Jamani Kuna haja ya mtaalam wa maswala ya share ktk biashara , watoe darasa humu jf, yaani huyu binti yupo USA lkn bado haelewi dunia inavyoenda. Puff daddy anauza nguo za kupitia jina Sean John wakati hana kiwanda, hajui bei ya uzi wala sindano, Jay z Roca wear nae hana kiwanda cha nguo, Kanye West ana viatu vya yeezy huyu nae hana kiwanda ila hawa wote wanamakubaliano, kwamba kila bidhaa itakayouzwa basi percent fulani inarudi kiwandani nyingine ni ya kwao. Njoo kwenye timu zote ulaya, wanafanya biashara ya jezi lkn hawana viwanda, ila kwa mkataba maalum kwa kila jezi, itakayouzwa club itachukua asilimia kadhaa na kiwanda asilimia kadhaa, ndivyo mambo yanavyoenda, man utd pamoja na utajiri wake jezi zake wanatengeza Adidas ila yy anapiga ela kupitia logo yake. Sasa cha ajabu nini diamond platnumz, anatumia umaarufu wake, kwa kutumia jina na logo yake (WCB, CHIBU, DIAMOND PLATNUMZ), kupiga ela ndio hivyo mambo yanavyoenda, ww ukiwaona Jay z, Diddy, Kanye, man utd, Madrid wanapiga ela kupitia majina na logo zao, wakati wao hawana hata hivyo viwanda vya kutengeneza hizo bidhaa. Tusiwe kama chuma, sehemu ya ubaridi basi kinakuwa cha ubaridi, sehemu ya joto kinakuwa cha moto, sometime mfuatilie vitu vinavyoenda, sio kila kitu akisema huyo mange kwenu mnaliona cha ukweli, acheni kupelekwa pelekwa. Nakusema kweli dogo anapiga ela ndefu kupitia diamond karanga, kwani anajua fursa, branding na ndio maana hata makampuni kama Vodacom, Coca cola, DSTV, redgold, safaricom yanamuamini (na usizani mpaka hizi kampuni wanakupa mkataba jua washafanya research na wamejitosheleza kwamba ela yao itarudi na thamini yao itaongezeka kupitia ww), kwa hiyo acheni huu uzushi wenu na bado dogo anapiga ela mwezi wa kumi na moja anatour yake na WCB mikoa kumi wadhamini Vodacom, sasa Pata picha dogo atapiga shillingi ngapi. TUKUBALI DOGO ANAAKILI, japo hana shule kubwa. Kuna wasanii wengine wakubwa, wanahiti lkn hata kampuni za pipi, zimeshindwa kuwaamini kwa kuwapa mkataba wa kutangaza pipi zao.