Wasanii mkishamaliza kuiweka CCM madarakani mkumbuke mtarudi kitaa kuganga njaa kama kawaida yenu hadi 2025

Nawakumbusha tu msije mkajisahau mkadhani CCM itaondoka na nyie kwenda Ikulu na kuendelea Kula Bata na kupewa visent mnavyodanganywa kwa Sasa.
Na mkiugua mkome kutembeza bakuli. Shuwaini nyie.
 
Wasanii wa bongo wasikuumize kichwa idadi kubwa afya mgogoro Ni swala la muda watashindwa kushuhudia waliowakana wakifurahia uongozi mpya wenye kuwatakia mema WaTz wote bila kujali vyama
Wengi watakuwa wamepotea hawatasikika tena
 
Kupitia show za CCM wanapata mpunga wa maana so ndio faida tayari au wewe ulitakaje? Mbona mnateseka Sana Wasanii kuwafanyia kampeni CCM Kama na Nyie mnawataka hao wasanii si kuwambieni Viongozi wenu wa wa Chadema walipeni wasanii
 
Hiiiiiììiiiiiiiiii.
 
Acheni ushamba

Msanii anafanya kazi na yoyote ili mradi ufike dau lake la malipo, kama una mkwanja hata Diamond unaweza kumlipa atumbuize kwenye birthday ya mtoto wako. Hio ndio ajira yao

Miezi michache iliyopita tulikuwa kwenye janga la corona nchini, hvyo wasanii wamepiga miayo sana kwakuwa hakuna show za ndani wala nje ya nchi, sasa kampeni zimeanza na wasanii ndo msimu wao wa kuvuna, kumbuka wana familia na ndugu wanaowategemea
je ulitaka wasusie show, wasusie pesa???

Kutumbuiza hakujaanza leo wala jana ni toka enzi na enzi, hawa akina Diamond na Ali Kiba hata 2015 walizunguka mikoani na CCM,,, na bado baada ya hapo wameendelea kuwa juu kimuziki

Ingia hata YouTube tafuta nyimbo ya 'Number one CCM' ya Diamond 2015 utaikuta,,, na baada ya hapo walirudi mtaani na kuachia madude na wamezidi kupaa ktk anga la muziki nchini na africa kwa ujumla
 
Nawakumbusha tu msije mkajisahau mkadhani CCM itaondoka na nyie kwenda Ikulu na kuendelea Kula Bata na kupewa visent mnavyodanganywa kwa Sasa.
Na kweli watakufa njaa, nani atalipa sh.10,000 kwenda kumwona Msanii anayeonekana bure kwenye mikutano ya CCM?
 
Acha unafki wewe mtoa mada,hivi ni lini ulilipia ili upakue nyimbo zao mitandaoni hata kwa shilingi 100 tu?
 
Na kweli watakufa njaa, nani atalipa sh.10,000 kwenda kumwona Msanii anayeonekana bure kwenye mikutano ya CCM?

Kuna vitu huwa mnajifanya hamvioni sababu mmeweka mahaba mbele na kula hata matapishi mnayotapikiana. Kabla ya kuamua kulipa hiyo 10,000 kwa ajili ya kiingilio,je ulishawahi kupakua wimbo wowote wa hao wasanii hata kwa shilingi 100 tu?
 
Acha unafki wewe mtoa mada,hivi ni lini ulilipia ili upakue nyimbo zao mitandaoni hata kwa shilingi 100 tu?
Nipakue vya Nini wakati nawaona kila siku kwenye show za bure kwenye mikutano ya CCM
 
Wapo wasanii kibao ambao wataipa Chadema na ACT. Ila wanakomaa na Magu coz ndo biashara hyo. Mfano Mpoki na Alikiba
 
Nipakue vya Nini wakati nawaona kila siku kwenye show za bure kwenye mikutano ya CCM
Kuanzia 2016 mpaka 2019 unataka kusema walikuwa kwenye mikutano ya CCM. Msijifanye wasafi kwa kukosoa kila kitu kwa mnaowaona hawafanyi kile mnachotaka. Unafki sio mzuri hata kwa wewe unayejiona una harakati.
 
Nawakumbusha tu msije mkajisahau mkadhani CCM itaondoka na nyie kwenda Ikulu na kuendelea Kula Bata na kupewa visent mnavyodanganywa kwa Sasa.
Huu ni wivu wa kipumbavu tu,maisha ya watu yanaendelea kama watu wengine duniani,huwezi zuia watu kwa matakwa ya moyo wako wa kishenzi,kila jambo hapa duniani ni maisha ya watu,kweni wangeshabikia upinzani na hao ccm wangesema kama uaemavyo wewe ungeona nini?acha watu waendelee na maisha yao we mjinga nini
 
Duuuh chama changu hiki! Mlipoulizwa mnapotoa hela za kuwalipa wasanii wote nchi nzima mkajibu wanajitolea, leo tena mmekuja na hii kuwa mlifika bei zao.

Yani mkibanwa kidogo mnajigeuza hivi, mkibanwa tena hivi mnageuka vile, mradi vurugu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…