Zumbe Kimweru
JF-Expert Member
- Jul 13, 2014
- 340
- 27
wakuu, BASATA na TCRA hii ni barua ya wazi kwenu ;Sina budi niseme kwamba BASATA na TCRA bado hamjatutendea haki Watanzania kwenye sanaa kuhusu maadili kabisa kabisa ,mmekuwa watu wakushtushwa ndipo mfanye.Niwaambie tu simamieni maadili na utu wa mwanamke na utamaduni wa Mtanzania.!!!Sioni tofauti kati ya shoo ya shilole na video mbalimbali zionyeshwazo na vituo vya redio na Tv .Wasanii wafuatao wanapaswa kufungiwa kabisa ni hawa wenye sifa hizi kwenye kazi zao1.Nyimbo zenye matusi na ujumbe usio hadhi kwa utamaduni.eg .Hiphop songs nyingi hovyo.2.Video zenye ujumbe na uvunjaji maadili ya mtanzania.3.filamu za hovyo..OMBI TCRA:Fungeni vituo vya redio na Tv vinapiga na kuonyesha nyimbo na video zisizo na maadili, wazazi tumechoka Tv za ndani Uozo,za nje uozo!!! Twende wapi sasa!!! TCRA na BASATA TUOKOENI WATANZANIA!!! WATOTO WETU WANAANGAMIA JAMANI.!!BY UMOJA WA WAZAZI WENYE TV & REDIO