WARUMI: Global Publisher kwa hili tena hapana hamtendi haki

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Ile ya Mara ya kwanza nimenyamaza kimya sasa ivi tena mkaamua kubeba habari nzima, yaani Mme copy na Ku paste kwenye Gazeti lenu, wakati mnajua habari mmechukua kwangu, mbaya zaidi hata taarifa hamkunipa wala uongozi wa humu sidhani kama wanalijua hili , Naumia kuona jasho langu linaliwa na mtu mwingine tena bila hata kifutia jasho, najua mtasoma apa , kwanzia sasa ivi inabidi niache kuandika thread yeyote hadi nijue hatma na haki Yangu , siwezi nikawa nafanya kazi ya kuwaingizia pesa wengine , Invisible naomba msaada wako kwa hili , GLOBAL PUBLISHER mnavyofanya sivyo , Leo nimeumia sana kwa hili.

Kwa wanajamii forum wenzangu siku kadhaa niliandika thread kuhusu LULU cha kushangaza leo nimeikuta kama ilivyo kwenye gazeti la shigongo. Ushahidi huu apa chin.nadhan mnakumbuka hii habari

 

Attachments

  • 1396525951354.jpg
    55.8 KB · Views: 2,522
Hahahahaaa binamu acha vituko, ni juzi tu hapa umesheherekea hao gpl kuchukua habari yako. Leo unakuja kulalamika haohao kwa kuchukua habari yako, umetishaaaaa
 
Hahahahaaa binamu acha vituko, ni juzi tu hapa umesheherekea hao gpl kuchukua habari yako. Leo unakuja kulalamika haohao kwa kuchukua habari yako, umetishaaaaa

yah ni kweli binamu unavyosema,ila sasa naona imezidi yaani wachukue habari nzima na ku paste kwenye magazeti yao?? hizo habari mimi nahangaika kuzipata ili nizilete humu inanishangaza kuona wenzangu wakijiingizia mkwanja kupitia jasho langu, nikinyamaza na hii watazoea, mwanzo sikujua kuwa nina kiwango kwa kiasi hicho kwenye uandishi, na nimekuwa nikiandika kama burudani na interest, sikujua maandishi yangu yangekuwa dhahabu kiasi hiki, naanza kuiona thamani ya hiki ninachokifanya humu. naomba tu wahusika wajitokeze na kuona jinsi gani tatizo lagu linaweza kutatuliwa.
 
Yaani hii habari nimeikuta kwenye ma blogs mbali mbali nikashangaa sana, siwezi kuvumilia binamu, natumia energry,skills na technique za kiwango, sasa wenzangu wana copy na kujiingizia mkwanja bila jasho huku mwenzao naambulia matusi na kuitwa kila aina ya majina, soo disgusting, natukanwa kwa ajili ya hiki ninachokifanya mimi humu halafu wenzangu wajiingizie mkwanja ivi ivi??. nachukua likizo ya mda nione kitakachoendelea humu.
 
Pole aisee! Bora wakuajiri tu ujue utapewa mshahara kwa habari utazowapelekea
 
inauma sana aisee
kama vp kaandamane ofic za GPL
hiyo itasaidia sana!!
 
Una hati miliki ya habari hii? Inawezekana kupitia habari yako wao waliamua kufatilia zaidi na wakapata zaidi?
Katika hili hakuna wa kukuelewa lasivyo uthibitishe pasi shaka wewe ni chanzo cha kwanza cha hii habari.

Katika hili unawachafua GPL na ni vyema Mhariri uka uhariri huu uzi.
 
Last edited by a moderator:

Siwezi kumchafua mtu bila sababu za msingi, we uwa ufuatilii sana thread zangu, hujui kitu ni bora ukae kimya kuliko kuongea kitu ambacho huna uhakika nacho. Search hii thread LULU MICHAEL soma content nzima halafu compare na hyo screen shot halafu ndo uje uongee humu
 
Last edited by a moderator:
Duh mkaweka front page na maandishi makubwaa duh Global nimewavulia kofia, mlivyokuwa waongo sasa eti chanzo cha karibu na familia ya lulu kililiambia gazeti la amani , duh kwa hiyo Mimi ni nilikuja global kuwaambia hizi habari? Au niliwapigia simu? Si mngesema ukweli tu mmetoa Jamii forum kwa warumi? Au basi ata kunifuata pm angalau mnipooze maana najua humu mnaingiaga sana tena inaweza mkawa member wa humu, sio poa mnavyofanya aiseeh , halafu mnawachonganisha na watu wa karibu wa familia ya lulu wakati hata hamjui nani Kasema hayo maneno.
 

Attachments

  • 1396534717685.jpg
    67.5 KB · Views: 419
Last edited by a moderator:
Reactions: amu
Shukuru umeficha identity yako, la sivyo wangekutoa kwenye OFM kama mgoni, usicheze na hao watu mzee
 
Njoo nikupe msaada wa kishelia utalamba kama mill 20 hiv kwa hilo kaka
 

kwa hiyo unahakika kila unachoandika humu chaukweli? kama hivyo dunia imekwisha....na hongera kwa kufanya kazi kwa weledi
 
kwa hiyo unahakika kila unachoandika humu chaukweli? kama hivyo dunia imekwisha....na hongera kwa kufanya kazi kwa weledi

Search thread imeandika LULU MICHAEL kasome content za hyo thread na hyo screenshot utaona content , siwezi kufanya vitu kama mpumbafu Nina uhakika na ninachokifanya mkuu
 
Wameona unawatafuniaa wao wamezeee tu,usikubaliiii aiseee
 
GPL ni wavivu wa kutafuta habari,wao wenyewe wanakuja tu wanacopy wanabandika kwao,halafu utakuta ndo members hawa hawa wanaocoment humu.
 
Wameona unawatafuniaa wao wamezeee tu,usikubaliiii aiseee

Nimeomba msaada kwa wahusika naona kimya, inabid nichukue likizo fupi kutoa thread maana hadi pozi nimeishiwa binamu
 
Sio hao tu watu wengi wana copy na kupest habari kutoka jf,
siku hizi hawajishughulishi kutafuta habari mitaani wanazitafutia JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…