kijanamtanashati
JF-Expert Member
- Aug 22, 2014
- 516
- 905
Sikuwahi kusikiliza nyimbo za huyu jamaa, kama bahati kupita pita youtube nakutana na nyimbo ya jamaa inayokwenda kwa jina la "ibaki story" nimejikuta natafuta nyimbo zake za nyuma, kwa kifupi jamaa anaweza kutumia vizuri lugha yake ya Kiswahili, hakuna makosa tunayoyaona kila siku kutoka kwa wasanii wengine.
Sehemu ya kuweka "R" wanaweka "L" badala ya kusema "siri" wakimaanisha "secret" wanasema "sili", "dharau" wanasema "zalau" makosa ya aina hii yanaharibu kabisa hamu ya kuendelea kusikiliza nyimbo yenyewe, hasa pale unapokuta nyimbo nzima wanapuyanga wa kuchanganya "R" na "L".
Wasanii wetu mjifunze kutoka kwa mwenzenu Richi yeye anawezaje kutumia Kiswahili vizuri halafu wengine mshindwe? Hongera sana Richi Mavoko kwa hili, unastahili pongezi!!