Wasanii kumpigia promo Diamond kwenye bidhaa yake ya karanga ni uzuzu wa kiwango cha juu

Wasanii kumpigia promo Diamond kwenye bidhaa yake ya karanga ni uzuzu wa kiwango cha juu

Chibu Perfume sio yake ya Kusaga.

Karanga sio zake za muhindi.

Gari X6 sio lake la Marehemu Seki.

Nillan sio mtoto wake ni wa Marehemu wa Uganda.

Huko mbele tutakuja kusikia hata ile nyumba kule Madale sio yake ni ya Babu Tale.
Hadi jinsia sio yake niya Qboy
 
Hata wewe unaweza kuzitangaza mradi huibi cha mtu Wala hutoi roho ya mtu.
 
Chibu Perfume sio yake ya Kusaga.

Karanga sio zake za muhindi.

Gari X6 sio lake la Marehemu Seki.

Nillan sio mtoto wake ni wa Marehemu wa Uganda.

Huko mbele tutakuja kusikia hata ile nyumba kule Madale sio yake ni ya Babu Tale.

Duh , kaka unaonekana uko well informed au tuseme unamfatilia sana Diamond, habari zote hizo umezipata wapi?
 
Chibu Perfume sio yake ya Kusaga.

Karanga sio zake za muhindi.

Gari X6 sio lake la Marehemu Seki.

Nillan sio mtoto wake ni wa Marehemu wa Uganda.

Huko mbele tutakuja kusikia hata ile nyumba kule Madale sio yake ni ya Babu Tale.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] yaani kila kitu fake ndo maana kiba anamuumiza sana kichwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha wivu... mtu hawezi kuwekeza kama ameona jina kama analotumia lilitumika!?
 
Jamani Kuna haja ya mtaalam wa maswala ya share ktk biashara , watoe darasa humu jf, yaani huyu binti yupo USA lkn bado haelewi dunia inavyoenda. Puff daddy anauza nguo za kupitia jina Sean John wakati hana kiwanda, hajui bei ya uzi wala sindano, Jay z Roca wear nae hana kiwanda cha nguo, Kanye West ana viatu vya yeezy huyu nae hana kiwanda ila hawa wote wanamakubaliano, kwamba kila bidhaa itakayouzwa basi percent fulani inarudi kiwandani nyingine ni ya kwao. Njoo kwenye timu zote ulaya, wanafanya biashara ya jezi lkn hawana viwanda, ila kwa mkataba maalum kwa kila jezi, itakayouzwa club itachukua asilimia kadhaa na kiwanda asilimia kadhaa, ndivyo mambo yanavyoenda, man utd pamoja na utajiri wake jezi zake wanatengeza Adidas ila yy anapiga ela kupitia logo yake. Sasa cha ajabu nini diamond platnumz, anatumia umaarufu wake, kwa kutumia jina na logo yake (WCB, CHIBU, DIAMOND PLATNUMZ), kupiga ela ndio hivyo mambo yanavyoenda, ww ukiwaona Jay z, Diddy, Kanye, man utd, Madrid wanapiga ela kupitia majina na logo zao, wakati wao hawana hata hivyo viwanda vya kutengeneza hizo bidhaa. Tusiwe kama chuma, sehemu ya ubaridi basi kinakuwa cha ubaridi, sehemu ya joto kinakuwa cha moto, sometime mfuatilie vitu vinavyoenda, sio kila kitu akisema huyo mange kwenu mnaliona cha ukweli, acheni kupelekwa pelekwa. Nakusema kweli dogo anapiga ela ndefu kupitia diamond karanga, kwani anajua fursa, branding na ndio maana hata makampuni kama Vodacom, Coca cola, DSTV, redgold, safaricom yanamuamini (na usizani mpaka hizi kampuni wanakupa mkataba jua washafanya research na wamejitosheleza kwamba ela yao itarudi na thamini yao itaongezeka kupitia ww), kwa hiyo acheni huu uzushi wenu na bado dogo anapiga ela mwezi wa kumi na moja anatour yake na WCB mikoa kumi wadhamini Vodacom, sasa Pata picha dogo atapiga shillingi ngapi. TUKUBALI DOGO ANAAKILI, japo hana shule kubwa. Kuna wasanii wengine wakubwa, wanahiti lkn hata kampuni za pipi, zimeshindwa kuwaamini kwa kuwapa mkataba wa kutangaza pipi zao.
 
