Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,

Nimeangalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinacharushwa Live na Star TV kila Jumamosi asubuhi. Namshauri Dialo atafute muda kipindi hiki kirudiwe jioni wakati wa prime time ili wengi waone.

Kipindi cha leo kusema ukweli muongozaji Dotto Bulendu na mgeni wake Ansbert Ngurumo wameitendea haki tasnia ya Habari dhidi ya vitisho vilivyotolewa jana na rais Magufuli kwa media.

Naomba nisiingie ndani sana kuhusu Ngurumo na Bulendu walisema nini kuhusu rais kutaka kuipangia media nini cha kuandika, mimi naomba kujikita kwa watu ambao ni wasaidizi wa rais wanajukumu la kumsaidia kwa kumpa ushauri sahihi wa hatua za kuchukua kwenye situation fulani fulani as wajibu wao, duty of care not favours, not options but as their responsibilities.
Haya chini ni yangu.

JF Kujadili Watu Badala ya Kujadili Maendeleo.
JF tumelaumiwa kutumia muda mwingi kujadili watu badala ya kujadili maendeleo. Maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu na sii maendeleo ya vitu, na maendeleo hayo yanaletwa na watu na hayaletwi na vitu, hivyo hatua ya kwanza kabisa kabla hata ya kufikiria hayo maendeleo, kitu cha kwanza na muhimu kuliko vyote ni watu kwasababu hata sababu ya hayo maendeleo ni watu, wenye kuyahitaji hayo maendeleo ni watu, na wanaoyaleta hayo maendeleo ni watu, kama ilivyo demokrasia ni " of the people, by the people and for the people", huwezi kabisa kukweoa kuzungumzia watu haswa ni nani anayewaongoza hao watu kuyaleta hayo maendeleo, hivyo watu wana haki ya kumjadili kiongozi yoyote mwenye dhamana ya kuwaletea maendeleo, hata katiba imeanza kwa maneno "We The People.." ikimaanisha ni watu, hata demokrasia ni "of the people, by the people and for the people", yaani ni serikali ya watu, iliyochaguliwa na watu, na inaongozwa na watu, kwa manufaa ya hao watu, hivyo, watu ndio kila kitu, hata nchi, kitu muhimu kabisa ni watu, ndipo lije eneo etc, hivyo watu ndio kila kitu.

Tanzania ni nchi yetu sote na sio nchi ya mtu mmoja, japo Tanzania ya sasa inaitwa ni Tanzania ya Magufuli kama Darisalamu inavyoitwa Jiji la Makonda, haya ni majina tuu, kiukweli Tanzania ni ya Watanzania wote, na Darisalamu ni ya wana Darisalama wote, it's the people who matters.
Jee Wajua Kuna Tofauti kati ya Mtu anayeitwa Dr. John Pombe Magufuli na Rais Dr. John Pombe Magufuli?.
Sii wengi wanaofahamu kuwa nafasi ya urais ina kitu kinachoitwa "a duality personality", mtu anayekuwa rais wa nchi, japo ni mtu mmoja, lakini anakuwa na kitu kinachoitwa "duality personality" ambapo wanakuwa ni watu wawili in one, yaani "two in one". Mtu wa kwanza ni mtu anayeitwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, huyu ni mtu, ni binadamu wa kawaida kama binadamu mwingine yoyote, lakini ndani ya huyu mtu, kuna na mtu mwingine anayeitwa "Rais", Dr. John Pombe Joseph Magufuli, huyu sio mtu wa kawaida!, huyu ni rais wa nchi, huyu sii mtu tuu ni mtu taasisi, (not a human being, but an institution), urais ni taasisi, hawa ni watu wawili tofauti wenye jina moja, mwili mmoja na personality moja. Mmoja ni mtu tuu kama mtu mwingine yoyote, anaweza kufanya chochote na kusema chochote, na huweza kukosea, huyu ni binaadamu wa kawaida. Huyu na mwingine Rais Dr.John Pombe Magufuli, sio mtu wa kawaida, huyu ni mtu taasisi ya urais, he is supposed to be perfect, hawezi kusema chochote au kufanya lolote, bali huelekezwa na katiba, na hawezi hata kukosea ndio maana hawezi kushitakiwa, hata ile kinga ya rais kutokushitakiwa, inahusu utekelezaji wake wa majukumu yake ya kitaasisi ya urais tuu na sii yeye kama mtu tuu. Ikitokea tunamjadili rais Magufuli, hatumjadili mtu anayeitwa Dr. John Pombe Magufuli, bali tunamjadili Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli ambaye ni kiongozi wetu tuliyemkabidhi taasisi yetu ya urais, ambayo ndiyo mamlaka kuu kiutawala kuliko mamlaka nyingine zote ndani ya JMT, ndio maana amewekewa wasaidizi mbalimbali wa kumsaidia wakiwemo mawaziri, wakuu wa taasisi na washauri lukuki.

