Warusi wazidi kumpinga Putin. Marekani watoa onyo kali kwa Urusi

Warusi wazidi kumpinga Putin. Marekani watoa onyo kali kwa Urusi

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Katika vita, hakuna jambo baya kama kukosa uungwaji mkono wa watu wako.

Kadiri siku zinavyokwenda, Rais Putin wa Urusi anazidi kupingwa na watu wake. Putin alijiaminisha kuwa vita dhidi ya nchi ndogo ya Ukraine, angeihitimisha ndani ya siku 3, na ndani ya muda huo angekuwa ameiondoa Serikali ya Ukraine na kupachika utawala anaoutaka, kama ilivyokuwa vipindi vilivyopita.

Matokeo yakawa tofauti sana. Vita vikawa vigumu kwake, na baadaye kushuhudia maelfu ya askari wa Urusi wakiuawa. Akaamua kuwatumia wapiganaji wa kulipwa, na baadaye kutoa matangazo nchi nzima kuwashawishi raia kwenda vitani kwa malipo ya sawa na dola 2,700 kwa mwezi. Wafungwa wakatolewa magerezani na kupelekwa mstari wa mbele. Bado mafanikio yake yakawa madogo sana. Baadaye Putin akaishia kuanza kupoteza hata baadhi ya maeneo aliyokuwa ameyateka. Wajinga walioeda vitani kutegemea malipo ya dola 2,700, wakarudi kwenye majeneza, bila kufaidi malipo ta dola 2,700.

Kutokana na kupungua kwa askari, Putin kaamua kutafuta wapiganaji 300,000 kwa nguvu. Hawa ni raia wenye umri kati ya miaka 18 na 60, waliowahi kupitia mafunzo ya kijeshi, kama yale ya JKT hapa nchini petu. Uamuzi huu wa Putin umewakasirisha na kuwatia hofu Warusi wengi, kiasi cha wengine kuamua kukimbia nchi, wakienda mataifa jirani kwa magari, kwa miguu na kwa ndege. Wengine wameamua kuchukua uamuzi mgumu wa kumpinga dikteta Putin hadharani kwa kuandamana. Baadhi wamekamatwa na kupelekwa mahabusi, wakiwa mahabusu wanalazimishwa kusaini kuridhia kuwa wataenda kupigana Ukraine.

Katika majimbo yale aliyoyateka, ambayo wananchi wamelazimishwa kupiga kura bandia waseme wanataka kujiunga na Urusi, tayari watu wanaandikishwa kwenda mstari wa mbele wakapigane dhidi ya ya wananchi wenzao wa Ukraine. Yaani wananchi wa Ukraine wapigane na wananchi wenzao wa Ukraine. Upande wowote utakaopoteza, watakaokuwa wamepoteza maisha na mali watakuwa wananchi wa Ukraine.

Kwa upande mwingine, Marekani imetoa onyo kali dhidi ya Putin aliyetishia kuwa anaweza kutumia silaha za nuclear katika vita hii. Marekani imesema kuwa itachukua hatua kali dhidi ya Urusi kama itathubutu kutumia silaha za nuclear. Marekani imesema kwamba imekwisha iambia Urusi hatua ambazo itachukua.

Vita hivi vitakapomalizika, kuna uwezekano mkubwa wa kulitengeneza upya Taifa la Urusi kwa kuliondoa kwenye siasa za kidikreta zilizoanza tangu enzi za fashisti Stallin mpaka leo, ambazo haziruhusu watu kuhoji utawala. Ni utawala uliotekeleza mauaji ya wapinzani wengi kwa miongo kadhaa.

Marekani imeapa kuwa itahakikisha nguvu za kivita za Urusi zinateketea kiasi cha kushindwa kuwa tishio kwa Taifa lolote. Pamoja na kupeleka silaha nyingi za kisasa Ukraine, na sasa imepeleka mfumo wa kisasa kabisa wa kulinda anga la Ukraine. Silaha za Marekani zenye precision ya hali ya juu dhidi ya silaha za Warusi zenye ubora mdogo, zimekuwa sababu kubwa ya Urusi kutofikia lengo lake.

Vita hivi vimekuwa na madhara makubwa kwa Urusi. Hapo kabla, Urusi iliwekwa kama Taifa la pili kwa nguvu za kivita Duniani, lakini kwa sasa, wataalam mbalimbali wa masuala ya kivita wanahoji na kudai kuwa nguvu za kivita za Urusi huenda zilitiwa chumvi kuliko uhalisia.

