Ukiona kipindi kinapata matangazo meeengi ya biashara ujue kinapendwa na wasikilizaji au watazamaji wengi. Ukiona kipindi kinapendwa na wengi ujue kimegusa maisha ya wanajamii husika wengi. ukiona kipindi kimegusa maisha ya wanajamii walio wengi basi ujue kimeakisi mawazo ya wanajamii wengi na mtindo wao wa maisha.
Kama kipindi cha kipumbavu kinapendwa na wanajamii wengi basi ujue jamii husika imejaa wapumbavu wengi. Kiufupi vipindi vyoote vinavyotrend maredioni kama vile vya michezo, umbea, upuuzi upuuzi na kuhamasiha udangaji na ushoga manaake vinaakisi jamii ya watanzania walio wengi.
Asenti