Pre GE2025 Wasanii kujiingiza kwenye siasa na kuwa machawa ipi faida yao kama nao wanashiriki kuingiza wananchi shimoni?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu salam,

Tumekuwa tukiona wasanii wakitumika kwenye kampeni na kujiingiza kwenye shughuli za kisiasa ambao karibuni imekuwa too much. Huko nyuma CCM walikuwa na bendi yao ikiongozwa na Hayati Kapt. Komba, kidogo kidogo wasaanii wakaanza kuingizwa kuburudisha, kwa Hayati Magufuli ndio ikawa kama usimikwaji rasmi ya Wasii kuwa chawa.

Wasanii makundi kwa makundi wakanyoosha moja kwa moja CCM na kidogo wakaenda kwa wapinzani.

Tukumbuke wasanii wananguvu kubwa ya ushawishi hasa kwa watu ambao hawajaelimika na kufuata mkumbo ambao ndio wengi. Akimuona tu Diamond anaunga mkono juhudi, au yuko kwa wazee wa babadiliko hata hafakirii mara mbili naye anakuwa chama husika, msanii huyo akipotosha taarifa fulani ni rahisi sana kwa wananchi huyu kukubaliana na alichosema.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mpoto akaanza vizuri na mjomba lakini ukiangalia sasa hivi ni takataka, yaani yeye na Mwijaku ni kama mapacha, tofauti mmoja anafanya upuuzi wake kwa mashairi mwingine anatiririka kwa kuongea kawaida kila anapopata nafasi, wasanii wa maigizo karibu wote ni kichefuchefu, waimbaji kidogo kuna baadhi wanajielewa.

Kwa namna hii, ipi faida ya kuwa na wasanii kama nao kwa namna kubwa wanakuwa sehemu ya upotoshaji?

Najua nyuki wa mama mtakuja, oooh usimpangie mtu, wanafanya wanavyotaka blaaa blaa blaaa, ila wote tunajua wanafanya hivi kwa maslahi binafsi ambayo yakitolewa hutawaona hapo tena, lakini wengine ni rafiki na ndugu zetu na wanasema wazi kabisa naelewa hiki nnachofanya ni upumbavu na napotosha wengi, lakini na mimi nataka niwe na nyumba au gari nzuri kwahiyo potelea pote!

Hawaoni umuhimu wa kuelimisha ili rasilimali hizi zisitumike vibaya kwake bali hata mtoto wake kesho na mjukuu wake keshokutwa afaidike na asije kuishi kwa tabu na umasikini wa kutupwa?

NB: Burudani tunaitaka lakini jukumu la wao kuelemisha jamii kama wasanii na nguvu ya ushawishi waliyonayo ikiishia kwenye uchawa nani ataikomboa jamii?

Au mpaka wageukwe waanze kutaabishwa na utekaji ubishe kwenye milango yao ndio wataamka kutoka kwenye usingizi mzito walionao.

Pia soma:
~ Mwijaku anajikuta nani hasa? Ifike mahala tuanze gomea biashara za chawa wote, unfollow kwenye mambo yao yote!
~ Machawa wanapata wapi pesa? Aristote amjengea ghorofa la kwenda mlinzi wake
~ Samia Challenge: kampeni kwa niaba ya mama?
~ Wasanii wetu tumieni mitandao na umaarufu wenu kukemea utekaji na mauaji yanayoendelea
~ Wasanii wa Tanzania mbona hawakemei utekaji na mauaji yanayoendelea nchini?
~ Nay wa Mitego na Nitasema: Movie ya Chato Part two ni Kizimkazi!
~ Ney wa Mitego aitwa BASATA kujadili wimbo wake wa ‘Nitasema’
~ Kuelekea 2025 - Haya ndiyo makosa ambayo BASATA wanamtuhumu Nay wa Mitego kutokana na wimbo wake wa Nitasema
- Kuelekea 2025 - Diamond Platnumz: Wana Mbeya mnatakiwa kutembea kifua mbele kwa kumchagua Tulia, tusikubali kulipoteza hili jembe


JANUARY
  1. Pre GE2025 Wasanii wakata Keki ya birthday ya Rais Samia na kutoa zawadi ya Mitungi Soko la Feri! Wakitoka hapo wanapitisha kikombe!
  2. Chawa na Samia Challenge, kuna kitu chawa wanaweza zaidi ya kujipendekeza?
  3. Ommy Dimpoz: Dhambi zote za Rais Samia apewe Tundu Lissu
  4. Musiba: CCM walikusanya wasanii Dodoma bila faida na CHADEMA haikuzimwa
  5. Hivi hawa wasanii wa bongo kwenye mkutano wa CCM kazi yao kubwa ni nini?
  6. Inasikitisha pengine wasanii wetu hawapo huru wameamua kujihusisha na siasa ili kulinda kazi zao na mali zao
  7. Wasanii wa Bongo movie waliokuwa CHADEMA wahamia CCM
  8. Wasanii mbalimbali watua Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wa CCM: Hivi, Wanaenda kwa lengo la Maendeleo au Wanatumika kwa Agenda za Kisiasa?
  9. Roma Mkatoliki abariki wasanii kupanda kwenye majukwaa ya CCM. Kwa sababu yanawanufaisha.
  10. Baba Levo: Nikipewa kadi ya CCM kwenye mkutano mkuu, nitamrudishia Zitto Kabwe kadi yake ya ACT
  11. Tofauti ya CCM na CHADEMA: CCM wanatumia Show Off ya Magari, mabango na Wasanii kutangaza Mkutano wao,Chadema wanatumia midahalo yenye hoja nzito!

