WASAFI BET Tuonyesheni Kodi mnayotukata, na Kwanini Mnatukata 20% badala ya 15%

WASAFI BET Tuonyesheni Kodi mnayotukata, na Kwanini Mnatukata 20% badala ya 15%

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,627
Reaction score
1,926
Wakuu Kwema,

Leo Mapema nilikua nimejisajili kwa Hii Kampuni nione labda ina nini Kipya wamekuja nacho tofauti na Makampuni mengine yaliyoko. Nikasuka Mkeka wangu, treni la leo leo odds kama 384 hivi (ukilitaka hilo behewa hili hapa Online Sports Betting |Best Odds and 2MB App| WasafiBet code Y69FW5T), nikiweka 1300 inaniletea kama 500k hivi, nkasema ngoja tu nione Mikeka ya hawa Wasafi inaendaje, kuonekanaje,yaan sikua serious sana na ushindi, bali kama nai-study tu hii kampuni na menu zao kama wa Customer Care Chat, Turbo/Cash Out, Rebet, Mult-bet Bonuses, Share Bet slips, Codes etc.

Cha ajabu ule mkeka nakuja kuuangalia baadae nakuta ukiwin wote ni TZS 400K, sio tena 500K walizoniletea awali wakati naweka stake. Kuja kupiga hesabu kumbe ile 500k nilioiona awali ilikua ni kabla hawajatoa kodi yao. Halafu cha ajabu nimekatwa 20% badala ya 15% iliyotangazwa na serikali. Huu ni wizi wa kimacho macho, na pengine ndio maana hawaonyeshi kodi wanayokata ili watu wasishtuke.

Mlionao karibu hawa watu waambieni tunataka ufafanuzi kuhusu hili, otherwise ni heri tuendelee kubaki tu huku huku tulikokua awali ambako kila kitu kiko wazi kinaeleweka.
 
Ukingia kwenya kamari kutoka tabu sana unakuwa teja la nguvu .Machina ndio wenyewe kwa kamari imo ndani ya damu yao.
 
Hao wasafi hata ukishinda million 50 hawawezi kukulipa lazima ulie
 
Hizi kampuni ambazo ni mpya sio za kuamini sana!
 
Back
Top Bottom