Uhuru wa Dr. John Pombe Magufuli Kuongea Chochote, Popote na Kwa Yeyote.
Mtu anayeitwa Dr. John Pombe Magufuli,yeye kama binadamu mwingine yoyote, ana haki zote za kiraia ikiwemo freedom of expression hivyo yuko huru kuongea chochote, popote na kwa yeyote, ali mradi havunji sheria, kama alivyo huru kula kitu chochote, popote, kunywa kinywaji chochote hata pombe yoyote na kulewa vyovyote, kwenda popote na kufanya jambo lolote kuhusu mapenzi yake binafsi ikiwemo kutazama vipindi vyovyote vya TV kikiwemo kipindi cha Shilawadu. Hakuna yoyote mwenye uhuru wa kujadili jambo lolote kumhusu mtu yoyote akiwemo Dr. John Pombe Magufuli, huku ni kuingilia uhuru wake wa his rights to privacy.

Uhuru wa Rais Dr. John Pombe Magufuli Kusema Chochote Popote na Yeyote.
Rais Dr. John Pombe Magufuli as rais na as taasisi anakuwa hayuko huru kufanya chochote, kwenda popote, kula chochote, kunywa chochote, na anapoongea kama rais wa JMT, hapa yeye ni taasisi, hawezi kujiongelea chochote tuu anachojisikia, popote na kwa yeyote, kwa sababu urais ni taasisi na chochote anachoongea kama rais kinakuwa na mamlaka nyuma yake, hivyo kauli yeyote ya rais ni amri yenye mamlaka, authority. Hivyo hawezi tuu kujisemea chochote na popote na hapa ndipo anapohitaji wasaidizi wa kumsaidia kutenganisha wapi awe huru kuongea kama mtu Dr. John Pombe Joseph Magufuli na wapi aongee kama rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli aseme nini na wapi. Kwa vile the two are in one, katika kuongea the dividing line between the two is very thin,

Na hawa ni baadhi ya wasaidizi niliowapendekeza

Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!.
Jee Lazima Hotuba Zote za Rais Lazima Ziandikwe?.
No, sio lazima hotuba zote za rais lazima ziandikwe, hotuba nyingine katika shughuli zisizo rasmi, informal events, huibuka tuu impromptu, na hazijapangwa na hizi hazina tatizo. Ila kunapotokea shughuli zozote formal, na rais ataongea, lazima wasaidizi wake wamsaidie kumpangia ataongea nini, japo adlib kwenye hatuba zote ni jambo ambalo haliepukiki. Ila pia pamoja na uhuru wa raisi wetu kuongea chochote popote, yeye kama rais, anapoongea kama rais, hapa yeye ni taasisi, hivyo anawajibu wa kuchunga sana kauli zake kwa sababu huyu sasa sio Magufuli tuu kama Magufuli mtu, bali ni Magufuli kama rais Magufuli wa JMT, jambo lolote analoongea akiwa live, anawaambia Watanzania wote.

Washauri Mshaurini Rais Magufuli Kutenganisha Anapozungumza, Kama Magufuli na Anapozungumza Kama Rais Magufuli.
Washauri wa rais, lazima mumsaidie rais wetu awe na uwezo wa kutenganisha ni wakati gani anazungumza kama mtu binaadamu anayeitwa John Pombe Joseph Magufuli, na ni wakati gani anazungumza kama rais wa JMT, ambaye ni John Pombe Magufuli.

