Wasafi Media bado mna kazi kubwa kufikia matarajio ya watanzania

sonofobia

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2015
Posts
1,171
Reaction score
4,295
Ni media changa ndio ila kwa kuwa jina la Wasafi tayari ni kubwa duniani raia wana matarajio makubwa na media zenu Tv na Radio kuliko ata hizi media mlizozikuta zenye miaka 20 na zaidi.
Mmeanza vizuri lakini bado hamjakata kiu ya washabiki wenu kwenye upande wa media. Mimi ni muangaliaji mzuri wa televisheni yenu navutiwa sana na selection ya muziki wenu lakini bado sijaridhishwa na program zenu. Nazungumzia zaidi TV sababu ndio eneo mna fursa kubwa ya kuteka soko sababu kwa sasa bongo hakuna TV yenye vipindi vya maana vya kustua.

Jipangeni tuone vipindi zaidi vya burudani.

Ningependa kuona Kubum Kubam ina content ya kuvutia na kurudisha hiphop kwenye ramani.
Ningependa kuona Queens inaenda mbali zaidi ya kupiga muziki tu.

Ningependa kuona show za sports, program za fasheni, lifestyle, trends etc etc .
Bado tunaitaji kuona zaidi na zaidi ili muweze kukata kiu zetu mashabiki wenu.

Shout out kwa Aliyah na Refresh team kwa kweli mmefikia standards za brand ya Wasafi.
 
Diamond ni mtu ambaye hakurukupi na ni mbunifu na ndo maana umeona anajatoa vipindi vyote for both radio na tv.
 
Diamond ni mtu ambaye hakurukupi na ni mbunifu na ndo maana umeona anajatoa vipindi vyote for both radio na tv.
Lakini ameionja joto ya jiwe baada ya jamaa wa mawingu kupitia kwa Baghdad kwenda mahakamani kukisimamisha kipindi chao cha The Bartender akidai mkwanja wa idea yake.

Awe makini watampiga sana matukio maadui zake huku sio kwenye muziki.
 
Lakini ameionja joto ya jiwe baada ya jamaa wa mawingu kupitia kwa Baghdad kwenda mahakamani kukisimamisha kipindi chao cha The Bartender akidai mkwanja wa idea yake.

Awe makini watampiga sana matukio maadui zake huku sio kwenye muziki.
Ni wivu tu na chuki, hamna kitu kipya duniani, istoshe jamaa wameanza kumchawia kitambo , ogopa Sana kupambana na mtu talented , utatumia nguvu nyingi kumwangusha ila yeye atatumia nguvu kidogo kupaa
 
Yeyote Mwenye full details kuhusu The Bar Tender kupigwa ban afunguke.
 
Yeyote Mwenye full details kuhusu The Bar Tender kupigwa ban afunguke.
Jamaa amechanganya mafile bagdad alilalamika kuibiwa idea na dada mmoja ambaye ameajiliwa na clouds media hiv karibuni anaendesha hiko kipindi kupitia clouds kuhusu bartender ni kwamba jonijo ambapo alikuwa anaenda kipindi Cha bartender teyali ana kipindi cha 89 block kimegongana na kipindi cha bartender kutokana na Hilo ikibadi bartender isimamwishwe kwanza ili watafute mtu mwingine ataekuwa anaendesha lakini pia diamond amesema watafanya pia maboresho Kuna vitu wataviongezea ili kiwe Bora zaidi before awaja kirusha.
 
Clouds bado haijawa na mpinzani wale jamaa ni wabunifu aiseee alivyokufa ruge nikasema ohooo clouds imeshafulia!..kumbe bado kuna wabunifu wengine wamebaki...
 
Ni wivu tu na chuki, hamna kitu kipya duniani, istoshe jamaa wameanza kumchawia kitambo , ogopa Sana kupambana na mtu talented , utatumia nguvu nyingi kumwangusha ila yeye atatumia nguvu kidogo kupaa
Slowly huyo jamaa amechanganya mafile bagdad amelalamika kubiwa idea ya kipindi na dada mmoja ambaye anakirusha hiko kipindi kupitia clouds media.
 
Clouds bado haijawa na mpinzani wale jamaa ni wabunifu aiseee alivyokufa ruge nikasema ohooo clouds imeshafulia!..kumbe bado kuna wabunifu wengine wamebaki...
Clouds Ina ubunifu upi? Hiv unaweza kufananisha clouds ya kipindi kile na kipindi ambapo wamechuja na hata watazamaji wamepungua kutokana na kuenda mabifu ambayo ya kijinga
 
