Wasabato fahamuni kuwa Yesu ndiyo hekalu halisi lililopo mbinguni haiwezekani akaingia kwenye hekalu lake mwenyewe

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wasabato fahamuni kuwa Yesu ndiyo hekalu halisi lililopo mbinguni haiwezekani akaingia kwenye hekalu lake mwenyewe

Wadau hamjamboni nyote?

Mada yangu ni habari ya hekalu la mbinguni na tafsiri yake kama inavyofundishwa na Wasabato

Nabii mke wa Kanisa la Wasabato Duniani alidai Yesu Kristo alihamiaga chumba cha patakatifu pa patakatifu kwenye hekalu la mbinguni!?

Sikusudii kuhoji alichokwenda kukifanya Yesu Kristo huko anakodaiwa kwenda ila hoja ni kweli mbinguni kuna hekalu kama lile la duniani au shida ya Wasabato ni kushindwa kutafsiri maandiko?

Karibuni tujadili

Jumapili njema
 
Kila dini na kila dhehebu lina kasoro na mapungufu yake mengi tu,mana dini ni njia ya mwanadamu kumtafuta mungu.
 
Kwanini msimuabudu tu MUNGU bila majina ya kisabato sijui kikatoliki. Ujinga ujinga tu. Sasa kama dini zote mbili zinaamini YESU ni MUNGU huu unyani wa kupigania usabato na ukatoliki wa nini? Ujinga.
 
Na kweli, hata walivyosema kuwa amri 10 za Mungu hazijawahi kufutwa nyie mnaendelea kushupaza shingo ila cha kushangaza ni kwenye amri mbili tu kutunza sabato na kujifanyia sanamu ya kuchonga

Haya mtu wa Mungu ni wapi kwenye Biblia aliagiza kuwa ujifanyie sanamu kwa kutaka wewe tu siku ukiamka unachonga?
Hao hata yesu wanatamani kumtoa kwenye usäbato tangu Alivyoo waambia mimi ndo bwana wa sabato
 
Kwanini msimuabudu tu MUNGU bila majina ya kisabato sijui kikatoliki. Ujinga ujinga tu. Sasa kama dini zote mbili zinaamini YESU ni MUNGU huu unyani wa kupigania usabato na ukatoliki wa nini? Ujinga.
Mkatoliki linapokuja suala la kumuabudu Mungu hana utengano that's why hukuti ktk mahubiri padre akisema maneno kama ”wale,wao au sisi”.

Ndani ya Kanisa Katoliki zipo hadi sala maalum kwa ajili ya kuombea mshikamano wa kiimani kwa wanaomwamini Kristo kama lilivyokuwa Kanisa la kwanza
 
Mkatoliki linapokuja suala la kumuabudu Mungu hana utengano that's why hukuti ktk mahubiri padre akisema maneno kama ”wale au sisi”.

Ndani ya Kanisa Katoliki zipo hadi sala maalum kwa ajili ya kuombea mshikamano wa kiimani kwa wanaomwamini Kristo kama lilivyokuwa Kanisa la kwanza
Iendelee hivyo na wengine wajifunze.
 
HUELEWI MAANA YA HEKALU.HEKALU LILE LA DUNIANI LILIKUWA MFANO WA HEKALU LA MBINGUNI.JE UNAIELEWA LILE HEKALU LA DUNIANI ILIKUWAJE?KM HUJUI BASI HUJUI HATA YESU YUPO WAPI NA ANAFANYA NINI
 
Wasabato fahamuni kuwa Yesu ndiyo hekalu halisi lililopo mbinguni haiwezekani akaingia kwenye hekalu lake mwenyewe

Wadau hamjamboni nyote?

Mada yangu ni habari ya hekalu la mbinguni na tafsiri yake kama inavyofundishwa na Wasabato

Nabii mke wa Kanisa la Wasabato Duniani alidai Yesu Kristo alihamiaga chumba cha patakatifu pa patakatifu kwenye hekalu la mbinguni!?

Sikusudii kuhoji alichokwenda kukifanya Yesu Kristo huko anakodaiwa kwenda ila hoja ni kweli mbinguni kuna hekalu kama lile la duniani au shida ya Wasabato ni kushindwa kutafsiri maandiko?

Karibuni tujadili

Jumapili njema
Hiyo sio hoja ya wasabato bali ni hoja ya Biblia kitabu cha Waebrania sura 8 na 9. Nenda kasome uelewe usiruke ruke na hoja za kuambiwa. Kazi anayoifanya Yesu ni kazi iliyokuwa inafanywa na makuhani katika agano la kale kama mfano wa kile ambacho Yesu angekuja kutimiza. Ndiyo maana wakati Yesu anakata roho msalabani pazia la hekalu la lilipasuka kuashiria kuwa huduma za mifano zilizofanywa na makuhani zimefikia mwisho na kuhani mwenyewe amekuja kumaliza kazi. Mambo haya wakati mwingine ni vigumu kuyaelewa kwa kutumia akili ya hisabati, fizikia na uraia bali walio na Roho mtakatifu ndio wanaweza kuyaelewa.
 
HUELEWI MAANA YA HEKALU.HEKALU LILE LA DUNIANI LILIKUWA MFANO WA HEKALU LA MBINGUNI.JE UNAIELEWA LILE HEKALU LA DUNIANI ILIKUWAJE?KM HUJUI BASI HUJUI HATA YESU YUPO WAPI NA ANAFANYA NINI
Revelation 21:22 Ufunuo 21:22
[22]And I saw no temple therein: for the Lord God Almighty and the Lamb are the temple of it.
Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.
 
Back
Top Bottom