- Thread starter
-
- #141
Kwa Vanessa umepuyanga kaka1. Prof jay
watu wa mwanzo kuifanya bongo hip hop kuwa ya maana na kupendwa na watu wa aina zote mfano: wimbo wa zali la mentali
2.Ay
Mzee wa bongo commercials na huyu si kwa upande wa tz tu ni hadi Afrika mashariki nzima.. yeye ndo aliyetutangaza kwa kufanya muziki international.. kabla ya diamond hakuna aliyekuwa na nyimbo zinazonguushwa katika intermational tv stations kama trace
3.Ray c na Jay dee
Jay dee anasifika kuwa legendary wa kike ama "Bongo flava goddess " na hii ni stahiki yake kwa kukaa muda mrefu katika game na kuchukua tuzo za ndani na nje. Ana heshima kubwa tu
Ray c alikuwa ni mpinzani wake mkuu na japokuwa ameanguka lakini Ray c ndiye alieileta show biz bongo yaani life la kistar bongo kuanzia fashion hadi scandals na ndiye aliyejulikana kama "sexiest female artist in East Africa".
muziki wake ulikuwa na nguvu na uliwavutia mabinti wengi kuimba na kuonesha sexuality katika muziki.. hivyo ray c ameacha gap kubwa na hatosahaulika kirahisi na hata skendo za madawa ni plus kwake
4.dully sykes na Mb dog huwezi kuiongelea bongo flava ya kuimba bila dully sykes..
huwezi kuiongelea bongo flava ya nyimbo tamu za mapenzi iliopo sasa bila kumtaja mb dog... hivyo impact yao ni kubwa kwa muziki tulionao kwa sasa
5.Saida karoli
Ukiongelea muziki wa asili kwa kanda yetu ya Afrika mashariki bhasi huwezi kuacha kumuongelea.. ni mkongwe aliyepo hai.aliitangaza Tanzania vyema hasa katika tuzo za nje kama kora awards
6.Diamond ni mkubwa kuanzia Tz, Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla.. aliikuta bongo flava katika hali nzuri lakini yeye ndiye aliyeiongezea thamani kwa video kali na kupandisha thamani ya muziki wetu kwa malipo na tuzo za kimataifa..
Ndiye msanii kutoka afrika mashariki ambaye unaweza kumuita star wa Afrika
7.Vanessa mdee
Huyu bado impact yake haijaonekana kutoka na muziki wa team uliopo lakini kwa upande wa kikeni hakuna aliyewahi kufanikiwa kimataifa kama yeye ... naamini muda utaongea
Over