Ujumbe wa Mbunge wa Muheza, Tanga na msanii MwanaFA akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Mohamed Mchengerwa kuhusu suala la mfuko wa utamaduni na sanaa ya Tanzania.
Sanaa imeajiri watu wengi kuna familia zinakula, watoto wanaenda shule kwa ajili ya sanaa. Awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu imeamua kuwashika mkono kwa kuwapa mikopo isiyo na riba ili kuboresha biashara yao ya sanaa.