Wasanii igeni kwa Rich Mavoko

kijanamtanashati

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2014
Posts
516
Reaction score
905
Sikuwahi kusikiliza nyimbo za huyu jamaa, kama bahati kupita pita youtube nakutana na nyimbo ya jamaa inayokwenda kwa jina la "ibaki story" nimejikuta natafuta nyimbo zake za nyuma, kwa kifupi jamaa anaweza kutumia vizuri lugha yake ya Kiswahili, hakuna makosa tunayoyaona kila siku kutoka kwa wasanii wengine.

Sehemu ya kuweka "R" wanaweka "L" badala ya kusema "siri" wakimaanisha "secret" wanasema "sili", "dharau" wanasema "zalau" makosa ya aina hii yanaharibu kabisa hamu ya kuendelea kusikiliza nyimbo yenyewe, hasa pale unapokuta nyimbo nzima wanapuyanga wa kuchanganya "R" na "L".

Wasanii wetu mjifunze kutoka kwa mwenzenu Richi yeye anawezaje kutumia Kiswahili vizuri halafu wengine mshindwe? Hongera sana Richi Mavoko kwa hili, unastahili pongezi!!
 
Una umri gani na upo mkoa gani?!

Yaani mpaka umri huo ujawahi kusikia Wimbo wowote wa Richard?!
 
Karibu uraiani mkuu,hv ulifanya kosa gani wakakuweka jela kipindi chote hicho? Yaani leo ndo unaisikia ngoma ya Mavocco
 
Kweri kabsa hanayua kiswahiri.
 
Yeah mtoto wa mama richard kwenye matumizi sahihi ya lugha adhim [emoji1] ya kiswahili yupo vizuri n mwingine ni Kassim mganga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…