FURSA KWA NDUGU ZANGU WAKULIMA WA KARANGA.... sasa waweza kutuuzia karanga mbichi nyeupe zenye rangi ya kwenye picha hapo, Maarufu kama Super Quality Small size....kuna nafasi ya kununua hadi Karanga Tani mia moja (Tani 100) kwa kila Mwezi... Usafi na Ubora wa karanga zako ndio nguzo ya kwanza sisi kuweza kuzinunua karanga zako....Wasiliana nasi kwa namba hizi +255714993724 @diamondkaranga [HASHTAG]#NogewaJirambe[/HASHTAG] MAZINGATIO: 1. Karanga ndogo Nyeupe (Super Quality Small Size) 2. Ziwe Safi sana sana. 3. Zifungwe katika ujazo wa kilo 20 kwa kiloba. 4. Tunanunua kwa Bei kati ya tsh 2300 - tsh 2700 kwa kilo. 5. Maitaji yetu ni tani 100 kwa mwezi. 5. Piga simu: +255-714-993-724 -
 
Hivi karibuni msanii Diamond Platnumz alizindua bidhaa yake ya Diamond karanga huku akijinasibu na kujitamba kuwa bidhaa ni yake na ananunua karanga hizo kutoka kwa wakulima na kuziboresha kwa kuziongezea vionjo mbali mbalimbali ili kuziuza

Kutokana na tangazo lake kuwa bidhaa hiyo ni ya kwake mwenyewe iliwafanya wasanii wenzake kujitokeza kwa wingi kumpa support Diamond kwa kupost picha na video wakitumia bidhas yake ya Diamond karanga wakiwa na nia njema ya kumsuport kijana mwenzao katika biashara yake mpya.

Lakini ukweli ni kuwa hizi karanga za Diamond hazikuanza kuuzwa leo sokoni bali zina muda mrefu tu na zinatengenezwa na kampuni ya SMART Industries ambao pia ni watengenezaji wa CHAMA, so kilichobadilika hapa ni kurudishwa sokoni kwa mara nyingine zikiwa na cover la blue baada ya toleo la kwanza kutofanya vizuri sokoni hivyo ikawabidi watumie mbinu ya kumtafuta mtu maarufu wa kuzipa promo ambaye ni Diamond Platnumz kwa makubaliano maalumu

Lakini baadhi ya wasanii wenzake bila kujua mwenzao kashapiga mkwanja mrefu wa kuzipa promo, wao bila kujua wakaanza kuzitangaza kwenye page zao wakijua wanamsaidia kijana mwenzao kwenye bidhaa yake mpya tena wengi wakiwa ni wasanii wakubwa wenye majina na brand kubwa

Kumbe mwisho wa siku wanamtajirisha Muhindi ambaye ndiye mmiliki wa hii bidhaa bila kujua thamani na Brands zao ni kubwa kiasi gani

Naweza nikaonekana namchukia Diamond lakini walaa sina chuki nae bali najitahidi kuwaelimisha wasanii wasitumike kichwa kichwa huku wakilia wana majina makubwa lakini ni masikini
HAHAHAHAH..Uchawi of the first order.
Afu unakuta wewe hapo hata hela ya kula huna
hela ya bando umepewa na dadako
na unaishi kwa shemeji
 
Chibu Perfume sio yake ya Kusaga.

Karanga sio zake za muhindi.

Gari X6 sio lake la Marehemu Seki.

Nillan sio mtoto wake ni wa Marehemu wa Uganda.

Huko mbele tutakuja kusikia hata ile nyumba kule Madale sio yake ni ya Babu Tale.

hahahhaha...wewe cha kwako ni nini??? hahahahahahaha
 
Back
Top Bottom