Wasanii ambao watakumbukwa hata kama muziki ukiwatupa mkono

Wasanii ambao watakumbukwa hata kama muziki ukiwatupa mkono

1. Prof jay
watu wa mwanzo kuifanya bongo hip hop kuwa ya maana na kupendwa na watu wa aina zote mfano: wimbo wa zali la mentali

2.Ay
Mzee wa bongo commercials na huyu si kwa upande wa tz tu ni hadi Afrika mashariki nzima.. yeye ndo aliyetutangaza kwa kufanya muziki international.. kabla ya diamond hakuna aliyekuwa na nyimbo zinazonguushwa katika intermational tv stations kama trace

3.Ray c na Jay dee

Jay dee anasifika kuwa legendary wa kike ama "Bongo flava goddess " na hii ni stahiki yake kwa kukaa muda mrefu katika game na kuchukua tuzo za ndani na nje. Ana heshima kubwa tu

Ray c alikuwa ni mpinzani wake mkuu na japokuwa ameanguka lakini Ray c ndiye alieileta show biz bongo yaani life la kistar bongo kuanzia fashion hadi scandals na ndiye aliyejulikana kama "sexiest female artist in East Africa".
muziki wake ulikuwa na nguvu na uliwavutia mabinti wengi kuimba na kuonesha sexuality katika muziki.. hivyo ray c ameacha gap kubwa na hatosahaulika kirahisi na hata skendo za madawa ni plus kwake

4.dully sykes na Mb dog huwezi kuiongelea bongo flava ya kuimba bila dully sykes..
huwezi kuiongelea bongo flava ya nyimbo tamu za mapenzi iliopo sasa bila kumtaja mb dog... hivyo impact yao ni kubwa kwa muziki tulionao kwa sasa

5.Saida karoli
Ukiongelea muziki wa asili kwa kanda yetu ya Afrika mashariki bhasi huwezi kuacha kumuongelea.. ni mkongwe aliyepo hai.aliitangaza Tanzania vyema hasa katika tuzo za nje kama kora awards

6.Diamond ni mkubwa kuanzia Tz, Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla.. aliikuta bongo flava katika hali nzuri lakini yeye ndiye aliyeiongezea thamani kwa video kali na kupandisha thamani ya muziki wetu kwa malipo na tuzo za kimataifa..
Ndiye msanii kutoka afrika mashariki ambaye unaweza kumuita star wa Afrika

7.Vanessa mdee
Huyu bado impact yake haijaonekana kutoka na muziki wa team uliopo lakini kwa upande wa kikeni hakuna aliyewahi kufanikiwa kimataifa kama yeye ... naamini muda utaongea

Over
Kwa Vanessa umepuyanga kaka
 
kwangu ni hawa Dully Sykes, Fid Q, Ray C, afande sele, Ali Kiba, Lady Jaydee, ngwair... hawa unaona wanafanya muziki kwa passion, wana talent na mashairi yanaokujia kichwani kila mara...Diamond naona alikuwa akifanya muziki mzuri enzi za Mbagala na kamwambie, hizi za siku hizi ni Big G hazidumu labda aache legacy kama mwanamuziki aliye exploit muziki kibiashara zaidi
 
Ohooo!!!
898371f0a44796a942429abc51083c30.jpg
irrelevant!
 
Umemsahau BIZIMAN
kwangu ni hawa Dully Sykes, Fid Q, Ray C, afande sele, Ali Kiba, Lady Jaydee, ngwair... hawa unaona wanafanya muziki kwa passion, wana talent na mashairi yanaokujia kichwani kila mara...Diamond naona alikuwa akifanya muziki mzuri enzi za Mbagala na kamwambie, hizi za siku hizi ni Big G hazidumu labda aache legacy kama mwanamuziki aliye exploit muziki kibiashara zaidi
Umemaliza
 
Nyimbo zote Duniani huwa zinachuja - Hakuna wimbo ambao huwa hauchuji Dunia, ila Kila mtu ana nyimbo zake ambazo huwa zinamkumbusha kumbukumbu fulani kwenye maisha.Basi. Laiti kama Ingekuwa kuna nyimbo hazichuji, Msanii angekuwa anatunga WIMBO Mmoja tu then anaacha Muziki - Kwanini utoe Ngoma mara kwa mara " WHY " Wakati nyimbo zako hazichuji ?

