Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,

Nimeangalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinacharushwa Live na Star TV kila Jumamosi asubuhi. Namshauri Dialo atafute muda kipindi hiki kirudiwe jioni wakati wa prime time ili wengi waone.

Kipindi cha leo kusema ukweli muongozaji Dotto Bulendu na mgeni wake Ansbert Ngurumo wameitendea haki tasnia ya Habari dhidi ya vitisho vilivyotolewa jana na rais Magufuli kwa media.

Naomba nisiingie ndani sana kuhusu Ngurumo na Bulendu walisema nini kuhusu rais kutaka kuipangia media nini cha kuandika, mimi naomba kujikita kwa watu ambao ni wasaidizi wa rais wanajukumu la kumsaidia kwa kumpa ushauri sahihi wa hatua za kuchukua kwenye situation fulani fulani as wajibu wao, duty of care not favours, not options but as their responsibilities.
Haya chini ni yangu.

JF Kujadili Watu Badala ya Kujadili Maendeleo.
JF tumelaumiwa kutumia muda mwingi kujadili watu badala ya kujadili maendeleo. Maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu na sii maendeleo ya vitu, na maendeleo hayo yanaletwa na watu na hayaletwi na vitu, hivyo hatua ya kwanza kabisa kabla hata ya kufikiria hayo maendeleo, kitu cha kwanza na muhimu kuliko vyote ni watu kwasababu hata sababu ya hayo maendeleo ni watu, wenye kuyahitaji hayo maendeleo ni watu, na wanaoyaleta hayo maendeleo ni watu, kama ilivyo demokrasia ni " of the people, by the people and for the people", huwezi kabisa kukweoa kuzungumzia watu haswa ni nani anayewaongoza hao watu kuyaleta hayo maendeleo, hivyo watu wana haki ya kumjadili kiongozi yoyote mwenye dhamana ya kuwaletea maendeleo, hata katiba imeanza kwa maneno "We The People.." ikimaanisha ni watu, hata demokrasia ni "of the people, by the people and for the people", yaani ni serikali ya watu, iliyochaguliwa na watu, na inaongozwa na watu, kwa manufaa ya hao watu, hivyo, watu ndio kila kitu, hata nchi, kitu muhimu kabisa ni watu, ndipo lije eneo etc, hivyo watu ndio kila kitu.

Tanzania ni nchi yetu sote na sio nchi ya mtu mmoja, japo Tanzania ya sasa inaitwa ni Tanzania ya Magufuli kama Darisalamu inavyoitwa Jiji la Makonda, haya ni majina tuu, kiukweli Tanzania ni ya Watanzania wote, na Darisalamu ni ya wana Darisalama wote, it's the people who matters.
Wasaidizi na Washauri wa Rais Wana Wajibu wa Kumshauri Rais ili Kumsaidia
Wasaidizi wa rais wa kila eneo wana wajibu wa kumsaidia rais wetu kwa kumshauri kufanya uamuzi sahihi na kumwachia rais kufanya uamuzi wowote ila sisi kama Watanzania tuna shauku ya kumuona kila wakali rais wetu akifanya na kutenda the right thing at the right time and doing it right. Rais asiposhauriwa vizuri, matokeo yake ni majanga kwa taifa letu, na kama ilivyo kanuni ya majanga kuwa mchuma janga hula na wakao, ushauri wowote ambao sio sahihi, rais akishauriwa, halafu katika kutekelezwa ushauri huu ukawa na matokeo mabaya, the impact ya matokeo hayo yatatuathiri sisi Watanzania wote collectively as a nation na sio rais pekee au rais na serikali yake bali madhara ya ushauri usio sahihi athari zake ni kwa Tanzania nzima kama Taifa.

Washauri wa rais mko wapi na mnafanya nini hadi kumuacha rais huku tukimshuhudiana kwa kumuona rais wetu anasema na kutenda baadhi ya mambo akiwa as if hakushauriwa vizuri, au yuko kama vile hana washauri?! .
Sisi jf tutaendelea kushauri kwa lengo la kujenga.

Kuhusu uhuru wa rais wetu kushauriwa, kupokea ushauri na kusema lolote, tulilizungumza hapa Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila...

