Wasanii 5 bora zaidi kuwahi tokea katika Historia ya Muziki wa Tanzania(Bongo Fleva)

Wasanii 5 bora zaidi kuwahi tokea katika Historia ya Muziki wa Tanzania(Bongo Fleva)

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,058
1. Lady Jay Dee

Ni wachache sana watapinga kuwa Jide hastahili kuwa mwanamuziki bora zaidi wa Bongo Fleva., moja ya silaha zake kubwa ni Consistncy aliyoonyesha tokea ameanza shughuli za muziki zaidi ya miaka 14 iliyopita.

Katika kipindi hicho wametokea kina Zay b, Ray c, Unique sisters, Juma nature, Sister P , Mandojo , Inspector, Domo kaya na Wengineo ila wakaja na wakapotea lakini Jide bado yupo ngangari kama sio ngunguri akimaintain status yake kubwa na pia kujipatia mafanikio zaidi katika biashara ya Muziki kushinda Msanii yeyote yule wa Bongo Fleva.

2. Diamond Platnumz..

Ukija kwa huyu jamaa lazima utapata views tofauti, wengine wanamkubali wengine wanampinga lakini bila ushabiki wala nini kama isingekuwa Jide basi Diamond angekuwa bora zaidi kuwahi kutokea.

Hivi ni msanii gani mwenye kiburi au aliyewahi kuwa na kiburi cha kufanya shoo na kutoza 50000 na kujaza kumbi?? Na diamond hajafanya hivyo si mara moja wala mbili hapa nnavyoandika huu uzi ana shoo Dodoma na kiingilio ni 30000/= kwa kila kichwa !!nani mwenye kiburi hiki aje kufanya Dodoma shoo kwa 30000/=

Achana na maisha yake labda ndo yanakufanya umchukie, Diamond ndiye msanii wa gharama zaidi kuwahi tokea hapa Tanzania....price yake haishuki chini ya 10 million kwa shoo za hapa ndani.

Pia Diamond amemaintain kiwango chake tokea atoke na kamwambie mwaka 2009 hadi Diamond huyu wa mdogomdogo utaona kuwa graph yake inazidi kupanda tu kwa kasi ambayo haijawahi kutokea katika muziki wetu wa Bongo.
kitu kingine kilichonifanya nione anashika nambari 2 ni mafanikio yake katika kutangaza muziki wake kimataifa , kushiriki tuzo na kushinda zikiwemo hizi za juzi za IRAWMA.

Ikumbukwe kuwa hatuangalii umeanza lini bali umepata nini ndicho kipimo kizuri cha mafanikio, wapo wakongwe wengi walioanza kabla ya Diamond ila level aliyofikia kwa sasa hawakuwahi kufikia na hiki ndicho kimemfanya ashike nafasi hii na tusisahau usemi wa Nabii hakubaliki kwao nenda Congo, Rwanda au Burundi utafahamu ukubwa wa Diamond.

3. JUMA NATURE

Huyu ni msanii ambaye anapendwa karibia na kila mtu, wanamuita msanii wa Masela.

Akiwa kwenye Peak ,Juma nature alifanikiwa kuuteka muziki wa Bongo kwa albamu yake ya Ugali., Juma nature huyu alilifanya kundi la Tmk wanaume kuwa moja ya makundi yaliyopendwa zaidi katika muziki wa Bongo Fleva.

Baada ya kuachana na Said Fella chini ya kundi la Tmk wanaume halisi Juma nature kwa nyota na mabega yake alilifanya kuwa kundi bora kiasi cha kushindana na lile lingine, kusema za ukwli kama kuwabeba Juma aliwabeba sana wale wenzake.

Kinachomfanya apitwe na Jide kupotea kwake kwa kasi ya ajabu tokea kuanza kwa mwaka 2008, na pia kinachomfanya Diamond ampite ni Juma kutoweza kupata mafanikio zaidi kwenye muziki wa nje japokuwa alishinda tuzo moja South Afrika(maoni yangu)

4 PRINCE DULLY SYKES.

huyu ndiye msanii mwenye hit nyingi zaidi katika muziki wa Bongo fleva, kuanzia julietha, salome, nyambizi, hi , ladies free, Bijou, Baby candy, shikide, na nyingine nyingi hadi kufikia Togola hit yake ya sasa huwezi mlinganisha Dully kwa ngoma kali za kibongo na msanii yeyote hapa Tanzania..

Pamoja na kuwa na Ngoma kali Dully ameshindwa kujipatia mafanikio ya nje kulinganisha na hao wa juu, kitu kinachomfanya aonekane ni msanii wa hapahapa tuu japokuwa alikataa asipewe tuzo zozote za ndani(KTMA)


5. Ally kiba...

Kabla ya kupanda juu kwa Diamond huyu ndiye alikuwa roho ya Muziki wa Tanzania, ally kiba ameufanyia muziki wa Tanzania mambo mengi makubwa japokuwa anaweza asiwe mkongwe kama Banana au Nurwell..

Sote tunakumbuka project yake na R kelly, ally kiba alipanda kwa kasi sana kuanzia mara ya kwanza namsikia kama underground kwenye ngoma aliyofanya na Mr blue+ abby skillz (maria) hadi kufikia cinderella, nakshi nakshi, usiniseme, Mc mugga hadi mwana inayobamba kwa sasa.

Ally kiba kwa research yangu anakubalika kushinda Dimond kwa hapa Tanzania maana Dimond hakubaliki kwa masela(wagumu wanavyojiita)ila kiba anakubalika.

Ukimya wake uliacha nafasi kubwa ya wengine kutake over, kinachomfanya apitwe na hao wa juu ni kutoweza kusogea hatua nyingine baada ya kufikia peak yake na ukimya wa muda mrefu..

N.B...

Hii list haihusishi wasanii wanaorap kama Prof jay na Afande sele la sivyo ingebadilika....

Pia sijaandika kwa mapenzi au kutumiwa na mtu au taasisi yyte haya ni mawazo yangu(maoni yangu) kama mtajavyotoa ninyi.
 
Barida ni maoni yako mkuu hatuna budi kuyaheshimu
 
wajua uzuri wa kitu anaujua yule anaengalia....
 
Back
Top Bottom