Wasabato masalia wapaa!!!

Wasabato masalia wapaa!!!

Msongoru

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2008
Posts
306
Reaction score
24
Bado wapo wapo! Ila si hamuamini? ipo siku itakuwa kweli!
 
Wanawapoteza watoto ambao wanatakiwa wawe mashuleni......wanasoma...wale wangewaacha kwanza wasome baadae waje waamue wenyeewe..mustakabali wao...
 
kazi kweli kweli hii,labda mtu ajitolee kuwakatia tiketi.
Huwezi jua kuna mtu anataka kuwa-prove wrong akatoa tiketi ikaonekana kama kwamba WAMEPAA.....!
 
Jamani kama wanaimani ya kweli lolote laweza kutokea(Maana Biblia yasema Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo na ni bayana ya mambo yasiyoonekana), ila nawaonea huruma wale watoto ambao nao wanashinda hapo badala ya kwenda shule.....Mungu atusaidie
 
Kupaa kwenda wapi bila utaratibu? Biblia inasema,heshimuni mamlaka zinazowatawala,mahali pengine biblia inasema nani atakayekujenga mnara asiyekaa chini na kuhesabu gharama? Jamani Mungu wetu ni wa utaratibu. Na ndio maana hata mteule Yakobo baba wa makabila kumi na mbili alikaa ukweni akilima ili alipe mahali kwa miaka kumi na nne.
 
Kaaaaazziiiii kweli kweli kwa wapendwa katika bwana...!
 
Back
Top Bottom