Note. Ukiona mtu anatumia vijineno kama Ujumbe, Sauti, Mzuri Mzuri, KUdumu kwa wimbo, Live band - Ujue ni mpuuze GRADE A, MPUUZE
...kuna nyimbo na sio nyimbo tu, hata movie kuna ambazo ni classic, na nyingine zinakuja kwa kiki kubwa ila baada ya muda zinapoteza ladha hadi unaona aibu kusikiza..kuna zile nyimbo za Mr. Nice zilivyobamba leo hii utamsikia akisikiliza? ila kuna nyimbo za akina dully sykes, ray c, lady jaydee akisililiza mtu haonekani mshamba
 
Mkuu sio kama nashabikia hizi team zisizo na viwanja Ila naoma kuhoji. Hivi ni wimbo gani wa mond ambao hata ukiusikia sasahivi bado haupotezi ubora( hauchuji)???
Op/ chaka, mada na tamko lako haviendani
 
Wanafanya style tofauti ya Muziki.

Hapo unamshindanisha Tupac na R.kelly au Michael Jackson na Bob Marley.

Kila mmoja kafanya lake kwa upande wake.
Sawa ila ujumbe unaobebwa kwenye tungo na ubora wa muziki bado unabaki pale pale. Kwani hao wasanii wanashindwa nini kuandika tungo za kueleweka katika hizo hizo style zao.?
 
Inategemea muziki umeanza kusikiliza lini, Mimi kwangu diamond ndo sitamsahau wengne Hanna kitu laba kidogo prof jay
 
mbn hamjagusa Saleh Jabir...hapo watoto wa 90 hawatamwelewa
 
Wakati MTOTO WA DANDU anafanya mziki MBELE ulimskiliza? Wakati SUGU anaimba na Peter Andre, uliiskia ile ngoma? Wakati JD anaperform KORA SA, AY alikuwa wapi?
Mtoto wa juzi hawezi elewa hata ukimwambia kuna Mtz kapiga cypher BET chin DJ PREMIER hajui
 
Sawa ila ujumbe unaobebwa kwenye tungo na ubora wa muziki bado unabaki pale pale. Kwani hao wasanii wanashindwa nini kuandika tungo za kueleweka katika hizo hizo style zao.?
Kwani hawajawahi kuandika Nyimbo za ujumbe?!

Ulitaka Nyimbo zao zote ziwe za ujumbe?Alafu wapate sifa bila kuwa na hela?!

Muziki ni biashara huria kila mtu anafanya anachoweza....Ila wewe unataka watu wote waimbe ujumbe kama Afande Sele
 
Nadhani mada original ni kuwakumbuka kwa kile kilichofanyika kwa bongoflav, huyu nond uwezo na kipaji cha kutumbuiza anacho lkn mchango mkubwa upo kwa hao waliowatengenezea njia. Narudia kusema, unless hujui bongoflav ilipotoka huwezi kuongea mafanikio ya mond bila sugu. Ni sawa na kusifia kilele cha ghorofa bila kujua foundation yake
Wewe unaejua Bongo flava unataka kusema Msingi ulijengwa na Sugu peke yake na hakukuwa na Wengine?!

Tuelewane hapa tafadhali Sugu alikuwa na mchango wake na naupa heshima pia ila sio kiasi cha kumfanya kama nabii wakati kuna watu kibao walifanya makubwa kuliko yeye.

Kwangu Profesa Jay anastahili heshima nyingi kuliko Sugu yeye kuanza haimaanishi wote waliokuja baada yake hawana uwezo kuliko yeye.
 
Back
Top Bottom