Clouds Ina ubunifu upi? Hiv unaweza kufananisha clouds ya kipindi kile na kipindi ambapo wamechuja na hata watazamaji wamepungua kutokana na kuenda mabifu ambayo ya kijinga
Hao wasafi wako wana ubunifu gani mwaka huu sasa hawana hata vipindi,
Ubunifu nnaozungumzia hapa angalia vipindi vyoote vya burudani asilimia kubwa watangazaji wana copy na ku-paste xxl,muangalie dj ommy,hao akina jonijo wenyewe wana-copy clouds japo hawajafikia kiwango chao wanaongea tu hovyohovyo wakiwa studio yaani kama walevi flan hivi,angalia ndondo cup,angalia vipindi vya michezo na uchambuzi E-fm akina maulid kitenge wamecopy clouds,angalia vipindi vya mchana na matukio kama vile "leo tena" siku hizi karibia redio zote zimecopy,vipindi vya jioni pia...juzi tu hapa sports extra wameanza kuzungukia matawi ya mashabiki wa simba na yanga,na wana kampeni ya ku-boost ujazwaji wa uwanja,unajua kwa nini?wanataka timu zote ziingize mashabiki 60000,huoni kama jambo la kheri??
Ukija kwenye vipindi vya tv ndo kabisaaaa
Leo hii kuna wasafi festival,ile ni copy ya fiesta jombaaa...
Mnajitahidi sana kuichukia clouds lakini wale ndo wataalamu wa hizi kazi.
 
Naona Kama naongea na mfanyakazi wa clouds naona ni kubishana na mtu Kama wewe ni kupoteza muda wangu.
 
Kwanza Wasafi Fm na Tv mpaka sasa hawana kipindi cha sports, ila wana segment ya sport ndani ya Block 89 ambayo ni kama dk 5 tu kupeana trending stories na inafanywa na Ricardo Momo huyu ni mwanamichezo na si wa mdomo tu anaupiga kabisa hivyo usiwaweke kundi moja na EFM au Clouds ambao wana wachambuzi na watangazaji mahiri na wa muda mrefu.
.
Umesema Wasafi wana copy vipindi XXL tumuangalie Dj Ommy na Jonijoo na wenzake wanaongea hovyohovyo, nikusaidie Clouds ndiko watangazaji wanapoongea hovyohovyo sikiliza Leo tena mambo ya Mussa Hussein na wenzake ni kelele tupu ila sio inshu XXL target yake ni vijana wa kuanzia miaka 18-28 tu wengine sio lengo lao na hili alishalizungumzia Dozen.
.
Jonijoo ni presenter mkali sana Bongo yule jamaa kaanzia Times Fm ni mtangazaji wa kiwango cha juu pamoja na Calypso wote wametoka Times hivi kiwango cha Callypso mnyamwezi yule unakionaje? Dj Ommy hafanyi kazi wasafi huwa anaitwa wakati wa festival tu
.
Umesema Sports xtra wanatembelea matawi ya mashabiki wa Simba na Yanga wanataka uwanja uingize mashabiki elfu 60 loh! Kwa ushawishi gani wakati Fiesta yenyewe hawawezi kufanya hivyo hao wanatembelea watu wao wa ndondo cup na si vinginevyo.
.
Ukasema pia tukija kwenye tv ndio kabisaa hapa unachekesha TV yenye vipindi vizuri bongo hadi sasa ni EATV, Clouds tv ina vipindi vya hovyo sana inazidiwa hadi na Tv E
.
Wasafi tv wana vipindi vichache vingi bado hawajavianzisha, umesema pia Wasafi festival ni copy ya Fiesta hivi Fiesta ndio tamasha la kwanza la muziki duniani au ulipitiwa tu?
.
ITV ndio wa kwanza kutumia neno Mubashara wengine wote wataiga kutoka kwao, ila Tamasha la muziki ukisema wasafi wameiga Fiesta unalifahamu tamasha la Kochela?
 
Kwahiyo idea ya fiesta clouds median ndo wakwanza kuwa na tamasha kubwa la muziki, hakuna kipya chini ya jua
 
Wenye Clouds ndio wenye Wasafi
 
Naona Kama naongea na mfanyakazi wa clouds naona ni kubishana na mtu Kama wewe ni kupoteza muda wangu.
hata ivo hatutaki ubishe, tunataka na ww utoe facts zako apa kama alivyotoa mteteaji clouds
 
Wenye Clouds ndio wenye Wasafi
Hapa ndio mwisho wa habari mengineyo ni mitazamo na mapenzi ya wasikilizaji na watazamaji kila mmoja kunogesha upande wake huku ukweli ukiwa wazi bila huyu huyu asingekuwepo
 
Clouds Tv wanakipindi gani chenye mvuto?
 
√Huyo jonijoo ni mtangazaji wa kawaida sana mkuu..sio mkali kihivyo..unaposema ni mkali bongo sijui unamlinganisha na nani??,labda na watangazaji wa mikoani

√Kimsingi Wasafi media platform ndo inayowabeba,na simaanishi kuwa ni wabaya,ila wanafanya vitu vya kawaida..

√Unaposema XXL wanapiga kelele unakuwa hueleweki..hivi kuna Show ya burudani yenye mpangilio mzuri kama XXL??..yaani segment zimepangwa na zinacover kila kitu..

√Finally,mmiliki wa Wasafi media ndo huyo huyo wa Clouds..sasa sijui mnapopasuana hapa ni kwa faida ya nani??..Yeye hawezi kuua upande mmoja ili apandishe mwingine,..Clouds tayari ni biashara iliyosimama huku wasafi ikiwa bado sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…