Wasafi TV yapunguziwa adhabu, sasa kutumikia adhabu mpaka 28 Februari, 2021

Wasafi TV yapunguziwa adhabu, sasa kutumikia adhabu mpaka 28 Februari, 2021

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imefanya mapitio ya adhabu iliyotoa kwa Wasafi TV baada ya Wasafi kupeleka ombi la kufanya hivyo.

Baada ya mapitio TCRA imeakuja na uamuzi wa Wasafi kuendelea kutumikia adhabu hiyo mpaka tarehe 28 Februari 2020.

UAMUZI WA TCRA DHIDI YA WASAFI

1. WASAFI TV wataendelea kutumikia adhabu hiyo mpaka tarehe 28 Februari, 2021

2. WASAFI TV inaelekezwa kuzingatia masharti ya leseni ya kutoa huduma za maudhui ya kulipia kwa njia ya televisheni(Subscription content); na

3. Iwapo WASAFI TV itashindwa, itakataa au kukaidi Uamuzi huu, hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti zitachukuliwa dhidi ya Wasafi TV



TCRA.JPG

Pia, soma: RUNGU: TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha matangazo kwa Miezi Sita (6) kuanzia leo kwa kurusha Maudhui ya utupu
 
Kwani imefungiwa?

Mbona Jumapili nimemwona Polepole akihubiri neno la Mungu hapohapo Wasafi tv akiwa na mchungaji Masanja?!
 
TCRA walitoa ile adhabu kimihemko bila kutumia akili na kuangalia other factors. Unagungiaje tv miezi sita ambayo imejiajiri watu na inabidi ifanye kazi kukkuza uchumi. Next time watumie akili hao tcra mihemko sio mizuri.
Kwani Tanzania daima,mwanahalisi,kwanza TV walikuwa hawatoi ajira na kukuza uchumi?Double standard katika nchi hutengeneza Taifa la visasi lakini pia huonyesha ni kwa kiwango gani viongozi ni incompetent!
 
Unafungiaje tv miezi sita ambayo imejiajiri watu na inabidi ifanye kazi kukkuza uchumi. Next time watumie akili hao tcra mihemko sio mizuri.

Double standards zipunguzwe.

Vipi kuhusu magazeti ya mwananchi, Mtanzania au Mwanahalisi?

Wao hawakuajili watu? Wao hawakuzi uchumi?
 
Double standards zipunguzwe.
Vipi kuhusu magazeti ya mwananchi, Mtanzania au Mwanahalisi?
Wao hawakuajili watu? Wao hawakuzi uchumi?
Ndio adhabu KWA wote zilikuwa za kishenzi na kukomoana Ili kutafta sifa kwa bosi mkubwa, makosa huwa yapo na sio kukomoana. Tcra Wana roho ya kichawi hao watendaji kwanini wasitoe inyo mtu akikaidi Mara kadhaa ndio ashushiwe rungu.
 
Kwani Tanzania daima,mwanahalisi,kwanza TV walikuwa hawatoi ajira na kukuza uchumi?Double standard katika nchi hutengeneza Taifa la visasi lakini pia huonyesha ni kwa kiwango gani viongozi ni incompetent!
Kote tu hawakustahili hyo adhabu hafu pia hayo masharti yaliongozwa na chuki na kutofautiana kiitikadi due to mature ya utawala wa visasi na roho mbaya.

Mimi wote kuanzia Mwanahalisi sijui wasafi adhabu zilikuwa za hovyo.
 
Askari wewe, Jugde wewe, Judge wa rufaa wewe, msamehe makosa wewe. wafungulieni tu wafanye kazi hata leo maana umesamehe mpaka tarehe 28 ili upate nini cha ziada. Hakuna vyombo huru vya kusikiliza rufaa baina ya msimamizi, mtoa huduma na mlaji.
 
Kungekuwa na chombo kweli huru kama mahakama kusikiliza kesi kama hizi hata mtoa adhabu angekuwa anafuata sheria maana ukiitwa inabidi utoe ushahidi na kutoa sheria zilikupa madaraka ya kufanya maamuzi.

Lazima kuwe na chombo huru cha kuamua migogoro ya kibiashara kwa kutumia sheria za haki sio unavyotafsiri wewe tukio. tunahitaji VAR
 
Ujinga mtupu,mbona wengine hawakupewa upendeleo huu,Kisa ni TV ya waimba mapambio?
 
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA imetafakari upya na kuwapunguzia adhabu WASAFI TV ambapo adhabu yao itaisha tarehe 28/02/2021, na ilianza tarehe 05/01/2020 ambapo watakuwa wametumikia adhabu mwezi mmoja na wiki 3.

Mnamo tarehe 05/01/2021 TCRA waliifungia WASAFI TV kwa muda wa miezi 6, hivyo Kama adhabu husika ingebaki kama ilivyo ingeisha tarehe 2 Julai mwaka huu, lakini kwa sasa itaisha mwishoni mwa mwezi huu.
IMG-20210204-WA0025.jpg
 
TCRA walitoa ile adhabu kimihemko bila kutumia akili na kuangalia other factors. Unagungiaje tv miezi sita ambayo imejiajiri watu na inabidi ifanye kazi kukkuza uchumi. Next time watumie akili hao tcra mihemko sio mizuri.
Ulichokiandika umekisoma? Bahahahaha!
 
Back
Top Bottom