Wasanii wa bongo moves na Vichekesho Tànzania(comedy)mpo ktk ubora ila mna kasoro moja kubwa...

Wasanii wa bongo moves na Vichekesho Tànzania(comedy)mpo ktk ubora ila mna kasoro moja kubwa...

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2018
Posts
448
Reaction score
409
Mimi ni mdau hasa na mfuatiliaji wa kazi za wasanii mbalimbàli duniani,tangu utoto wangu nimeangalia kazi za ndani za wasanii na za nje toka Marekani,Ulaya,India,China na hata Korea zisizo na idadi tena nilianzia kwenye sinema za vibatari na sinema za kuganda(Picha mnato).

Nikiwa chuo kikuu nilisoma na muigizaji Pastor Myamba japo alikuwa mbele na Mara kadhaa alifika geto kwetu Ubungo tulipopanga hivyo nawajua wasanii

Pia nimeshawashudia wasanii mbalimbali live kwa Kuonana barabarani kama marehemu King Majuto-Mabibo hostel,Senga,Kingwendu alipotembelea Meatu,Joti na Mpoki walipokuwa kinda hawajui hata kama watatoka,walipokuwa stejini jijini Dodoma na Ray Kigosi alipokuwa ktk action ya kulikimbiza gari Ubungo na kadhallka.

KASORO YAO:
Kasoro yao kubwa ni Uchawi,mnalogana sana,tofauti na Hollywood,Nollwood,Bollywood ambako wasanii wanadumu


Huku wasanii wanavipaji lakini inabidi wajifanyishe kuigiza chini ya kiwango wakiogopa kuonewa wivu na hatimae kulogwa.

Ona mmesha mloga Steve Nyerere miguu,mnaipasha moto tu hebu mfungueni,eti kisa kumuonea wivu alipokuwa mwenyekiti wenu.

NB:sijawahi kumuona hata msanii mmoja wa kike,ushauri muwe mnaenda hata Mlimañi City mnakaa kidogo kuliko kutoka viwanja usiku pekee kama bundi

Pia makampuni ya simu Ttcl,Vodacom,Tigo,Hallotel,Airtel na Zantel waleteni wasanii mikoani mnaweza anzisha hata shindano la wadada waliojaliwa kuzungusha nyonga au kukata mauno maana wamekuwa adimu,wakalisimamia nyie mnawapendelea Bongo Fleva tu,not fair!

Niliewaandikia msijaribu kuniloga hamtaweza ni ngoma nzito

instagram:kaukwaju
 

Attachments

  • IMG_20180915_221302_546.jpg
    IMG_20180915_221302_546.jpg
    8.2 KB · Views: 35
mods naombeni kibali cha dk 5 tu cha kumtukana mleta mada...

dk 5 tu zitanitosha nikimtukana baada ya hapo mnipige BAN
 
Back
Top Bottom