FEBRUARY
  1. Steve Nyerere akusanya wasanii na viongozi wa dini kugawa mitungi bure kwa wakina mama ili "kuunga mkono juhudi" za Samia
  2. Wasanii wa Injili wakiongozwa na Mwamposa wajipanga kukutana Mlimani City kumuombea Rais Samia!
  3. Shilole azindua mama lishe na Samia
  4. Wasanii Ay, Madee na Chege tumeridhia kuitwa Samia Kings baada ya kushiriki pamoja katika shughuli za CCM
  5. Pre GE2025 Huu ndiyo ubunifu wa wasanii au ni kujitoa akili?
  6. Dar: Viongozi wa Dini kufanya maombi kwaajili ya Rais Samia kuelekea Uchaguzi 2025
  7. Wasanii wanahamasisha vijana kushiriki UVCCM marathon, ila kwenye baadhi ya mambo mfano kutekwa kwa raia wapo kimya
  8. Ni lini Wasanii wa Muziki na Filamu wa Tanzania Watahamia Dodoma ili kuunga Mkono CCM?
  9. Ni jambo moja kwenda kwenye shughuli za CCM kikazi, ni jingine kuvaa magwanda yao ya kijani na kuwa chawa. Wasanii wa bongo hamna thamani kabisa
  10. CCM inatumia pesa nyingi kwa wasanii na michezo kuficha ukali wa CHADEMA kwenye media na mitandao kuelekea 2025
 
Sema wasanii wa Tanzania jau sana na wanazingua hii ni kutokana wengi wao kuwa na shule ndogo kichwani ila kusema ukweli Magu aka Jiwe mnamsingizia sana haya mambo ya CCM kutumia wasanii yalikuwepo hata wakati wa kikwete
 
Hao wasanii hawajielewi kabisa

Hivi mtu mwenye akili timamu, unawezaje kukishabikia chama Cha CCM, ambacho kinatuhumiwa Kwa utekaji na kuua raia wasio na hatia??😭
 
Wasanii nao ni wananchi wana haki ya kufanya wanachoona kinawafaa ili mradi hawavunji sheria. Kama msanii anakukera mpotezee. Ninawapongeza sana wasanii wa Tanzania kuwa upande wa ushindi.
 
ile kauli ya kuleni kwa urefu wa kamba zenu bila kujali ina athari kiasi gani kwa taifa letu na ndiyo maana unawaona wanachakarika kweli kweli kuitengeneza kesho yao kwa machozi, jasho na damu ya wasio na uwezo/masikini.
 
Kati ya kundi wasiojielewa ni hao, wao wanawaza kula yao tu. Wakati sanaa yao inawategemea wananchi wote. Ni kususia tu kazi zao. Usiidharau nazi, embe tunda la msimu...✍️
 
Elimu ndio mkombozi wa kweli na wa uhakika na ukombozi wake huwa haujali ni muda upi.

Ukikosa elimu utamlaumu kila anayekatiza mbele ya macho yako, utamtwika mzigo wa lawama hata asiyehusika.
 
Wasanii nao ni wananchi wana haki ya kufanya wanachoona kinawafaa ili mradi hawavunji sheria. Kama msanii anakukera mpotezee. Ninawapongeza sana wasanii wa Tanzania kuwa upande wa ushindi.
Hata yeye anayeona udhaifu kwa upande wa wasanii angekuwa ni msanii hivi sasa angelaumiwa na watu wengine.

Anaongea hivi kwa sababu sio msanii hivyo hizo faida wanazozipata yeye hazipati kwa muda huu.
 
Sema wasanii wa Tanzania jau sana na wanazingua hii ni kutokana wengi wao kuwa na shule ndogo kichwani ila kusema ukweli Magu aka Jiwe mnamsingizia sana haya mambo ya CCM kutumia wasanii yalikuwepo hata wakati wa kikwete
Ndio sababu ya uwepo wa kundi la taarabu la TOT.
 
Hao wasanii hawajielewi kabisa

Hivi mtu mwenye akili timamu, unawezaje kukishabikia chama Cha CCM, ambacho kinatuhumiwa Kwa utekaji na kuua raia wasio na hatia??😭
Unao ushahidi wowote unaoweza kuupeleka mahakamani? zinaweza kuwa ni tuhuma bila ya ushahidi.
 
Kila mtu anaangalia maisha yake huko Ccm wanaenda kufata pesa tu na vyama vingine kama vinahitaji wasanii waweke pesa pia maana hata hao wanasiasa wote wanataka madaraka ili watengeneze maisha yao hamna mwenye nia njema hata mmoja.
 
UPUMBAVU!
wewe kama unawapenda sana vyama vya upinzani kaimbe kwenye mikutano yao,hakuna wa kukuzuia.
WAPUMBAVU wengi humu jf wanajifanya wanapigania demokrasia bila kujua demokrasia nini.Kwa akili zao fupi wanafikiri demokrasia ni kuunga mkono vyama vya upinzani tu na kupinga serikali.
 
Kama Roma na Nay wa mitego walivyo machawa wa Chadema. Hovyo sana.hawajitambui
 
Tanzania kila mtu anapambana na Hali yake kwa maana ukiifuata mifumo inakula kwako ikibidi hata ukijizima data yaani kuahirisha kufikiri kwa nafsi tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo
 
Tanzania kila mtu anapambana na Hali yake kwa maana ukiifuata mifumo inakula kwako ikibidi hata ukijizima data yaani kuahirisha kufikiri kwa nafsi tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo
Sio kweli ni mindset tu za wapuuzi wachache ndio zitaufikisha huku. Ingekuwa kila mtu anafanya hivyo sidhani hata jamiiforums ingekuepo leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…