Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
Makada wawili wa Chama cha Mapinduzi(ccm)wanaotajwa kuusaka Ubunge wa Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro,wanadiwa kuanza kilumwaga pesa kwa watu wanaominika kuwa ni wajumbe wenye kuamua kura za maoni.
Taarifa kutoka Mwanga zinapasha kuwa makada hao wanapishana huku na kule kusaka ushawishi wa kuungwa mkono kwenye harakati zao.
Mmoja wa makada hao ni mtoto wa kigogo mmoja ambaye pia amewahi kuwa mbunge wa Jimbo Hilo .
Inadaiwa kuwa kigogo huyo ndiye anayempigia upatu mtoto wake huku naye akitajwa kutapanya pesa na kutengeneza mtandao wa kumuuza mtoto wake.
Harakari hizo zinafanyika huku kukiwa na katazo la CCM ambapo chamq hicho kimesisitiza kuacha mara moja harakati hizo .
Msimamo wa CCM ni kuwapa nafasi wabunge waliopo madarakani kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi na muda wa uchaguzi ukifika ruksa kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha kusaka ubunge.
Mbunge wa Sasa wa jimbo Hilo ni Wakili msomi Joseph Thadayo aliyerithi mikoba kutoka kwa Profesa Jumanne Maghembe.
Kwa upande wake Thadayo amesema hajui chochote kuhusiana na wanaotajwa kusaka ubunge na kwamba nguvu zake amezielekeza iatika kusimamia Mirada ya maendeleo jimboni kwake.
Mongoni mwa miradi hiyo ni Hospital ya wilaya ya Mwanga ambayo ujenzi wake upo kwenye hatua za mwisho na mradi mkubwa wa Maji utaozinufaisha wilaya za Mwanga,Same na Korogwe.
"Nadhani wanaoweza kulizungumzia hilo ni viongozi wa chama hao ndiyo wadhamini wetu, mimi maelekeza nguvu zangu kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo hospital yetu ya Wilaya"
Je, viongozi wa CCM wanasemaje,wasaka Ubunge nao wanasemaje, usikose kesho hapahapa