DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Kwa takribani kipindi cha miezi miwili sasa, nchini Tanzania kumeshuhudiwa kampeni za kimtandao zinazoendeshwa na baadhi ya watu maarufu na wanaharakati, zikihamasisha umma kusitisha kuzipa sapoti kazi za wasanii wa Tanzania. Kampeni hizi zimehusisha kutosikiliza nyimbo zao, kutohudhuria matamasha yao pamoja na kupuuza maudhui wanayochapisha kwenye mitandao ya kijamii.
Hatua hiyo imeibua mjadala mpana katika jamii hususani kwenye majukwaa ya kidigitali. Wapo wanaoziunga mkono kampeni hizo wakiziona kama njia ya kuwawajibisha wasanii, huku wengine akiwemo baadhi ya viongozi na wadau wa sanaa wakipinga wakidai si sahihi kumchukia au kumbagua msanii kwa misimamo yake ya kisiasa au kwa kuunga mkono Serikali au chama fulani, wakisisitiza kuwa huo ni uhuru wa kisanaa na sehemu ya kujitafutia kipato.
Lakini je, kampeni hizi zimeibuka bure?
Chanzo cha Kampeni: Sanaa na Dhamana kwa Jamii
Kwa muda mrefu kumekuwepo na mtazamo kuwa msanii ni kioo cha jamii. Kupitia sanaa yao, wasanii huathiri mitazamo, maamuzi na mienendo ya jamii. Umaarufu wao huwapa nguvu kubwa ya kuhamasisha, kuonya au kuunganisha jamii katika nyakati nyeti. Kwa upande mwingine, wasanii hutegemea jamii hiyo hiyo kama chanzo kikuu cha kipato na uhai wa kazi zao.
Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imeshuhudia madai na malalamiko ya mara kwa mara kuhusu matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu, ikiwemo mauaji, utekaji, vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kisiasa, kukatwa kwa wakosoaji wa Serikali. Haya ni masuala mazito yanayogusa maisha ya wananchi wa kawaida ambao ndio wasikilizaji zaidi wakiwa mashabiki na walaji wakuu wa kazi za wasanii.
Hata hivyo, katika mazingira haya, wasanii wengi wamechagua kukaa kimya. Badala ya kutumia majukwaa yao makubwa kukemea au angalau kuonesha mshikamano na waathirika, baadhi yao wameonekana wakishiriki au kusifia majukwaa ya mamlaka ambazo mara nyi zinatuhumiwa kushindwa kukemea au kukomesha matukio hayo. Kimya hicho kimefasiriwa na sehemu ya umma kama kutojali mateso ya wananchi.
Ukimya, Upendeleo na Hasira ya Umma
Zaidi ya hapo, imeonekana kuwa ni rahisi kwa baadhi ya wasanii kusimama kwenye majukwaa ya Serikali au chama tawala, lakini ni jambo gumu kwao kuonekana kwenye majukwaa ya vyama vya upinzani. Wengine wamenukuliwa wakitoa kauli zinazodhalilisha au kudhihaki wananchi wanaokosoa Serikali, hususan kwenye masuala nyeti kama ajira, maisha magumu na haki za msingi.
Katika muktadha huo, hasira ya umma inaonekana kuelekezwa si kwa sababu wasanii wanaunga mkono Serikali, bali kwa sababu wanashindwa kusimama upande wa wananchi wanapokumbwa na dhuluma.
Umma unauliza: kama msanii anaweza kuitumia sauti yake kutangaza bidhaa, kampeni au sera fulani, kwa nini ashindwe kuitumia sauti hiyo hiyo kutetea uhai, haki na utu wa watu waliomuinua?
Wanavuna walichopanda
Si ajabu, kwa sasa kumeshuhudiwa kundi la wasanii, hususan wa muziki wa Bongo Fleva, wakianza kuomba radhi kwa umma. Katika kauli zao, huku ikiwepo hofu kwao kwamba kampeni hizi zinaweza kuathiri mitindo yao ya maisha na vyanzo vyao vya kipato. Hatua hiyo nayo inazua tafsiri kuwa msukumo wa kuomba radhi unatokana zaidi na hofu ya kupoteza sapoti ya kifedha, kuliko msimamo wa dhati juu ya maslahi ya umma.
Kwa mtazamo mpana, hali hii ni funzo kwamba umaarufu una gharama na wajibu. Wasanii wanapochagua ukimya au upande mmoja katika nyakati za mateso ya jamii, wanapaswa kuwa tayari kukabiliana na matokeo ya uchaguzi wao. Kampeni hizi, kwa namna fulani, zinaonesha kuwa umma nao umeamua kutumia nguvu yake pekee "sapoti" kama chombo cha kudai uwajibikaji.
Hitimisho
Kwa msingi huo, ni vigumu kukwepa hoja kwamba wasanii wanavuna walichopanda. Walipopata nafasi ya kusimama na umma wakachagua kukaa kimya au kupuuza vilio vya wananchi, hawapaswi kushangaa umma unapoamua kuwanyima sapoti. Katika jamii inayozidi kuwa na uelewa, sanaa haiwezi kutenganishwa na dhamana ya kijamii. Msanii si burudani tu, bali ni sauti; na sauti isipotumika kwa haki, huweza kupoteza uhalali wake mbele ya jamii.