Mfano Mtu anayeitwa John Pombe Magufuli ni mpenzi wa kutazama Clouds TV, na ni mpenzi wa kipindi cha Shilawadu, hivyo yuko huru kupiga simu Clouds wakati wowote na kuwapongeza Clouds kwa kipindi chao kizuri cha Shilawadu na yeye kuelezea jinsi anavyokipenda kipindi hiki. Kwa vile kiko live nchi nzima, simu ya rais inapopokelewa, Tanzania nzima wanasikia, hivyo japo amepiga simu kama Mtanzania mwingine yoyote mwenye mapenzi na Clouds, chochote atakacho sema, ni kulihutubia taifa kupitia Clouds TV, hivyo rais anapopiga simu clouds kuwapongeza kuwa anaangalia kipindi cha Shilawadu na anakipenda, ni kama anatuma ujumbe kwa Watanzania wote kuwa kipindi cha maana kuangaliwa ni Shilawadu, sasa kwa watu ambao walikuwa hata hawakijui, wakakitafuta na kuangalia kipindi kinachopendwa na rais wetu, this leaves much to be desired, tuna rais wa aina gani kama vipindi ambavyo rais wetu anapenda kuangalia ni vipindi vya type ya shilawadu?!. Vitu kama hivi vinashusha hadhi ya taasisi yetu ya urais hivyo wasaidizi wake akiwemo msaidizi mkuu nambari one, lazima wamsaidie rais wetu kuweka mipaka kati ya mtu anayeitwa John Pombe Magufili na Rais John Pombe Magufuli, japo the dividing line is very thin.

Hii imepelekea kuna wakati rais kama rais anatoa matamko tata au maamuzi tata yanayoashiria kuwa rais hakupewa ushauri sahihi kabla, kisha waziri wake anakuja kuibuka baadae na kuirekebisha kauli ya rais kwa kuifuta na kuweka mambo sawa.

Mfano mzuri ni siku ile rais alipotoa tangazo hili
Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni ...
kisha waziri wake akaja kuibatilisha kauli hii kwa kusema rais alikuwa anatania tuu watani zake. Rais anapozungumza kwenye hotuba inayotangazwa moja kwa moja kwa taifa zima na akatangaza jambo fulani, hii maana yake ni kulitangazia taifa. Sijadhani kama Watanzania walichagua rais Msukuma ili atoe maagizo kwa watani wake Wazaramo kwenye matangazo ya moja moja mubashara ya kulitangazia taifa zima. Kauli yoyote ya rais ni sheria.

Rais kama binadamu na kama Msukuma ana haki ya kutaniana na watani zake Wazaramo vyovyote vile ataona inafaa, lakini utani huo ama autolee kwa Wazaramo wwnyewe na sio mubashara kwa taifa zima, na utani kama huu ukitolewa kwenye matangazo mubashara ya moja kwa moja kwa taifa zima, then rais akiishatoa utani kama huo amalizie kwa kusisitiza ni utani tuu au kwa Wazaramo tuu.

Kuna vitu rais wetu anasema au anafanya vinavyoashiria amekosa ushauri sahihi.

Mfano mzuri ni issue ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, hii issue imekuwa too much mishandled hadi kumchafulia rais na kumjengea chuki ndio maana kwenye mitandao ya kijamii watu wamekasirika sana hadi kumkosea heshima na kutoa lugha za machukizo.

Japo mimi sio mtu wa serikali, bali naamini Wakuu wa Utumishi wa Umma wote popote walipo ni wasaidizi wa rais. Wasaidizi wa rais wanaopaswa kuwa pro active kumsaidia rais wakali wote na sio kusubiri hadi waulizwe rasmi ndipo wasaidie.

Kadhia na Kashfa ya Paul Makonda Kughushi Vyeti na Ndiye Daudi Bashite.
Kadhia ya Paul Makonda kutumia vyeti ya kughushi na kufanya udanganyifu ilipoibuka tuu, kabla haijafikia stage ya kumchafulia rais, wasaidizi wa rais wanaohusika walipaswa kujitokeza wao na kumweleza rais ukweli kuwa ni kweli Paul Makonda ndie Daud Albert Bashite na yote yanayosemwa kumhusu mtu huyu ni ukweli kabisa hivyo wangemshauri the right thing to do, hili jambo lingekuwa limekwisha, lakini kumfukuza Waziri Nape kwa hasira na kuendelea kunyamaza as if nothing has happened, hukuwezi kusaidia kitu kuondoa hizo negative perception. Solution ya kudumu ni kuja na ukweli tuu. He has to tell the truth and the truth will set him free. Nikimaanisha baada ya ukweli kujulikana kuwa Daud Albert Bashite ndiye Paul Christian Makonda, then kwa wanaoujua ukweli huu kuwa Daud Albert Bashite ndiye Paul Christian Makonda, kwao he will always be Daud Albert Bashite, and never will he be Paul Christian Makonda, na huyu Paul Makonda he is an imposter!. Na kwa wale wote wanaomfahamu Paul Christian Makonda as Paul Christian Makonda, wataendelea kumfahamu kama Paul Makonda but with much skepticism and reasonable doubt kuwa could he be the real one or ni imposter hadi tuhuma zile zikanushwe rasmi kuwa ni uongo na uzushi!.

