye kuwa msaidizi wake walikuta nchi haina kabisa akiba ya fedha za kigeni.

Warioba amesema hii ilitokana na ukweli kwamba nchi ilikuwa imetoka kwenye vita ya Kagera pia palikuwa na uhaba mkubwa wa mafuta.

Warioba amesema hayi kwenye mdahalo wa kumbukizi la Edward Moringe Sokoine unaofanyika chuo kikuu cha kilimo SUA.

Source: TBC
 
Halafu kuna watu wanasema Mzee Mwinyi hakufanya lolote la maana.

Mama zetu walikuwa wanavaa vitenge vya kupika. Kulikuwa na viatu fulani vinaitwa “Asante Salim” vya kitambaa.

Tulikuwa choka mbaya.
Na hivyo Vitenge na Viatu vilitakiwa vitengenezwe na "Wajomba" zetu wa Ulaya watuletee?.
 
Halafu kuna watu wanasema Mzee Mwinyi hakufanya lolote la maana.

Mama zetu walikuwa wanavaa vitenge vya kupika. Kulikuwa na viatu fulani vinaitwa “Asante Salim” vya kitambaa.

Tulikuwa choka mbaya.
Sijui Kama Mataga walikuwa wamezaliwa,Wanda zilikuwa zinapikwa kwenye Rangi,ndipo vinapatikana vitenge vilikuwa vinaitwa MASANTULA.
 
Kila raisi Alie ingia madarakani aliweza kukutana na changamoto zake, kuanzia kwa Mwalimu mzee mwinyi mkapa kikwete na huyu mama.

Ila aliekutana na changamoto kubwa nadhani Ni mzee mwinyi kwa mujibu wa historia.

Mwalimu aliingia kwa changamoto nyingi ndio maana hata kupata matokeo tarajiwa kwake kuligubikwa na mengi ndio maana mwinyi nae akapata kuingia na kuanza kwa shida nyingi na mpaka pale alipoishia.

Sio vyema kumcheka kila kiongozi kwa Yale yanayo onekana mabaya Bali yawe changamoto kwetu kwamba walikosea vile na sisi tuende tofauti, lengo Ni kufika palipo na uafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sera za ujamaa uchwara ndizo zilizoichakaza na kuifanya nchi fukara
Nchi ilikuwa kwenye majaribio ya sera ya ujamaa.Ni bora tungeenda na sera za ukoloni za uchumi tungekuwa mbali.Sio KILA kitu cha mkoloni kilikuwa kibaya tungeyachukua mema yao
 
Sera za ujamaa uchwara ndizo zilizoichakaza na kuifanya nchi fukara
Kuna waafrika wenzetu wengi waliamua kuwa mabepari na mpaka leo wamechoka pengine kuliko sisi.

Malawi ya Kamuzu Banda ilikuwa ni tawi la Muingereza mpaka leo wanyasa wamechoka na hawajui lini watakuwa na taifa imara.
 
Back
Top Bottom