Wasanii Africa Mashariki wajipanga kuzisusia tuzo za MTV Africa Music Awards

Wasanii Africa Mashariki wajipanga kuzisusia tuzo za MTV Africa Music Awards

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Website ya Nairobi News imeripoti kuwa wasanii wa Afrika Mashariki wanapanga kuzisusia tuzo za MTV Africa Music Awards, MAMA.​




Wasanii hao wanazishutumu tuzo hizo kwa kutozitendea haki nchini za Afrika Mashariki mwaka huu na kwa kuwapendelea wasanii wa Afrika Kusini na Nigeria zaidi. “Uganda imeumia zaidi kwasababu kutajwa kwao pekee ni kwa collabo na Amani,” msanii mkubwa wa Kenya ambaye hakutaka kutajwa jina lake aliuambia mtandao huo.​




Umeandika kuwa wasanii waliotarajiwa kutajwa kwenye tuzo hizo ni AY, Ommy Dimpoz na Lady Jaydee, Tanzania, P-Unit, STL, Elani na Wyre wa Kenya na Jose Chameleone na Navio wa Uganda. Mtandao huo umeripoti kuwa wasanii wengi zaidi wanapanga kutoshiriki kwenye show za utangulizi za Road to Mamas zitakazofanyika Dar es Salaam kwa Afrika Mashariki.​
 
Hivi kora music awards ya wapi?
 
Nigeria na South Africa zimejitangaza sana kimuziki hata Ghana sasa hivi haiko nyuma we angalia hao MTV event zao nyingi wanaanda huko huko alafu na kule sasa hivi sector ya muziki ni biashara kubwa .

So East Africa tunaweza kuacha kulalamika na kuanza kuu-uza mziki wetu kimataifa hata itafute channel moja ya muziki itakayo base sana na East African fleva kama wao sasa hivi Nigeria wana tv za burudani kibao Dstv,mziki ni biashara usitegemee TraceTv,Sound City,Afro ndo zitatangaza mziki wetu,never!,hawa azima waanze na chakwao.

Mziki mzuri tunao kwanini tuwe wanyonge?!

Alafu Support ndo kila kitu!
 
Kwanza hao waliotajwa hao kuwania hakuna hata mmoja aliyetoa wimbo wa kuhit kustahili kuingia kule wangetuaibisha tu huyo Dimpoz na ule mduara wake na Jmartins ndo alitegemea aitwe. Mbona Domo kaitwa au yeye hastaili wanataka wao tu kila siku hata kama singo zao mbovu waache kukariri tangu waingizwe huko walituletea tuzo ngapi za Mtv hasa bongo.


Nao wakenya kususa show za Road to MAMA ni wivu tu wanataka kila mwaka iwe kwao tu Nairobi mbona miaka ikifanyika kwao hawakutoa hilo wazo la kususa. Roho mbaya tu!
 
Mbona diamond anataka tumpigie kura?
Hawajielewi
 
Tuanzishe yetu huku East Africa ama mnaonaje.
 
Back
Top Bottom