========

Ukraine war: Protests in Russia's Dagestan region against new draft

Over 100 people were arrested during protests in the regional capital Makhachkala, OVD-Info, an independent Russian human rights monitor said.

It said it was concerned by reports of the province's "very tough detentions".

Dagestan is a mainly Muslim region of Russia with a higher death toll than any other province in the war.

More than 2,000 people have been arrested at mass protests since Russian President Vladimir Putin announced the partial mobilisation of military reservists on Wednesday.

While large protests have taken place in major cities across Russia in recent days - with more than 700 people being arrested on Saturday alone - the images of Dagestani demonstrators fighting with police marked a rare outbreak of violence against authorities.

Dozens of videos posted to social media showed protesters confronting police and other security officials in Makhachkala, with OVD-Info reporting that officers resorted to using stun guns and truncheons on the crowds.

In one video, a man detained by officials headbutts a police officer, before being beaten by other personnel.

Another video showed a security officer fleeing from a large group of demonstrators, some of whom attempted to grab and trip him as he ran.

Elsewhere, a large group of women confronted an officer guarding a recruiting centre and angrily condemned the war in Ukraine, with one telling the officer that "Russia is on the territory of another country".

"Why are you taking our children," the women shouted. "Who was attacked? Russia was attacked? They didn't come to us. It was us attacking Ukraine. Russia has attacked Ukraine! Stop the war!"

OVD-Info also reported that locals in the village of Endirey had blocked a federal highway, in an attempt to stop security officials seeking to enforce the draft entering the area.

US warns of consequences if Russia uses nuclear weapons

US National Security Advisor Jake Sullivan said on Sunday that the US would respond decisively to any Russian use of nuclear weapons against Ukraine, and that it had spelled out to Moscow the “catastrophic consequences” it would face.

“If Russia crosses this line, there will be catastrophic consequences for Russia. The United States will respond decisively,” Sullivan told NBC’s Meet the Press news programme.

Source: Aljazeera
 
Habari hizi zinaniumiza mimi Mrusi wa Buza, kwani hakuna habari nyingine?

Mtaani niliwaaminisha wamarekani wa Buza kuwa tutawapelekea moto wa Yukreini mpaka waseme wawa badala ya ubwabwa.

Sasa mambo yamebadilika Dejan Mtukazi anamtwanga Ocra Andunje.
 
Ninamuonea huruma Putin kwani kuacha vita ni ngumu na kuendelea nako anaumizwa kila uchao.
Ni jambo gumu kujinasua ukiingia kwenye 18 za US tena iwe siku ya 40 yako
MK254
... way forward kwa sasa ni kumng'olea mbali fashisti na genge lake lote linaoloona Russia kama mali yao na kuweka utawala wa kidemokrasia. Ukisikia jambo limezua jambo ndio kama hivyo!
 
... way forward kwa sasa ni kumng'olea mbali fashisti na genge lake lote linaoloona Russia kama mali yao na kuweka utawala wa kidemokrasia. Ukisikia jambo limezua jambo ndio kama hivyo!
Safi sana
 
sababu ni Marekani, najua unajua, ni vile tu uchawa umekujaa

Marekani anamiliki atomic warheads kadhaa, za nini ? akilimiki Iran au North Korea vikwazo bwelele, kiranja huyo
 
Hizi taarifa za upande mmoja huwa hazina ladha.
Wangeruhusu RT itoe za upande wa pili ili sisi walaji tuone uhalisia.
Vita hii wamarekani wanapigana zaidi kwenye media kuliko uhalisia ulioko kwenye uwanja wa vita.
 
sababu ni Marekani, najua unajua, ni vile tu uchawa umekujaa

Marekani anamiliki atomic warheads kadhaa, za nini ? akilimiki Iran au North Korea vikwazo bwelele, kiranja huyo
Hao uliowataja akili zao ni mbovu wakimiliki hizi silaha hatari wataangamiza wengine bila sababu.
Huoni Iran kila wakati anatamka atamfuta Israel?
Huoni Iran anaua raia wake kisa unuwwle kuchomoza?
Utaruhusuje kichaa kutembea na kisu?
 
Ukuambiwa lete ushahidi wa Urusi kusema atamaliza vita ndani ya siku 3 hautakuanao, zaidi utaleta matusi.
Ukiambiwa lete ushahidi wa ukraine kukombaoa mji upi kati ya miji iliyochukulia hautakuanao zaidi ya matusi pia.

Ukraine aondea majeshi ya wavamizi pale kwake, akiweza atakua ameshinda vita, akishindwa kama ambavyo inaendelea means Ukraine hana huo ubabe.
 
Back
Top Bottom