Warioba: Wananchi tunaowaita Wanyonge ndio wenye nchi, Katiba ni kipaumbele hata kwenye marekebisho Bungeni

Warioba: Wananchi tunaowaita Wanyonge ndio wenye nchi, Katiba ni kipaumbele hata kwenye marekebisho Bungeni

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Katiba mpya Jaji Warioba amesema wananchi hawa wanaoitwa " Wanyonge" ndio wenye nchi.

Warioba amesema Rais Samia amesimama imara kwenye utendaji wake baada ya kifo cha hayati Magufuli na amekubali kushughulikia suala la katiba mpya.

Jaji Warioba amesema kuna mambo ya katiba ambayo yanaweza kupelekwa bungeni na kufanyiwa marekebisho kama ambavyo sheria ya mawasiliano inafanyiwa ammendmends mara kwa mara.

Cha ajabu tunaambiwa mawasiliano ni " kipaumbele" na sisi tunasema katiba ni kipaumbele.

Mahojiano ya Jaji Warioba yatarushwa jumatatu ITV kipindi dakika 45.

Chanzo: ITV habari

Nawasalimu kwa jina la JMT.
 
Hapa ndipo ujinga wetu waTz ulipo mtu akitaja tu katiba ni lazima irekebishwe tayari wanamuamini.

Huyu warioba kaishi na hito katiba kwa muda mrefu na ameitumikia kwanini hakujiuzuru kuwa katiba haifai?

Werema naye mnafiki tu kwani aliapa kuilinda katiba ileile mbaya,why?

Leo wanajifanya kukosoa katiba iliyopo ni wanafiki na viongozi wengi ni wanafiki ktk hili
 
Hapa ndipo ujinga wetu waTz ulipo mtu akitaja tu katiba ni lazima irekebishwe tayari wanamuamini.

Huyu warioba kaishi na hito katiba kwa muda mrefu na ameitumikia kwanini hakujiuzuru kuwa katiba haifai?..
Afadhali ya Warioba na Werema Wanauthubutu wa KUSEMA KATIBA MPYA ni MUHIMU kuliko KABUDI,POLEPOLE na KIGWANGALA wanaosifia KATIBA ILIYOPO
 
Ili lipo wazi wazee wanataka katiba mpya

Kwa waliyopitia chini ya Magufuli labda uwe taahira tu ndio utakataa katiba mpya.

Huyu mama mwenyewe awashukuru wazee kama warioba ambao alitaka kujiuzulu wakamtaka aache Mara moja pengine sasahivi Rais angekuwa Makonda!

Katiba sio Mali ya ccm wala chadema ni ya watanzania ila Chadema na ccm wanayo haki ya kutumia hoja kushinikiza katiba mpya iweje!
 
Msimamo THABITI wa Mzee Warioba kuhusu madai ya Katiba mpya ndiyo sababu kama Waziri Mkuu Mstaafu hakujumuishwa katika ule msafara wa wastaafu wenye UNAFIKI katika kudai katiba mpya. Mwenyezi Mungu akupe afya njema na maisha marefu ili hivi karibuni ushuhudie matunda ya Tume yako.

Aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Katiba mpya Jaji Warioba amesema wananchi hawa wanaoitwa " Wanyonge" ndio wenye nchi.

Warioba amesema Rais Samia amesimama imara kwenye utendaji wake baada ya kifo cha hayati Magufuli na amekubali kushughulikia suala la katiba mpya...
 
"... ni heri mkawapa wananchi katiba mpya wakati hawaihitaji kuliko kusubiri wakaidai". Haya maneno yamejaa busara na hekima nyingi sana japo sikumbuki yalitamkwa na nani.
Prof wa jalalani. Akiwa mjumbe wa Kamati ya Warioba ya kukusanya maoni ya wananchi. Kabla ya kumezeshwe tonge kubwa na kuvimbiwa na kukengeuka wakiwa na Mr. Slow slow.
 
Nchi ngumu hii,

Watu wanataka kubadili Katiba ambayo hata hawaifahamu ,

Yaani hiyo wanayosema wanataka ibadilishwe ni wachache sana wanaoifahamu kwa mapana yake,

Na ndio hao wanaowadanganya kundi kubwa ambalo haliifahamu vyema.

Kelele za Katiba Mpya zimeanzia Chadema Sasa chadema ndio hao wanyonge??
 
Prof wa jalalani. Akiwa mjumbe wa Kamati ya Warioba ya kukusanya maoni ya wananchi. Kabla ya kumezeshwe tonge kubwa na kuvimbiwa na kukengeuka wakiwa na Mr. Slow slow.
... shukrani Mkuu, johnthebaptist kaniingiza chaka hapo juu! Kumbe aliyatamka yale maneno kipindi kile roho wa hekima na maarifa akiwa juu yake; tangu aanze kushiriki mezani pa waovu roho yule amemtoka ndio hayo tunayoshudia leo kutoka kinywa kile kile kilichoongea kwa busara ya ajabu nyakati zile, leo ni kinyume kabisa!
 
Wameyaona yale maneno ya Mwalimu kuhusu katiba yakitimia kikamilifu mbele ya macho yao kupitia jiwe.
Hapa ndipo ujinga wetu waTz ulipo mtu akitaja tu katiba ni lazima irekebishwe tayari wanamuamini.

Huyu warioba kaishi na hito katiba kwa muda mrefu na ameitumikia kwanini hakujiuzuru kuwa katiba haifai?...
 
Anataka akumbukwe kwenye hili?

Mungu amlinde ataiona tu katiba mpya, ila kama alivyosema mh Rais kwamba, Katiba isubiri basi!!
 
Back
Top Bottom