Wasanii Irene Uwoya na Steve Nyerere waitwa BASATA baada ya kuwarushia Wanahabari pesa

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka Wasanii hao kufika katika ofisi za Baraza hilo siku ya kesho, Julai 17 kufuatia kitendo chao cha kuwarushia fedha Waandishi wa Habari wakati wa Kikao jana Julai 15

Hata hivyo, Uwoya amewaomba radhi Waandishi kufuatia kitendo hicho kilichopelekea baadhi ya waandishi kuharibu baadhi ya vifaa vyao kutokana na vurugu zilizotokea wakati wa kudaka fedha hizo alizokuwa anarusha

Amesema hakufanya hivyo kwa lengo la kudhalilisha waandishi wa habari kama ambavyo imetafsiriwa na watu wengi, kwani dhahiri anatambua umuhimu mkubwa wa waandishi wa habari katika jamii

Tanzania hakuna waandishi wa habari bali full Kanjanjas!
 
Sijaelewa! Kwahiyo kosa la Irene ni kurusha pesa ambazo kila leo huwa zinarushwa kwenye kumbi za starehe; au kosa lake ni kuwarushia Waandishi wa Habari?!

Kama mpaka sasa hujagundua Kosa lake basi nikiri wazi wazi kuwa huenda Tanzania ya sasa kuna Watu wengi wenye tatizo Kubwa la Akili ila Wao hawajajigundua tu.
 
Tushasema BASATA wamekosa kazi sasa kitu chochote kidogo kikitokea inabidi wakirukie ili waonekane relevant.
 
Back
Top Bottom