The hitman
JF-Expert Member
- Nov 30, 2017
- 3,673
- 2,288
Mbona mwanza nyegezi wameitangaza mkuu ?Nadhani ingekuwa vyema kuwa wazalendo kidogo, katika moja wapo ya nyimbo zao wakawa wanachomeka neno Serengeti au hata Ngorongoro, itasaidia sana kiutalii wa ndani na wa nje.
Uzalendo ni neno jepesi sana likitamkwa kwenye midomo ya watu ila ni neno pana sana kwa magreat thinker. Kenya madaktari au walimu wakiandamana waongozewe mishahara na malupulupu wanaongezewa. Odinga kajiapisha tena kaita mpaka judge amtawaze kuwa raisi. Polisi wameenda na wamesimamia zoezi mpaka mwisho na mwisho wa siku Kenyata amemuita Odinga ikulu na wameyamaliza na Odinga hajafungwa wala kushitakiwa.Ninaposema uzalendo inabidi uelewe maana ya uzalendo, angalia wasanii wa Kenya, kila shairi lazima ataje "Kenya yetu, wanyama wetu, lugha yetu, mlima wetu", sasa angalia huku kwetu, "Bonge nyaya tetema, ai, mama, nakufa, konki , Lwikwidiii..." hahahahahah
Wewe hupendi kugegedwa?Miziki yao wanaimba kuhusu kugegedana tu ndy wabongo asilimia kubwa wanapenda wakubwa kwa wazee
Ova
Sent using Jamii Forums mobile app
Wameitaja Nyegezi Mwanza mmewafungia unadhani nani tena atakua na moyo wa kutaja ngorongoro au serengeti? bora hata utaje likwidi unaeza pata bia na nyama choma za kulipwa fadhira kwa kuwapaishaNadhani ingekuwa vyema kuwa wazalendo kidogo, katika moja wapo ya nyimbo zao wakawa wanachomeka neno Serengeti au hata Ngorongoro, itasaidia sana kiutalii wa ndani na wa nje.
we umeisaidia nini nchi yako?Boss nafikiri ni vizuri watu kuwa na uelewa kidogo wa mambo. Kwan nani mwenye nchi. Nchi ni yetu sisi RAIA. Aman tuliyonayo ndo inatufanya tuwe free hata kufanya muziki, na shughuli zingine. Mashabiki, makampuni yanayotufadhili yote yanafanya kazi kwenye nchi yenye aman na miundo mbinu sahihi. Hivyo vyote havipatikan kutoka tu from nowhere. Kuna kazi inafanyika. Sasa, kila mtanzania anapaswa kusaidia kuifanya nchi iwe nzuri ili kazi zake zifanyike vizuri
Sijui kwann watanzania tunataka kila mtu awe mwanasiasa. Kila unachokifanya una ki connect na siasa. Achen upuuzi. Isaidieni nchi isonge mbele. Makampuni haya yakikua ndio hata shughuli za muziki, mpira na vitu mbali mbali vitapata sponsorshipi kubwa na nyie mtapata hela ya kutosha
Huwezi ukawa unaimba nyimbo zinawika Dunia nzima. Makampuni ya nchin kwako yanakupa sponsorship mpaka unakuwa tajiri et huwezi kutunga hata kawimbo hata kamoja ka kutaja sifa hata moja tu ya nchi yako.
Kama akina AY amepata hela tena kutoka kwenye kampuni ya Kitanzania, anaenda kununua nyumba marekan na kuwaza kuhama kabisa nchi. Kama vile anadhan akienda marekan atakuwa na nafasi ya kufanikiwa kama RAIA wa Kule.
Ndo maana watu husema huwezi kuvuna usichopanda. Unataka nchi ikufanyie kila kitu wakati ww huwezi kuifanyia hata kitu kidogo tu cha kuitaja sifa moja ili labda watali wawili au watatu watavutiwa na kuja kutembea au kuwekeza.
Sio vibaya kwenda kuishi nje lakin wazalendo au watu wenye akili timamu huwa wanaenda nje kutafuta then huleta nyumban kusaidia walio Hm. Sio unapata mafanikio Hm then unataka kuhama kabisa uende ukaishi ugenini.
Usiseme Tanzania itakufanyia nn, sema katika kipindi cha uhai wako umeisaidia nn nchi (Tanzania) yako!!?
