Wasanii mliokuwa mnabaniwa na Ruge huu ndo muda wa kithibitisha kauli zenu

Point.
 

Wewe unafatilia matukio ya diamond kimuziki au unaongea kiushabiki? Dai kapiga show nyingi za nje mwaka jana bila hao clouds, na pia tuzo zilikuwa juhudi zake sio za clouds, hao clouds wangekuwa na jeuri hiyo basi wasanii wao wa THT wakiongozwa na barnaba wangekuwa mbali sana, mana kwangu mimi kwa wanamuziki wa bongofleva namkubali mno barnaba lakn mtoto wa watu pamoja na kipaji choooote hana tuzo hata moja ya kimataifa hizo show za nje ndo kabisa anaziota tu. Na ushindani wa alikiba na daimond ulikuwa unamsaidia alikiba na sio daimond means alikiba needs diamond kuendelea kusikika but diamond hamuhitaji alikiba kuendelea kutrend. Na kingine daimond amefanya wasafi festival na ikawa ya mafanikio bila hao clouds. Na unapozungumzia hizo tuzo tuambie na za alikiba alizopata recently manake its like anasubiri diamond afanye jambo na yy afatishe, dai alipoacha kujishugulisha na tuzo za kimataifa naona na yy katulia
 
Mm mwenyewe ningekuwa msanii mkubwa muda huu basi tu
 

Hata kama humpendi Diamond si kihivyo,mwaka jana Diamond alikuwa katika list ya One Africa show zote kubwa tatu.hebu nitajie 2015-2017 Diamond alikuwa na show kubwa zaidi ya hizo na kwa mwaka jana tu Diamond kapiga show zaidi ya 80 ,naweza sema ndio mwaka aliofanya show nyingi kuliko mwaka wowote ule.

Hata kama humpendi dogo yupo vizuri kutanua brand yake WCB ,mwaka jana kaanza na Wasafi Festival (Kapata na mdhamini mkubwa PEPSI) imefana mpaka Kenya wakaiomba akaenda kufanya Mombasa na Nairobi,mwaka huu mwezi wa nne MASACAT OMAN anaenda kufanya Wasafi Festival,usishanga Rwanda na Burundi wakaiomba Wasafi Festival.

Alafu lini Wizkid na Davido waka sawa na Diamond ,unatumia takwimu gani kupima hilo,Diamond hajawahi kuwa sawa na hawa watu zaidi ya kuwakaribia na si kuwa nao sawa ,alafu mziki una ups and down mbona Davido alislow karibia miaka miwili sasa hivi karudi tena.

Ushindani wa Kiba na Diamond umeua sana Bongo fleva,sababu kuna wasanii walikuwa na nyimbo nzuri lakini hakupewa nafasi huo ndio ukweli wenyewe na sasa hivi hali mbaya sana,wanampa promo Kiba na Kings music wakizani wanawakomoa WCB kumbe wanawaumiza wasanii wengine kabisa,ambao wana nyimbo nzuri,wenzao WCB wanatumia njia nyingine kupromote kazi zao ndio maana huwasikii kulalamika.
 
No mkuu sikuwa na maana mbaya WCB Ni wasanii wa Music na mimi nimewachukulia Kama sample tu maana pia wanawashabiki wengi
Na ukifuatila hao mashabiki wanawalaumu Sana clouds wakati kinachofanywa Ni sawa na wanchofanya Ea radio na Tv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mostly wasanii wanakufa kimziki naturaly, mbaya zaidi ni hali ya wao kutokuamini kuwa kila kitu kina era(period) na kikishapita hakirudi. Msanii kama dudubaya anakwambia clouds ndio waliomshusha na wewe ukaamini hivyo mimi nitapata shida na uelewa wako. Msanii ambaye alikuwa anaachia nyimbo hazinishtui then unasemaje ameshushwa? Same to mangwea, naweza kukwambia kuwa ngwea ni mmoja wa wasanii pendwa wa clouds kwa kipindi hicho, muda wote bata na watangazaji wa clouds, kuna kipindi watu walihisi kuwa hata kazi yake ya upunda wa ngada ilikuwa chini ya hao hao unaosema walimbania. Ndio maana ulipotokea msiba baada ya vidonge kumpasukia clouds walitumia nguvu na rasilimali kubwa sana watu kuwatoa kwenye kilichosababisha kifo chake. Clouds waliupromote msiba wa ngwea kama walivyoupromote wa ruge. Wasanii inabidi wajiandae kisaikolojia kwamba fans ndio wanaamua sio clouds. Era yao ikipita ni lazima watakuwa chini na wengine kutamba. Hii ipo dunia nzima, Wakina r kelly, wakina ja rule, wakina ashanti still wanaachia nyimbo huko marekani but era imewakataa, Godzila ni msanii mwenye followers wengi twitter, instagram alikuwa na followers 1.8ml it means social media tu peke yake alikuwa ana uwezo wa kuitumia na kureach pakubwa, unfotunately audience haikuwa tayari, audience ndio inaamua nani a trend, ndio inaamua pierre konki atrend kuliko fidQ, Media zinamtafuta piere kwa sababu audience inahitaji kusikia kitu kutoka kwake, Hata kwenye mziki kuna muda media zinaachana na msanii kama impact yake itapungua na atakufa natural death kisanaa
 

Ndugu yangu mbona umebandika mm as if ndo niliesema me nimewakilisha mawazo ya wengi na ya wenyewe wahusika, zaidi ya hapo mimi ni mpenz msikilizaji tu
 
Mimi nashangaa eatv/earadio hawajawahi gonga nyimbo ya harmonize&rayvany tokea watoke na hawalalamikiwi ,lakini kwa clouds ni tofauti.

