Wasafiri Wanaotumia Njia za Mbuga za Wanyama Wasihesabiwe kama Watalii

Wasafiri Wanaotumia Njia za Mbuga za Wanyama Wasihesabiwe kama Watalii

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii amesema Wizara isiwahesabie abiria kutoka Mkoa mmoja kwenda Mkoa mwingine kwa kupitia njia zilizopo kwenye Mbuga za Wanyama kama Watalii wa ndani kwani hawaigizi fedha za kigeni

"Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 (Uk. 11-67a) Ifikapo 2025 tunatakiwa tuweze kuingiza fedha zinazotokana na Utalii Dollar 💵 Bilioni 6 (Tsh. Trilioni 14), pia Tanzania 🇹🇿 iwe imepokea Watalii Milioni 5" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Hali ilivyo sasa, hadi kufikia Aprili 14, 2023 tulikuwa na Watalii 1,412,719 pungufu ya lengo kwa Milioni 3.5 na kuingiza fedha za Kitanzania Bilioni 288 ambayo ni asilimia kidogo sana ukilinganisha na Trilioni 14 zinazokusudiwa" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Watalii wa ndani ni 718,299. Watalii wa nje ni 694,420 ambao wametokana na Ziara ya Rais Samia kupitia "The Royal Tour". Mtu akipita kutoka Arusha kupitia Momera kwenda Vijijini, akitoka Bagamoyo, Saadan, Pangani kwa gari binafsi anahesabiwa kama mtalii wa ndani? Kutoka Arusha kupitia Serengeti, Ngorongoro anaenda Musoma, Tarime, Mwanza anahesabiwa ni mtalii? Hawa ni wasafiri" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Wizara ya Utalii ondoeni VAT kwenye Airline Industry. Utalii tunafanya Export of Services ndiyo maana tunapata Dollar 💵 katika kipindi Dunia ina msukosuko wa FOREX Utalii ndiyo unatakiwa utulinde tupate fedha za kigeni" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Ondoeni VAT kwenye Airlines, Injini ya Ndege, Spare Parts za Ndege, Aircraft Maintenance. Hizi Ndege zinasaidia wawindaji kupeleka Watalii wao kwenye vituo vya kuwindia, zinasaidia Watalii kutoka eneo moja kwenda eneo jingine" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Ondoeni VAT kwenye ada za Vitalu, mtu anapokuwa amelipia kitalu kwa mwaka Amelipa ada ya kwanza anakuwa amekilipia kwa miaka 10, lakini fedha anayolipia kwa miaka inayofuata mnaipiga VAT kwa 100%, hii si sawa!" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Ilani ya CCM 2020-2025 inasema "Fanyeni mapitio ya Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo" Sheria ya VAT siyo msahafu. Kwenye Finance Bill Serikali iweke Commitments ya kuondoa VAT. Tunataka fedha za kigeni, tusifike mahali tukashindwa kuagiza bidhaa nje ya nchi kwa sababu hatuna Dollar" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

"Watu wa Mahoteli wanaosafirisha wanatozwa VAT mahali ambapo siyo sahihi kwasababu ya ubovu wa Sheria. Ondoeni VAT kwenye deposit" - Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini

 
Back
Top Bottom