Warning: Utapeli wa kikundi wanajiita Mo Dewji Foundation

A

Anonymous

Guest
Kuna hiki kikundi wanajiita wanatoa mkopo kwa kupitia MO DEWJI Foundation na wanatumia nyaraka za Mo dewji kinyume na sheria na wana kila kitu hadi leseni za biashara na namba zao za mawasiliano ni hizi +255 780 525 780 tuwe makini na tuwaripoti iwezekanavyo___

MO DEWJI FOUNDATION ipo ndio lakini haijihusishi na utoaji mikopo kama wanavyosema watu hawa

 
Umesema wana leseni, unajuwa maana ya leseni?
 
Wadau kama kichwa cha habari kilivo hapo juu,kuna taarifa inatambaa hiko facebook ya kwamba Mo anatoa mikopo online,sifa kitambulisho chochote kinachotambulika na serikali na hela ya akiba kama dhamana ya mkopo.
Je,sasa nauliza kwa yeyote aliekutana na hiyo kitu mitandaoni au anaefahamu ukweli wowote juu ya jambo hilo anijuze.
 
Watanzania shirikisheni akili mtatapeliwa hadi lini.
Hapa tanzania hakuna mtu anaweza kukopa tu kisa una ktambulisho bila hata kujua anakupata wapi.
 
Matapeli hao
 
Sawa



Sasa kwanini waandishi wa habari wasiende kumuhoji mo mwenyewe ili akaweka sawa hizi taarifa
We utajibu kila kinachoandikwa mtandaoni? Huo utapeli upo muda toka 2010, kulikuwa na halima mdee, kulikuwa na zitto, kulikuwa na anna makinda, kulikuwa na tulia, kulikuwa na nandy supermarket, n.k.
Ni kutumia tu akili kujua kuwa ni utapeli sema watu hawapendi kushirikisha akili yao.
 
....Hivi Kwa Nini hawakamatwi wakati Mo Mwenyewe aliishatangaza kutohusika?? Wana Mpaka kadi ya Kugushi ya Bunge???
 
Haya matapeli yataumiza sana watu yachukuliwe hatua mapema mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…