Sent using Jamii Forums mobile app
tuna mbuga kibao sio lazima hizo Diamond kwao Kigoma kuna Gombe park, Hamornize Mtwara ni jirani na Selous kwanini wataje za kwenu. tuna Mikumi, Ruaha, SadanNadhani ingekuwa vyema kuwa wazalendo kidogo, katika moja wapo ya nyimbo zao wakawa wanachomeka neno Serengeti au hata Ngorongoro, itasaidia sana kiutalii wa ndani na wa nje.
sasa wakitaja hiyo Serengeti wewe mtazamaji utajuaje kama wametaja mbuga ya wanyama maana neno Serengeti linamaana au linawakilishwa na vitu vingi mfano; mahali, kinywaji, shuleWalitaja neno Kitulo? Sisi watazamaji/wasikilizaji tutajuaje hapo ni Kitulo bila wao kutaja neno Kitulo kwenye mashairi ya Nyimbo?
Wakati nasoma post yako, ikanijia nyimbo ya tetema, sasa swali hiyo Serengeti au ngorongoro itaingiaje au ndo Serengeti tetema ooh mama tetema, ngorongoro tetema oooh mama tetema (daaah funny) ila mziki ni biashara kama watawalipa wcb watangaze hivyo vivutio inawezekana.Sio mawazo mabaya, lakini ulivyoandika kama vile ni lazima kutaja hayo maneno.
Muziki ni biashara lazima uzalishe kile wateja wako wanataka na haifai kupaingiana cha kuwauzia wateja wao.
Wapo wenye dhamana ya kutangaza hivyo vivutio na wanalipwa kwa kazi hiyo.
Je! wewe uliyemzalendo unaitangazaje nchi yako?
Sent using Jamii Forums mobile app
kuna wakati twajifanya wazalwndo uchwara tu, ukichunguza vizuri ni wivu tu sawa na maskini wanavyowalalamikia matajiri kutokufanya mambo flani fani kwenye jamii, je maskini kwanini hafanyi hata kwa kiwango kidogo?Wakati nasoma post yako, ikanijia nyimbo ya tetema, sasa swali hiyo Serengeti au ngorongoro itaingiaje au ndo Serengeti tetema ooh mama tetema, ngorongoro tetema oooh mama tetema (daaah funny) ila mziki ni biashara kama watawalipa wcb watangaze hivyo vivutio inawezekana.
Sent using Jamii Forums mobile app
kitendo cha wewe kuona picha za Diamond akiwa kwenye national parks za hapa TZ tayari kishakuhamasisha na wewe kwenda kutembelea huko sasa wewe huoni kama atakuwa amekutangazia biashara yako kwa kutumia umaarufu wake halafu yeye hapati kituKuna kipindi kulikuwa na tamasha la jembe ni jembe kule mwanza, nakumbuka alialikwa mpaka msanii NE YO toka USA. Baada ya tamasha walipewa offer ya kutembelea mbuga serengeti (Usafiri, kiingilio na malazi) ajabu ni kuwa diamond alikataa kwenda akasema kama wanataka aende wamlipe(waliowaalika ambao walikuwa TANAPA na kampuni moja ya Utalii) kama vile anaenda kufanya show
Utasemaje kuwa hapati kitu wakati tayari amepewa of ya kuingia bure, amelipiwa malazi, chakula na kinywaji akiwa mbugani?kitendo cha wewe kuona picha za Diamond akiwa kwenye national parks za hapa TZ tayari kishakuhamasisha na wewe kwenda kutembelea huko sasa wewe huoni kama atakuwa amekutangazia biashara yako kwa kutumia umaarufu wake halafu yeye hapati kitu
angalia JD alivyoenda kupanda mlima Kilimanjaro baadae mapokezi wa wapanda mlima unakumbuka yalikuaje??
me naona ametumia vizuri jina lake ili afaidike na yeye, uzalendo tutaishia kuusemea mdomoni tu katika nchi hii
Pundamilia tetema, ooh mama tetema, Serengeti tetema, ooh mama tetema..Wakati nasoma post yako, ikanijia nyimbo ya tetema, sasa swali hiyo Serengeti au ngorongoro itaingiaje au ndo Serengeti tetema ooh mama tetema, ngorongoro tetema oooh mama tetema (daaah funny) ila mziki ni biashara kama watawalipa wcb watangaze hivyo vivutio inawezekana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio ajabu kwani diamond ni mfanyabiashara , hao kina neyo waliokuja si wamelipwa na waliowaleta ?Kuna kipindi kulikuwa na tamasha la jembe ni jembe kule mwanza, nakumbuka alialikwa mpaka msanii NE YO toka USA. Baada ya tamasha walipewa offer ya kutembelea mbuga serengeti (Usafiri, kiingilio na malazi) ajabu ni kuwa diamond alikataa kwenda akasema kama wanataka aende wamlipe(waliowaalika ambao walikuwa TANAPA na kampuni moja ya Utalii) kama vile anaenda kufanya show