Wasanii ambao watakumbukwa hata kama muziki ukiwatupa mkono

Mkuu sio kama nashabikia hizi team zisizo na viwanja Ila naoma kuhoji. Hivi ni wimbo gani wa mond ambao hata ukiusikia sasahivi bado haupotezi ubora( hauchuji)???
Ukiona kwako zinachuja usifikiri na kwa wengne zinachuja......diamond ana ngoma nyingi tu ambazo ata ukisikiliza Leo bado zina vibe ile ile kwa mfano, kamwambie, mbagala, mapenzi basi, kesho, ukimuona, lala salama, na zngne nyingi
 
Usifanye mchezo na Mrs Mengi...
 
Mkuu sio kama nashabikia hizi team zisizo na viwanja Ila naoma kuhoji. Hivi ni wimbo gani wa mond ambao hata ukiusikia sasahivi bado haupotezi ubora( hauchuji)???
Diamond ndo msanii wa kwanza kutoka Africa sio Tanzania pekee tu kushinda tuzo 2 kwa wakati moja za MTV Ema , African act and world wide act
Hakuna alievunja record take hadi Leo sio kwamba atakumbukwa tu na bongo flava but Africa nzima itamlilia Sikh akiwa hayupo
 
Sugu kafanya makubwa sana katika mziki wa bongo fleva akifatiwa na sosibi kama kuna anayemkumbuka then profesa j wengine ndowafate,mziki ulikuwa unaonekana wakihuni kama singeli vile lakini kwa tungo zao mziki wa bongofleva ulisimama
 
Sugu hajafanya cha maana kwenye bongo flava, kwanza alikuwa analazimisha fani tu
 
Mziki wetu una phase 4
1. Sugu alianza kurap kuitambulisha bongo fleva elimu ya mtaani wazee wa deiwaka yaani mziki wa wahuni

2. Project jay ...huyu ndo akailainisha kidogo hip hop kutokana na tungo zake ikaanza kupendwa na rika zote.
Ukawa mziki wa kizazi kipya

3. Juma nature, Dully Sykes.... Hawa aliitransform kutoka kutoka kurap had I kuimba , wabana pua wakaanzua hapa mziki ukawa biashara kubwa , pesa inaingia na wakajitokeza wasanii kibao

.Diamond platnumz... Huyu phase yake akaleta mapinduzi ya kweli ya kuiongezea bongo fleva thamani, kufanya video Kali zaidi, promotion kubwa ya Kazi zake , kuset price kubwa ya shows, kutafuta masoko ya kimataifa.
Nakumbuka Diamond alizamia hadi harusi ya Psquare wabongo wakawa wanamcheka wakati ameenda kufanya video ya remix ya number one
Wasanii wengine ndo wakazinduka akili kufanya video nzuri south Africa na wengine walikuwa wamepumzika mziki wakapata nguvu na wakaamua kurudi tens kwa nguvu ya mashabiki waliokuwa wanamchukia aliekuwa juu.
Hadi Leo maybe tusubiri phase mpya uko mbeleni
 
Sugu kafanya makubwa sana katika mziki wa bongo fleva akifatiwa na sosibi kama kuna anayemkumbuka then profesa j wengine ndowafate,mziki ulikuwa unaonekana wakihuni kama singeli vile lakini kwa tungo zao mziki wa bongofleva ulisimama
Mkuu hilo hawataki kuliona wanachoangalia kwa sasa ni hawa tu waliopo. Lakini ikumbukwe hata hayo mafaniko ya kina mond kwa sasa yasinge kuwepo bila hawa wakongwe. Hebu jiulize hizi nyimbo za ovyo ovyo zinazopigwa sasa kama zingekuwa ndo zinaimbwa kipindi kile bongo fleva ikipingwa kuwa ni uhuni je unadhani ingekuwaje?.
Hebu ikumbukechemshabongo ya pro j, darubini kali ya Afande, kamanda ya dazi nundaz.
Hivi hawa wasanii wa sasa kuna mwenye uwezo wa kutunga tungu kama zile.
Utakuta ngoma za ajabu ajabu mara sijui kijuso, mara nataka kulewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…