themagnificient
JF-Expert Member
- Dec 13, 2016
- 1,033
- 3,720
Hivi karibuni msanii Diamond Platnumz alizindua bidhaa yake ya Diamond karanga huku akijinasibu na kujitamba kuwa bidhaa ni yake na ananunua karanga hizo kutoka kwa wakulima na kuziboresha kwa kuziongezea vionjo mbali mbalimbali ili kuziuza
Kutokana na tangazo lake kuwa bidhaa hiyo ni ya kwake mwenyewe iliwafanya wasanii wenzake kujitokeza kwa wingi kumpa support Diamond kwa kupost picha na video wakitumia bidhas yake ya Diamond karanga wakiwa na nia njema ya kumsuport kijana mwenzao katika biashara yake mpya.
Lakini ukweli ni kuwa hizi karanga za Diamond hazikuanza kuuzwa leo sokoni bali zina muda mrefu tu na zinatengenezwa na kampuni ya SMART Industries ambao pia ni watengenezaji wa CHAMA, so kilichobadilika hapa ni kurudishwa sokoni kwa mara nyingine zikiwa na cover la blue baada ya toleo la kwanza kutofanya vizuri sokoni hivyo ikawabidi watumie mbinu ya kumtafuta mtu maarufu wa kuzipa promo ambaye ni Diamond Platnumz kwa makubaliano maalumu
Lakini baadhi ya wasanii wenzake bila kujua mwenzao kashapiga mkwanja mrefu wa kuzipa promo, wao bila kujua wakaanza kuzitangaza kwenye page zao wakijua wanamsaidia kijana mwenzao kwenye bidhaa yake mpya tena wengi wakiwa ni wasanii wakubwa wenye majina na brand kubwa
Kumbe mwisho wa siku wanamtajirisha Muhindi ambaye ndiye mmiliki wa hii bidhaa bila kujua thamani na Brands zao ni kubwa kiasi gani
Naweza nikaonekana namchukia Diamond lakini walaa sina chuki nae bali najitahidi kuwaelimisha wasanii wasitumike kichwa kichwa huku wakilia wana majina makubwa lakini ni masikini