Watanzania wanafiki sana.
Kabisa! Eatv hawachezi nyimbo za WCB lakini watu lawama zote kwa Clouds! Utamaduni wa kutafuta visingizio sio mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo langu sio halikuwa kuwalinganisha Alikiba na Diamond Kama ulivyoeleza hapa mimi nilikuwa najaribu kukuonyesha jinsi mziki wa Bongo fleva ulivyostack.
Tukizungumzia bongo fleva kimataifa tunazungumzia Wasanii wachache wakiongoza na Diamond.
Ukubwa wa Diamond na hits zake mwaka 2015 hadi 2017 huwezi fananisha na sasa.
Kipindi kile anafanya "tandale to the world" tour Europe alikuwa anajaza Venue walizokuwa wanajaza wakina Davido na Wizkid sasahivi wakina Wizkid na Davido wanakuwa kwenye matamasha makubwa Kama Wireless na wasanii wakubwa, yeye Diamond amestack sasahivi tamasha kubwa kafanya labda One Africa Fest ambalo hata Nandy sikuhizi anaenda.
Sijui Kama umeelewa nachojaribu kusema
Mziki wetu kwasasa umestack hausogei Kama ulivyokuwa mwanzo miaka hiyo
Bado tumestack palepale kwenye Kuna viewers wangapi YouTube wakati wenzetu Nigeria washahama


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka kusema katika media zote Tanzania Clouds ndo wana nguvu kiasi hicho? Inamaana hizo media nyingine zimeshindwa kupambana kuondoa huo umonopoly wa influence ya Clouds kwa wasanii?

Sent using Jamii Forums mobile app
Media zingine hazina system,clouds ilikuwa inafanya kazi zake ki mfumo,yaani ukiona sifuri mbili wao wanataka waione 8,redio zingine haziko hvo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ndo mana nikakuuliza umefatilia matamasha aliyofanya nje mwaka jana tena bila clouds? Ungefatilia sizan kama ugesema ame stack alijaza kumbi vibaya mno
 
Kama ni kweli, hata kutokuwepo kwake hawawezi toboa maana atakua ametengeneza mfumo ambao utaendelea na utendajikazi hata asipokuwepo.
 
Sasa ukiwa na kipaji mtu akakikwamisha ukakwama, pale akifa yeye si ndo muda wa kuonesha kipaji chako?? Watumie hao wasiokubania kuonesha kipaji chako. Maana kipaji hakipotei, otherwise labda kama ulikuwa unataja upewe upendeleo (favour) kutoka kwa marehem

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo mana nikakuuliza umefatilia matamasha aliyofanya nje mwaka jana tena bila clouds? Ungefatilia sizan kama ugesema ame stack alijaza kumbi vibaya mno
Mkuu kukuwa namaanisha kupata washabiki wapya mfano mwaka jana diamond kafanya matamasha maeneo Yale Yale ya miaka yote
Tanzania
Kenya
Rwanda
Mayyote
Oman
Dubai
London
ilitakiwa kwa Sasa kuonyesha mziki umekuwa anafanya maeneo mapya Kama Ivory coast, Senegal,Togo, South Africa, na kwengine
Mfano mzuri Ni wakina Davido na Wizkid sasahivi wanafanya matamasha hadi Bahamas, Jamaica, tridand and tobeco, Maleysia.

Point yangu ilikuwa hiyo wakina Diamond , Vanessa mdee, Alikiba wanatakiwa kufanya show maeneo mapya Kama kweli mziki wetu unaendelea kukuwa na haujastack

Sio kila siku ukitoa mziki tranding Ni Kenya , Tanzania na Uganda


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakin muda nao una matter,watu tunatofautian tunavyo handle matatizo yetu.

Hivi unakipaji ,unatoa ngoma kali ila kuna watu wanakukazia,hii imepelekea hata baadh ya wasanii kua stressed ,sasa ukishakua na stress kuna kipaj tena hapo?

Wengi tu wameishia kufanya mambo nje ya mzik,wengne wkawa walevi kupindukia,wengne wakaingia kweny madawa..unapo mbania msanii basi unamweka kweny mazingira hatarishi sana.

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
 
Vitapatikana visingizio vingine,just wait and see.
 
Tatizo lako Dogo uanamchukia Daimond kafanya show Mozambique,Madagascar ,Malawi,Zambia,Zimbabwe,Namibia,DRC,US,Sweeden,Denmark,Uganda nk nchi nchi hizi za Kusini mwa jangwa la Sahara Diamond kabakisha inchi moja tu ambayo hakupiga show nayo ni Angola.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…