JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 2,118
- 4,863
Hakuna vitu sipendi kama kuona video ya mziki msanii wa bongo ana rusha rusha mikono kwa ishara za kuiga kwa wasananii wa hip-hop wamarekani bila kujua kama zina maana au laa mwenyewe akijua ni fasheni.
Huu ushamba hata wasanii wa Nigeria kina davido wanao utakuta video ya afrobeat mtu anatupia gang signs bila kujua hata ni vitu gani kisa tu kaona kina lil wayne au quavo katupia kwenye video yake na yeye anaiga.
Nawapongeza sana wasanii wa Kwaito hawa jamaa wako tofauti sana kila siku wanabuni vitu vipya hadi leo wana amapiano na style zao za kucheza na ku act kwenye video hawaigi marekani hata kidogo.
Wasanii acheni kuigiza kwenye video kurusha rusha mavidole mnajichoresha, wenzenu kule ukiona katupia vidole style flani ujue anatuma ujumbe kwa watu wa mji flani ambao ni members wa genge flani hata wenyewe wakiona hizo video msanii wao kawawakilisha wanalipuka kwa furaha
Sasa wewe uko afrika huku unatupia mividole kwa sign hata huzijui wenyewe wenye magenge yao wakiona video yako wanakushangaa mwisho wa siku utajikuta umeenda kwenye mji huko marekani ukapigwa risasi kwa kuonekana wewe ni member wa genge la maadui zao bure.