Siungi hoja mkono, unataka kutuaminisha kwamba chanzo cha wasanii wetu kwa wingi wao kushindwa kufikia soko la kimataifa ni kushiriki kwenye kampeni za uchaguzi.? Pili unataka kutuaminisha hao wanaoandaa tuzo wanatumia shows za kampeni kupata nominees kwenye categories? Unataka kutuaminisha Huko Nigeria wasanii ndio walianzisha maandamano? Siyo kwamba wananchi walianzisha Kisha wasanii wakaunga juhudi? Ni lini wananchi wa Tanzania mumewahi kujitokeza kupinga jambo fulani lisilo la kisiasa dhidi ya serikali kuhamasisha haki itendeke? Tatizo la watanzania ni wanafiki sana mnapenda kutupia watu lawama kwa kushindwa kwenu wenyenyewe kutimiza majukumu yenu.