Tanzania ni yetu sote na rais Magufuli ni rais wetu wote.
Mungu Ibariki Tanzania.
Jumamosi njema.
Paskali
 
Tatizo Paskali huwa hueleweki una simamia nini, mara Makonda awe Rais, Mara tuthibitishe kama kweli Makonda ndio Bashite, leo tena umerukia huku, yaani hutulii kwenye lane moja uka elewekaga bro, sasa hata siku ukiongea mambo ya maana una kuta watu wanakushangaa tuu maana hawajui huwa una amini kitu gani. Nakumbuka kwenye fasihi tulikuwa tukisoma kazi yoyote lazima tujue msimamo wa mwandishi, well hii siyo fasihi ila mkuu kwa kweli najaribu kutafuta msimamo wako huwa siuoni.

Ya Bashite na kuropoka tusha ongea sanaa Prezidaa ni mbishi na wasaidizi wake hawana la kufanya labda kama wamfunge kamba, ila jamaa ni sikio la kufa.
 
Umeandika vyema mpaka inafika pahala unaona kama hawa washauri wanakula kodi zetu bure maana hawafanyi kazi yao. Kibinadamu kila mmoja wetu ana udhaifu wake nukuu "nchi hizi mungu katupa tuziongoze na si malaika sasa kama binadamu tunakosea na inapotokea kujirekebisha sio dhambi wala udhaifu "mwalimu jk Nyerere.
 
Hakuna msukuma mwenye akili kama za Sizonje anaaribia watu kabila lao.

Wale wakarimu wasiompita mtu bila salaam wasiopenda uwatembelee kisha usile kwao!!

Ndio watoke kabila moja na Sizonje mwenye roho mbaya kupita ubaya wenyewe.

Jamani mara ingine mkiona [emoji84] kubwa hiyo ni housing tu ndani mashine ndogo.
 
Mie kama mtu mzima ni kweli maneno anayoambiwa mkuu mara nyingine yananiumiza, watu hawafichi tena na hii si dalili nzuri, kibaya chanzo ni yeye, mimi naamini suala la Bashite angeweza kulihandle kwa namna nyingine ili huu upepo upite. Litamvua nguo.
 
Kuwa mbayu wayu utamuelewa Pascal .msikilize anacho eleza alafu changanya na akili yako
 
Kwa hapa Tanzania hata hao washauri wa raisi nadhani wanawaza zaidi maslahi yao binafsi kwa hiyo hawana muda wa kumshauri..kama si hivyo basi wanamuogopa sana na ni utumwa kukuogopa binadamu mwenzio
 
Hivi alivyokwambia yeye huwa hapangiwi cha kufanya ulielewa? Maana yake yeye hashauriki.

Kwa mfano jana, washauri wake walimshauri asiongee lolote ndiyo maana mwanzo akasema hana la kuongea, alivyokumbuka kuwa hapangiwi la kuongea ndiyo akaanza kutoa vitisho na madharau kwa vyombo vya habari, wanavijiji wasiyojua nini kinaendelea kwenye vyombo vya habari(kama alivyosema yeye) wapo watamchagua tu 2020, wasiwasi wa nini?
 
Hii nchi inahitaji uongozi wa kiamri..uongozi wa mashauriano ulishafeli..wacha twende na huu maana unaonyesha njia..siku zote maendeleo ya nchi huletwa na uthubutu wa wachache..na wengi huachwa nyuma kama ilivyokuwa kwa nape na wenzie..
 
Wewe Mayalla vipi bwana.Kwani huwezi kuandika kitu kingine tofauti na Siasa na hasa Makonda?.Kwa mfano,serikali imezuia ORE concentrate export.Tangu Serikali imetoa tamko hilo what has been the positive/negative impacts to the nation's economy so far..Mheshimiwa Waziri Mkuu alikuwa Mauritius siku chache zilizopita na kuwaasa waMauritius kuja kuwekeza Tanzania nikawa najiuliza hawa Wamaurius wana nini cha ziada kuwekeza huku TZ nk,unaweza kuja kwenye angle hiyo tukajadili,tukaelimishana,nk.Mambo ni mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…