Wasanii kumpigia promo Diamond kwenye bidhaa yake ya karanga ni uzuzu wa kiwango cha juu

themagnificient

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2016
Posts
1,033
Reaction score
3,720
Hivi karibuni msanii Diamond Platnumz alizindua bidhaa yake ya Diamond karanga huku akijinasibu na kujitamba kuwa bidhaa ni yake na ananunua karanga hizo kutoka kwa wakulima na kuziboresha kwa kuziongezea vionjo mbali mbalimbali ili kuziuza

Kutokana na tangazo lake kuwa bidhaa hiyo ni ya kwake mwenyewe iliwafanya wasanii wenzake kujitokeza kwa wingi kumpa support Diamond kwa kupost picha na video wakitumia bidhas yake ya Diamond karanga wakiwa na nia njema ya kumsuport kijana mwenzao katika biashara yake mpya.

Lakini ukweli ni kuwa hizi karanga za Diamond hazikuanza kuuzwa leo sokoni bali zina muda mrefu tu na zinatengenezwa na kampuni ya SMART Industries ambao pia ni watengenezaji wa CHAMA, so kilichobadilika hapa ni kurudishwa sokoni kwa mara nyingine zikiwa na cover la blue baada ya toleo la kwanza kutofanya vizuri sokoni hivyo ikawabidi watumie mbinu ya kumtafuta mtu maarufu wa kuzipa promo ambaye ni Diamond Platnumz kwa makubaliano maalumu

Lakini baadhi ya wasanii wenzake bila kujua mwenzao kashapiga mkwanja mrefu wa kuzipa promo, wao bila kujua wakaanza kuzitangaza kwenye page zao wakijua wanamsaidia kijana mwenzao kwenye bidhaa yake mpya tena wengi wakiwa ni wasanii wakubwa wenye majina na brand kubwa

Kumbe mwisho wa siku wanamtajirisha Muhindi ambaye ndiye mmiliki wa hii bidhaa bila kujua thamani na Brands zao ni kubwa kiasi gani

Naweza nikaonekana namchukia Diamond lakini walaa sina chuki nae bali najitahidi kuwaelimisha wasanii wasitumike kichwa kichwa huku wakilia wana majina makubwa lakini ni masikini
 
Duh jaman kweli wabongo sie wachawi...yaani ajira mtaani hakuna..magu kabana kila kona but atleast dogo katoa Katanga na vijana kibao wasio na elimu na wenye elimu wamepata unafuu wa kuendesha maisha na family zao...but bado unaleta uchawi kisa utimu...acheni uchawi ....!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yan wasanii wetu hawajui au hawatak kujua kuhusu matangazo,. Mfano mzuri ni ommy dimpoz alivyopost lile kopo la vesline, ya amewatangaza vesline ila ye hajaingiza chochote.. Same to hao wanaopost diamond karanga huku wanatoka kapa wakat mwenzao dai kalipwa
 
umeongea jambo muhimu kwa wasanii wetu kujifunza...ila kwa kuwa jf na hasa jukwaa hili watu hawataki kushughulisha akili zao bali ni kumuattack mtoa mada hutaelewaka.
wasanii wanapaswa kuwa makini sana mara nyingi hufanya matangazo na kuwafaidisha watu wengine huku wao hawapati kitu bila wao kujijua.
 
Wengi humu ni vilaz.a wengine wamesomea biashara lakini hawajielewi kabisa yaani wengi hapa wanaona namuonea wivu Diamond kumbe natoa somo zuri kwa wasanii

Karanga hizi ni za kampuni ya smart ya wahindi ambayo huwa wanatebgeneza na CHAMA ukiangalia nyuma ya karatasi ya Diamond karanga utaliona jina la hiuo kampuni ya SMART company na hili ni toleo la pili cuz toleo la kwanza zilikuwa kwenye karatasi ya rangi nyekundu na zilikuwa zinauzwa sh 200, so baada ya kupoteza soko hawa smart company wakawa wametulia kwanza kulisoma game na kuangalia ni jinsi gani watairudisha hii bidhaa kwa nguvu zaidi sokoni

So wakampa deal diamond la pesa ndefu kutangaza hizi karanga kwa mgongo wa kuwa yeye ndie mmiliki ili ziuzike sana so Diamond amevuta mamilioni ya pesa kw kuitangaza hii biashara inayomilikiwa na wahindi wa smart company

Sasa hao wasanii wanaozipa promo hizi karanga wanamsaidia Diamond au wanamsaidia Mhindi?
 
Hawajitambui mkuu na ndio maana daily wanalialia wanaibiwa

K
 
Mwenzao kashakula mamilioni+ katulia tu wao wanazitangaza na hawapati kitu wanajiona wanamsaidia platnumz kumbe wanamtajirisha muhindi ambaye ndie mtengenezaji na mmiliki wa hizi karanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Struggle with your situation young nigga

Even a black folk hate to see another nigga made it..
 
Hili povu ungelitumia kuandika mradi si ungeuza au ungelisaidia taifa acha mapovu yasiyo na faida kwako fanya ya msingi kwako na taifa kama ni muhindi katumia akili ww unatoka povu tubadilike ndg zangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bi shosti upo vizuri unakaba kila kona anzia insta hadi JF aiseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…