Rais Hakushauriwa Vizuri Kuhusu Kashfa ya Paul Makonda Kuvamia Clouds Media
Tukija kwenye tukio la uvamizi wa Clouds Radio, Msaidizi wake Nape did the right thing kwa ku come forward na kusema wazi ule ni unajis wa mtu binafsi na sio serikali. Japo kuunda tume wasn't the right approach Nape kama Msaidizi wa rais ambaye ni Waziri, Makonda ni bwana mdogo sana kwake, angemkabili kuupata ukweli yeye and go straight kwa rais kumpa first hand information na kumwachia rais kufikia uamuzi.

Rais angekuwa ameshauriwa vizuri na wasaidizi wake wanaoujua damage control, wangemshauri rais kuwa dogo ame mess, hivyo ili kulipa millage ya kutosha tukio la rais wa Benki ya Dunia, rais hakupaswa kusema chochote kumhusu huyo dogo. Tukio la uvamizi wa RC kwenye Chumba cha Habari ni tukio kubwa kuliko hata Benki ya Dunia ingehamishia strong room yake pale ikulu kutokana na proximity na impact ya news ya uvamizi.

Kipi ni Habari Kubwa Kati ya Rais Kufanya Ziara Bandarini Au Kichaa Mmoja Kumtishia Bastola?
Juzi asubuhi rais anafanya uteuzi mpya kwa hasira bila kutengua uteuzi wa zamani, kisha akaenda bandarini kwenye ziara ya kushtukiza. Huku nyuma akatokea kichaa mmoja kumtishia bastola waziri wake aliyetumbuliwa. Kihabari yaani ki newsworthyness, tukio la waziri kutishiwa bastola na kichaa fulani ni bigger news kuliko rais kutembelea bandarini.

Kwa vile rais hakufurahishwa jinsi media haikutoa umuhimu stahiki kwa matukio ya msingi yenye umuhimu mkubwa sana kwa taifa, na yeye pale ikulu anayo kurugenzi yake ya habari, lilikuwa ni jambo dogo tuu hata kuteta na Msigwa kwa kumuuliza hivi hii inakuwaje, Msigwa angemweleza tuu ukweli what was news kuliko rais kuonyesha hasira kwa media.
Wasaidizi na Washauri wa Rais Wana Wajibu wa Kumshauri Rais ili Kumsaidia
Wasaidizi wa rais wa kila eneo wana wajibu wa kumsaidia rais wetu kwa kumshauri kufanya uamuzi sahihi na kumwachia rais kufanya uamuzi wowote ila sisi kama Watanzania tuna shauku ya kumuona kila wakali rais wetu akifanya na kutenda the right thing at the right time and doing it right. Rais asiposhauriwa vizuri, matokeo yake ni majanga kwa taifa letu, na kama ilivyo kanuni ya majanga kuwa mchuma janga hula na wakao, ushauri wowote ambao sio sahihi, rais akishauriwa, halafu katika kutekelezwa ushauri huu ukawa na matokeo mabaya, the impact ya matokeo hayo yatatuathiri sisi Watanzania wote collectively as a nation na sio rais pekee au rais na serikali yake bali madhara ya ushauri usio sahihi athari zake ni kwa Tanzania nzima kama Taifa.

Washauri wa rais mko wapi na mnafanya nini hadi kumuacha rais huku tukimshuhudiana kwa kumuona rais wetu anasema na kutenda baadhi ya mambo akiwa as if hakushauriwa vizuri, au yuko kama vile hana washauri?! .
Sisi jf tutaendelea kushauri kwa lengo la kujenga.

Kuhusu uhuru wa rais wetu kushauriwa, kupokea ushauri na kusema lolote, tulilizungumza hapa Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila...

Tanzania ni yetu sote na rais Magufuli ni rais wetu wote.
Mungu Ibariki Tanzania.
Jumamosi njema.
Paskali
 
Tatizo Paskali huwa hueleweki una simamia nini, mara Makonda awe Rais, Mara tuthibitishe kama kweli Makonda ndio Bashite, leo tena umerukia huku, yaani hutulii kwenye lane moja uka elewekaga bro, sasa hata siku ukiongea mambo ya maana una kuta watu wanakushangaa tuu maana hawajui huwa una amini kitu gani. Nakumbuka kwenye fasihi tulikuwa tukisoma kazi yoyote lazima tujue msimamo wa mwandishi, well hii siyo fasihi ila mkuu kwa kweli najaribu kutafuta msimamo wako huwa siuoni.

