Wasanii kushindwa kujigharamia matibabu nini tatizo?

shalet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
3,430
Reaction score
3,547
habari wadau,

Leo nikisikiliza taarifa ya habari channel msemaji wa familia ya mchekeshaji maarufu king majuto aliomba wadau wasaidie kugharamia safari ya mzee kwenda kutibiwa india sina shida kuhusu kusaidiana tatizo ni kwanini hawa wasanii wetu richa ya kufanya kazi kubwa ya sanaa kuigiza matangazo na kuishi maisha tunayoona ni ya juu ila wakipata tatizo serious kidogo tu wanaanza kutembeza bakuri.
Na nini litakuwa suluhisho la muda mrefu kwa hawa wasanii wetu waweze kujimudu hata kwa kujiunga na bima za 1m tu kwa mwaka.

All the best king majuto.
 
Ila kweli Bongo nyoso maana king majuto na marehemu small ilibidi wawe na ela chafu.
Wameanza kuigiza enzi hizo yeye majuto, small, bi chau, tupa tupa hata kabla wengi hawjazaliwa na wengine wanaoga nje
 
Mie nimesoma Tanga 1977-80, Mzee Majuto alikuwa anakuja kuigiza shuleni miaka hiyo hivyo sio wa leo au jana katika fani yake.
 
Mie nimesoma Tanga 1977-80, Mzee Majuto alikuwa anakuja kuigiza shuleni miaka hiyo hivyo sio wa leo au jana katika fani yake.
Shikamoo mkuu sijazaliwa hata kipindi hicho.
Leo Mzee ilibidi awe na ela sana
 
Ni kwa sababu usanii Tanzania haulipi, ungelipa usingewaona kina Wema na machangu wengine wa bongo movie wanajidhalilisha mitandaoni kutafuta mabwana wa kuwaweka mjini. Siku hizi mpaka wamefikia kurogana wenyewe kwa wenyewe ili wapate mabwana.
 
Wanachokipata sicho wanachokifanyia kazi. Ndio maana diamond anaonekana anajishaua lakini ana akili sana kwenye maslahi.
wengi hawana plan ya muda mrefu na maisha yao hasa kwenye uwekezaji msanii akilazwa wiki moja tarajia ataanza kuomba msaada
 
Ila kweli Bongo nyoso maana king majuto na marehemu small ilibidi wawe na ela chafu.
Wameanza kuigiza enzi hizo yeye majuto, small, bi chau, tupa tupa hata kabla wengi hawjazaliwa na wengine wanaoga nje
Kuwa/kupata hela ni jambo moja...matumizi na serving ni jambo lingine.

Hata huko kwa Wenzetu wapo watu wanalipwa mabilioni, ila baada ya muda gharama za maisha zinawaelemea.
 
Mzee Majuto ameanza kitambo nakumbuka primary miaka ya 90's alikuwa anakuja kufanya maigizo yake shuleni tanga, Cha kusikitisha mafanikio yake hayaendani na jina lake, kuna watu wamemtumiaa bila mzee kunufaika
 
Mimi nina maoni tofauti kidogo..Mimi nadhani gharama za kwenda kutibiwa india ni kubwa sana labda kufanya wasanii kushindwa kumudu sijui lakini?
 
Sekta yao hapa kwetu haipewi hadhi yake,.. matibabu nchi km india sio mchezo.
Hawa watu umaarufu wao kisanaa unachukuliwa kimaigizo sana . Serikali haina mipango mizuri juu yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…