Ya Bashite na kuropoka tusha ongea sanaa Prezidaa ni mbishi na wasaidizi wake hawana la kufanya labda kama wamfunge kamba, ila jamaa ni sikio la kufa.
 
Umeandika vyema mpaka inafika pahala unaona kama hawa washauri wanakula kodi zetu bure maana hawafanyi kazi yao. Kibinadamu kila mmoja wetu ana udhaifu wake nukuu "nchi hizi mungu katupa tuziongoze na si malaika sasa kama binadamu tunakosea na inapotokea kujirekebisha sio dhambi wala udhaifu "mwalimu jk Nyerere.
 
Hakuna msukuma mwenye akili kama za Sizonje anaaribia watu kabila lao.

Wale wakarimu wasiompita mtu bila salaam wasiopenda uwatembelee kisha usile kwao!!

Ndio watoke kabila moja na Sizonje mwenye roho mbaya kupita ubaya wenyewe.

Jamani mara ingine mkiona [emoji84] kubwa hiyo ni housing tu ndani mashine ndogo.
 
Mie kama mtu mzima ni kweli maneno anayoambiwa mkuu mara nyingine yananiumiza, watu hawafichi tena na hii si dalili nzuri, kibaya chanzo ni yeye, mimi naamini suala la Bashite angeweza kulihandle kwa namna nyingine ili huu upepo upite. Litamvua nguo.
 
Tatizo Paskali huwa hueleweki una simamia nini, mara Makonda awe Rais, Mara tuthibitishe kama kweli Makonda ndio Bashite, leo tena umerukia huku, yaani hutulii kwenye lane moja uka elewekaga bro, sasa hata siku ukiongea mambo ya maana una kuta watu wanakushangaa tuu maana hawajui huwa una amini kitu gani. Nakumbuka kwenye fasihi tulikuwa tukisoma kazi yoyote lazima tujue msimamo wa mwandishi, well hii siyo fasihi ila mkuu kwa kweli najaribu kutafuta msimamo wako huwa siuoni.

Ya Bashite na kuropoka tusha ongea sanaa Prezidaa ni mbishi na wasaidizi wake hawana la kufanya labda kama wamfunge kamba, ila jamaa ni sikio la kufa.
Kuwa mbayu wayu utamuelewa Pascal .msikilize anacho eleza alafu changanya na akili yako
 
Kwa hapa Tanzania hata hao washauri wa raisi nadhani wanawaza zaidi maslahi yao binafsi kwa hiyo hawana muda wa kumshauri..kama si hivyo basi wanamuogopa sana na ni utumwa kukuogopa binadamu mwenzio
 
f851275b931fa269b645ff839151feab.jpg

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]
 
Hivi alivyokwambia yeye huwa hapangiwi cha kufanya ulielewa? Maana yake yeye hashauriki.

Kwa mfano jana, washauri wake walimshauri asiongee lolote ndiyo maana mwanzo akasema hana la kuongea, alivyokumbuka kuwa hapangiwi la kuongea ndiyo akaanza kutoa vitisho na madharau kwa vyombo vya habari, wanavijiji wasiyojua nini kinaendelea kwenye vyombo vya habari(kama alivyosema yeye) wapo watamchagua tu 2020, wasiwasi wa nini?
 
Hii nchi inahitaji uongozi wa kiamri..uongozi wa mashauriano ulishafeli..wacha twende na huu maana unaonyesha njia..siku zote maendeleo ya nchi huletwa na uthubutu wa wachache..na wengi huachwa nyuma kama ilivyokuwa kwa nape na wenzie..
 
Wewe Mayalla vipi bwana.Kwani huwezi kuandika kitu kingine tofauti na Siasa na hasa Makonda?.Kwa mfano,serikali imezuia ORE concentrate export.Tangu Serikali imetoa tamko hilo what has been the positive/negative impacts to the nation's economy so far..Mheshimiwa Waziri Mkuu alikuwa Mauritius siku chache zilizopita na kuwaasa waMauritius kuja kuwekeza Tanzania nikawa najiuliza hawa Wamaurius wana nini cha ziada kuwekeza huku TZ nk,unaweza kuja kwenye angle hiyo tukajadili,tukaelimishana,nk.Mambo ni mengi
 
Back
Top Bottom